Bajeti ya ku-copy na ku-paste | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bajeti ya ku-copy na ku-paste

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Vox Populi, Jun 14, 2012.

 1. Vox Populi

  Vox Populi Member

  #1
  Jun 14, 2012
  Joined: Oct 23, 2010
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  BAJETI YA TANZANIA HUANDALIWA WAKATI HAZINA HAINA HELA, NA HUWA HAITEKELEZEKI, NI BAJETI YA KISIASA ZAIDI KULIKO UHALISIA, PAMOJA NA KUSOMWA KWA MBWEMBWE LAKINI HAITEKELEZEKI. HII NI KUTOKANA NA... KUTOKUWA NA UCHUMI SHIRIKISHI, UCHUMI WA NCHI KWA TANZANIA HUPIMWA KWA KUANGALIA TU TABAKA LA WALIONACHO. NI MPAKA PALE TUTAKAPOKUWA NA PEOPLE' CENTRED ECONOMY, NDIPO BAJETI ITALENGA MAFANIKIO. NI AJABU... KUPANGA BAJETI MATHALANI YA MAENDELEO WAKATI KULE VIJIJINI AMBAKO NDIKO WANAISHI WAZALISHAJI MALI HAKUNA UNAFUU WOWOTE. BAJETI HII HAITAWEZA KUWA YA MATUMAINI YOYOTE KWA MTANZANIA. Bajeti ambayo hutegemea stika za magari, bia na soda, huku ikiacha misamaha kedekede ya kodi kwa makampuni na mashirika ambayo kimsingi yangeweza kuiondoa nchi ktk umasikini uliokithiri. Bajeti hii egemezi katika ni tegemezi mno, na ni aibu kwa serikali na nchi kubwa yenye raslimali nyingi kuendelea kuwa tegemezi. HII INANIKUMBUSHA MSEMO WA WANAZUONI KWAMBA "HUWEZI KUMFUNDISHA MBWA MZEE MBINU MPYA". HAKUNA JIPYA, BAJETI IMEJALI ZAIDI MATANUZI YA WAHESHIMIWA. HUKO KWENYE EXPENSE ACCOUNT, NDIKO WIZI MKUBWA UNAKOFANYIKIA, KWANI AKAUNTI ZA NAMNA HIYO KWA ASILI HUISHA PESA KILA MWISHO WA MWAKA WA BAJETI. WAZIRI KWA MFANO AMEZUNGUMZIA KUONGEZA KODI YA USAJILI WA MAGARI MPAKA TSHS. 5000000/- KAMA CHANZO MOJAWAPO CHA PATO LA TAIFA, HUU NI UHUNI, NA KEJELI KWA MAENDELEO YA TAIFA, YAANI HANA HATA AIBU, KWANI NI WATU WANGAPI ANAFIKIRI WANASAJILI MAGARI YAO HIVYO KWA MAJINA AU NAMBA WANAZOPENDA WAO, HUU NI UZANDIKI, HATUPASWI KUVUMILIA UHUNI KAMA HUU. HII BAJETI INAIONESHA MAISHA YATAZIDI KUWA MAGUMU ZAIDI KILA SIKU AU MIAKA INAVYOZIDI KUSONGA. SERIKALI HAINA DHAMIRA YA DHATI YA KUWAKOMBOA WANANCHI KUTOKANA NA LINDI LA UMASIKINI. NA KUONGEZA USHURU KWA MATUMIZI YA SIMU MATHALANI, NI NANI SASA ATATUMIA SIMU KUTAFUTA WATEJA HUKU YEYE MWENYEWE AKIWA NA KIJIMTAJI KIDOGO? ETI CD NAZO ZIMEWEKEWA USHURU ILI KUDHIBITI WA WIZI WA KAZI ZA WASANII, HII NI FIKRA POTOFU KABISA, IVI HAWAONI KWAMBA BEI YA UZALISHAJI WA KAZI YA USANII PIA ITAONGEZEKA NA KUWAFANYA WASANII WADOGO WASHINDWE KUZALISHA KAZI ZAO. INA MAANA SERIKALI IMESHINDWA KABISA KUSIMAMIA ULINZI WA KAZI ZA WASANII ISIPOKUWA KWA KUPANDISHA BEI YA CD!!!!! AWKWARD !!!!! HII INANIKUMBUSHA BAJETI YA 2011/2012 AMBAPO ETI SERIKALI ILIAMUA KUPANDISHA BEI YA MAFUTA YA TAA ILI KUTHIBITI UCHAKUCHUAJI. HII NI UTHIBITISHO KWAMBA SERIKALI HII IMEKOSA DIRA.
   
Loading...