Bajeti ya Elimu kugomewa na wabunge wa CCM?

ila tuache masihara ualimu bongo bahati mbaya, Yaani mtoto wako bora umpeleke veta mapemaaa kuliko kumpeleka A level then university akasome Bsc ed/ Baed
Mpeleke veta sasa aje mtaani apate vibarua vya kurekebisha umeme alipwe na mwalimu Ali
 
Tutakufa naye sahani moja na huo ubunge atausikia tu tutampiga kila kona
Nilivyo muelewa ni kwamba pamoja na kuwa mbunge huyu anapambana kuungamkono kutopitisha bajeti kama serikali haitoahidi kuwalipa walimu wa serikalini madai yao... Yeye binafsi hajawalipa walimu wa shule zake binafsi na wakidai maslahi yao anatishia kuwafukuza kazi!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbunge huyu amezoea kutudhurumu lakini sasa basi ,pamoja na kutufukuza ila tutamwonyesha
Malalamiko yenu walimu ni ya msingi. Kuna watu wanapenda dhuluma, ukidai haki yako unapewa vitisho au kufukuzwa kazi ila kwa uandishi wako nina mashaka kama wewe ni mwalimu kweli. Kama wewe ni mwalimu nawapa pole wazazi unaowafundishia watoto wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Atakuwa amewapa pesa wabunge wenzake wamtetee ila Mungu yupo
Anaangalia maslahi yake binafsi badala ya maslahi ya nchi. Ninachojua shule binafsi, wanafunzi wanalipa ada ya muhula kabla ya kwenda shule na wanaenda na pay-in slip kuonesha malipo.

Kwa maana hiyo, ada zipo shuleni na walimu wa shule hizo wanatakiwa kulipwa na shule na sio Serikali. Je, shule hizo zinawalipa walimu wao kupitia nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa Kuna hoja sijaielewa. Yaani huyu mbunge kwanza hajawalipa mshahara wafanyakazi wake.

Pili anataka kwenda bungeni kupinga bajeti ili serikali iwalipe ruzuku walimu ili naye awe mnufaika kwa shule zake ( yaani kwa manufaa yake binafsi)

Tatu ameanza kuwapa hela wabunge wenzake waunge mkono hoja ya kutopitisha bajeti ila ameshindwa kuwalipa wafanyakazi wake.

Kama haya yana ukweli kuna shida kubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom