Bajeti ya Kenya ndo kubwa East Africa,kizuri zaidi..

Naamini watakuwa werevu na kukaa chini kudesign laptop special kutokana na mahitaji ya watoto wa kenye kiujumla na Africa. Sio lazima ziwe hizi tulizo zoea hata zile za UN zilikuwa design special kwa ajili ya watoto na zilikuwa cheap. Nataka na wao waende step zaidi ya zile ikiwezekana hata assembling ifanyike Kenya kwani hizi ni nyingi na wanauweo wa kula dili Uganda, sudan, Tanzania na nchi zingine africa na kujikuta wanakiwanda chao.
Mkuu hili lafanyiwa kazi na tayari yupo Mkurugenzi wa Microsoft kwa ajili hiyo.Kutakuwa na Special kwa watoto wa Shule ya Msingi.Kamati imeshaundwa na miundomsingi yote inafanyiziwa kazi.Project itatoboa wala usiwe na shaka.
 
kiujumla bajeti za kenya na rwanda zina uwazi na ubunifu katika vyanzo na matumizi,njoo 255 sasa...mtu yeyote anaweza iandaa kwasababu vyanzo ni vilevile tangia nanyonya hadi leo hii nna mvi kadhaa kichwani.
SHANTA

Lakini mwaka huu wamevumbua chanzo kipya:

Cha kuongeza gharama za matumizi ya Simu za mikononi. Wakati TCRA wanasema wana mkakati wa kupunguza gharama Serikali nao kwa upande mwingine wanaongeza na hadi matumizi ya M-pesa, Tigo Pesa nk.

SHAME ON YOU AND YOUR POOr BADGET.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
kweli tz kila k2 tambararee, hivo hiyo diff ya 10 trilion tutailipa vipi? a very big gap....
 
Kenya wananchi wake wako aggressive... Tatizo ni letu sote waTanzania sio Viongozi tu!

Mkuu umenifurahisha sana.

Hawa viongozi wa Tanzania, haya magamba yanayoongoza taifa letu kwa sasa, ni matokeo ya sisi watanzania kuwa watu wa kuitikia 'ndiyo mzee' bila kujiuliza. Kuna watu wanaimba kwa sauti kubwa na kutetemeka, kutokwa na povu kusifia ccm bila ya kutaka kuangalia na kukemea uovu na uozo uliokithiri kwenye utendaji wa kazi. Tumebakia kuimba 'nchi yetu ni nchi ya amani', bila hata kutathmini nini maana ya amani. Hakuna amani penye uonevu, hakuna amani penye matabaka, hakuna amani penye njaa na dhuluma.

Kama Tanzania ni nchi ya amani kama tunavyodai, kwa nini nyumba zetu tunajenga na kuta ndefu na kuweka mageti na grill kama tuko jela? Mtu unajenga nyumba yako mwenyewe halafu unajifungia na makufuli, unamwogopa mpaka jirani yako, lakini unakuwa wa kwanza kuimba wimbo usioujua wa 'Tanzania ni nchi ya amani' kisa ccm na serikali ya jk wamesema hivyo?

Siku kadhaa zilizopita nilihudhuria semina moja ambayo mtoa mada aliongelea vizuri sana kuhusu hili. Akasema 'uongozi ni taswira (reflection) ya jamii'. Uongozi mbovu tulio nao ni matokeo ya jamii yetu kuharibika kiasi cha kufikia kuwaweka watu wabovu madarakani. Ni sisi sote, (mimi, wewe na yeye) ndiyo tuliochangia kwa kura zetu, ama kwa kutokuwa makini kuzilinda kura zetu ama kutosema ukweli pale tunapopaswa kusema ukweli, tukawapa madaraka ccm ambao wameendelea kutudhulumu na kutudhalilisha. Watanzania tunapaswa kutembea vifua juu, sisi ni taifa kubwa, siyo sisi kuwa kila siku watu wa kujilinganisha na mataifa madogo madogo kama Kenya ambayo eti sasa tunabaki kuyasifia.

Tuamke watanzania, tudai kilicho chetu kwa nguvu zote mpaka kieleweke! La sivyo tutabakia kuwa wasindikizaji tu kwenye safari ya maendeleo tunaambulia kuona taa za nyuma za magari kwenye barabara ya maendeleo wakati tumeachwa mbali...
 
Pale Watanzania watakapogundua kuwa CCM imeshindwa na waamue kuchukua maamuzi ya kuchagua chama kingine mbadala ndio tutaweza kuendelea mbele
 
wakenya washagundua sasa hivi ni science and information age,wameshaanza kuwekeza at primary level.tuamke sio masikhara watoto wetu watakosa ajira mbele uko
 
Pale Watanzania watakapogundua kuwa CCM imeshindwa na waamue kuchukua maamuzi ya kuchagua chama kingine mbadala ndio tutaweza kuendelea mbele

trueeeeeeeeeeeeee.tunatakiwa kuogopwa na wanasiasa na sio sie tuwaogope wenyewe
 
Ongereni kenya sisi tanzania viongozi wetu wamechapa usingizi hawaoni kama bajeti ndogo wanabaki kupiga makofi kama mazuzu
 
Mkuu hili lafanyiwa kazi na tayari yupo Mkurugenzi wa Microsoft kwa ajili hiyo.Kutakuwa na Special kwa watoto wa Shule ya Msingi.Kamati imeshaundwa na miundomsingi yote inafanyiziwa kazi.Project itatoboa wala usiwe na shaka.

BIG mistake mkuu, Huwezi kuwaandaa vijana kujifunza kwa kutumia ubapari unatgemea nini baadae,
Walitakiwa waende OPEN SOURCE wakachukue LINUX waichakachue watoke na kitu yao(OS) au yetu ya Afrika mashariki na iende kw ajina la UHURU kama South walivyotoka na UBUNTU.

Swala la Hardware wangenda china na kupata hardware nzuri tu kwa ajili ya kubeba hiyo OS na itakayo tengenezwa special kwa ajili ya mazingira yetu ya kiafrica.
kiasi laptop itumike vijijini na kwenye mavumbi na matope na iendelee kudumu.
 
Mkuu umenifurahisha sana.

Hawa viongozi wa Tanzania, haya magamba yanayoongoza taifa letu kwa sasa, ni matokeo ya sisi watanzania kuwa watu wa kuitikia 'ndiyo mzee' bila kujiuliza..

Yes, Viongozi wote waKisiasa wamepigiwa kura, means those are what our wananchi saw them as best.... from us a community.

Mfano Mzuri... Mh. Lema ndio best and role model ya viongozi wa Bongo... Very sad.

Kila ki2 kinatokana na sisi tulivyo.
 
BIG mistake mkuu, Huwezi kuwaandaa vijana kujifunza kwa kutumia ubapari unatgemea nini baadae,
Walitakiwa waende OPEN SOURCE wakachukue LINUX waichakachue watoke na kitu yao(OS) au yetu ya Afrika mashariki na iende kw ajina la UHURU kama South walivyotoka na UBUNTU.

Swala la Hardware wangenda china na kupata hardware nzuri tu kwa ajili ya kubeba hiyo OS na itakayo tengenezwa special kwa ajili ya mazingira yetu ya kiafrica.
kiasi laptop itumike vijijini na kwenye mavumbi na matope na iendelee kudumu.

well that's what techies are complaining about but it seems uhuru preferred to go for tried and proved systems such as it is in south American nations like Colombia where the one laptop per child has been a much touted success. the laptops are designed in the simplest of ways and can be manually charged too.the choice of Microsoft is probably because majority of users are already well versed with it than theu are with Linux thereby making it easy for even parents to help their kids to learn.
 
Mkuu umenifurahisha sana.

Hawa viongozi wa Tanzania, haya magamba yanayoongoza taifa letu kwa sasa, ni matokeo ya sisi watanzania kuwa watu wa kuitikia 'ndiyo mzee' bila kujiuliza. Kuna watu wanaimba kwa sauti kubwa na kutetemeka, kutokwa na povu kusifia ccm bila ya kutaka kuangalia na kukemea uovu na uozo uliokithiri kwenye utendaji wa kazi. Tumebakia kuimba 'nchi yetu ni nchi ya amani', bila hata kutathmini nini maana ya amani. Hakuna amani penye uonevu, hakuna amani penye matabaka, hakuna amani penye njaa na dhuluma.

Kama Tanzania ni nchi ya amani kama tunavyodai, kwa nini nyumba zetu tunajenga na kuta ndefu na kuweka mageti na grill kama tuko jela? Mtu unajenga nyumba yako mwenyewe halafu unajifungia na makufuli, unamwogopa mpaka jirani yako, lakini unakuwa wa kwanza kuimba wimbo usioujua wa 'Tanzania ni nchi ya amani' kisa ccm na serikali ya jk wamesema hivyo?

Siku kadhaa zilizopita nilihudhuria semina moja ambayo mtoa mada aliongelea vizuri sana kuhusu hili. Akasema 'uongozi ni taswira (reflection) ya jamii'. Uongozi mbovu tulio nao ni matokeo ya jamii yetu kuharibika kiasi cha kufikia kuwaweka watu wabovu madarakani. Ni sisi sote, (mimi, wewe na yeye) ndiyo tuliochangia kwa kura zetu, ama kwa kutokuwa makini kuzilinda kura zetu ama kutosema ukweli pale tunapopaswa kusema ukweli, tukawapa madaraka ccm ambao wameendelea kutudhulumu na kutudhalilisha. Watanzania tunapaswa kutembea vifua juu, sisi ni taifa kubwa, siyo sisi kuwa kila siku watu wa kujilinganisha na mataifa madogo madogo kama Kenya ambayo eti sasa tunabaki kuyasifia.

Tuamke watanzania, tudai kilicho chetu kwa nguvu zote mpaka kieleweke! La sivyo tutabakia kuwa wasindikizaji tu kwenye safari ya maendeleo tunaambulia kuona taa za nyuma za magari kwenye barabara ya maendeleo wakati tumeachwa mbali...

Kila mtanzania angekua analielewa hilo hii nchi isingekua tofauti na nchi za Asia kama Singapore samahani ashakum si matusi huwa naamini hii nchi imejaa matahira na umasikini tulionao tunastahili kwasababu hatuna akili
 
Bajeti hizo zilizotangazwa na mawaziri wa fedha wa nchi hizo sambamba na ile ya Tanzania, ni za Uganda, Rwanda na Kenya ambayo iliongoza kwa ukubwa wa bajeti.

Bajeti hizo zilitofautiana kwa kiasi kikubwa kutokana na mahitaji na vyanzo vya mapato kwa kila nchi.

Mwelekeo wa bajeti hizo pia umelenga kuongeza mapato kupitia vyanzo vya ndani kwa kuongeza ushuru na kodi kwenye vileo, vyombo vya usafiri na bidhaa za anasa.

Kenya Sh28.5 trilioni

Waziri wa Fedha wa Kenya, Henry Rotich alisema kwamba Bajeti ya nchi hiyo kwa mwaka wa Fedha 2013/14 itafikia Sh1.5 trilioni za Kenya (sawa na Sh28.5 trilioni za Tanzania).

Bajeti hiyo ilisomwa jana bungeni jijini Nairobi, ndiyo ya kwanza kwa Rais Uhuru Kenyatta aliyechukua madaraka hivi karibuni.

Moja ya ameneo muhimu yaliyopewa kipaumbele katika bajeti hiyo ni elimu, ambapo Sh17.4 bilioni (Sh330.6 bilioni za Tanzania) zimetengwa kwa ajili ya kukamilisha mkakati wa Serikali ya Jubilee wa kununua kompyuta ndogo 1,300,000 kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi.

Wewe nafikiri utakuwa kilaza! Na hauna akili hata kidogo!
Kenya ndio nchi yenye Uchumi mkubwa kuliko nchi zote na ndio ina Ngedere wengi karibu sawa na Tanzania, sasa ulitegemea wawe na Bajeti ndogo kuliko ya Rwanda au Burundi?
 
Laptop 1,300,000 kwa ajili ya wanafunzi wa Primary?? Huku kwetu bado serikali ya CCM inajiuliza jee kuna mitaala au hakuna? Jee title ya kitabu iwe Jiografia au Jogorafia? Hili taifa ni la ajabu sana,Msigwa alisema tatizo ni kuruhusu akili ndogo kuongoza akili kubwa.
Kwa ukweli kabisa tunatia aibu kama taifa. Rasilimali tulizonazo hapakuwa na sababu ya jirani zetu kutuacha mbali kimaendeleo ila kwa vile tuna Viongozi dhaifu,Bunge lililo jaa wabunge wa hovyohovyo na Chama kinachotawala kilicho jaa upuuzi hatuwezi songa mbele bali tutaenda mbele hatua 7 na kurudi nyuma 9.

inauma sana
 
Back
Top Bottom