Bajeti ya kuagiza noah Japan

Udochi

JF-Expert Member
Jul 25, 2015
782
1,056
Kwema waheshimiwa?

Kwenye mada,

Pamoja na kipato kidogo,
Nimehangaika kwa takribani miaka mitatu Kutafuta riziki kwa njia halali Kabisa ili niweze kutimiza lengo langu la kununua TOYOTA NOAH,
Ili inisaidie kwa matumizi ya familia,
Mizunguko binafsi,
Na pia safari za mikoani kama vile Mbeya na Mtwara japo Mara mbili kwa mwaka.

LENGO:
Kwa Kuwa Mimi ni mgeni Kabisa Kwenye Haya mambo (sijui taratibu na gharama za kuagiza gari hadi kufika bandarini kulitoa hadi nyumbani),
Naombeni mwongozo,
Kwa bajeti yangu ya mil. 9

Naweza kuagiza NOAH ambayo haijachoka kutoka Japan plus kuitoa bandarini
Na Ku_clear masuala ya TRA na kuanza kuitumia?

Pia
nisaidieni Kwenye maswala ya injini, chassis, model, mwaka wa kutengenezwa kwake na yenye unafuu wa kula fuel.

Natanguliza Shukrani.
 
Kwa budget ya 9M huwezi kupata noah. Sasa hiv unahitajika kuwa na kuanzia 14m ndio unaweza kupata noah ya 1999, model SR40
 
Kwa budget ya 9M huwezi kupata noah. Sasa hiv unahitajika kuwa na kuanzia 14m ndio unaweza kupata noah ya 1999, model SR40
Daaaaah!

Hapo sasa yabidi niongeze miaka miwili mbele kufaiti kama tutajaaliwa uzima.
 
milion 9 hata vitz za kisasa haupati, dola moja inacheza kuanzia 2180 mpaka 2240..

kwa ushauri wangu tu andaa milion 14 - 17 kuagiza noah na kodi yake..
 
milion 9 hata vitz za kisasa haupati, dola moja inacheza kuanzia 2180 mpaka 2240..

kwa ushauri wangu tu andaa milion 14 - 17 kuagiza noah na kodi yake..
Hapo nimekuelewa mkuu,
ila nasikia kwa watumishi wa umma Kuna punguzo kidogo pale bandarini.

Katika 14M yaweza pungua kiasi Gani?
 
Pole mkuu, kwa 9 m kamwe hupati labda ununue used toka kwa MTU alietumia, Mimi mwaka Jana Jan niliagiza kwa 11.5
 
Kwa website ya bewarded.com ni cheap kidogo lakini website ya buynpick24 zina quality ila bei Ndio iko juu, embu zipitie kidogo
 
Be forward unapata sana tu. Nimecheki noah ya mwaka 2007 mwezi huu huu. Ina maana kodi na port charges zinaweza kuzidi CIF?
bei ilikuwa CIF Dola 2300 (almost million 5)
kwa bei hiyo na-assume kodi Na charges zingine million ni kama 3.9 au 4.
Kwa dharura weka 10 kabisa unapata Noah yako safi ya mwaka 1999
 
Kodi na port charges huwa zinazid CIF mara nying tu, kod huwa wanathaminisha kwa bei zao sio bei ulonunulia wewe gari
 
Vip Wakuu Mark X ya 2007 mpaka 2010! naweza pata kwa million 13?
 
Bajeti ya Noah Seper Extra Limo from Japan to nyumbani kwako ni 13 mil. Niliagiza last yr mkuu .
 
Kwema waheshimiwa?

Kwenye mada,

Pamoja na kipato kidogo,
Nimehangaika kwa takribani miaka mitatu Kutafuta riziki kwa njia halali Kabisa ili niweze kutimiza lengo langu la kununua TOYOTA NOAH,
Ili inisaidie kwa matumizi ya familia,
Mizunguko binafsi,
Na pia safari za mikoani kama vile Mbeya na Mtwara japo Mara mbili kwa mwaka.

LENGO:
Kwa Kuwa Mimi ni mgeni Kabisa Kwenye Haya mambo (sijui taratibu na gharama za kuagiza gari hadi kufika bandarini kulitoa hadi nyumbani),
Naombeni mwongozo,
Kwa bajeti yangu ya mil. 9

Naweza kuagiza NOAH ambayo haijachoka kutoka Japan plus kuitoa bandarini
Na Ku_clear masuala ya TRA na kuanza kuitumia?

Pia
nisaidieni Kwenye maswala ya injini, chassis, model, mwaka wa kutengenezwa kwake na yenye unafuu wa kula fuel.

Natanguliza Shukrani.
Mtafute huyu MTU kwa WhatsApp.... 0655901110 utapata maelezo mazuri tu... Wasikukatishe tamaa... Utapata.
 
Back
Top Bottom