Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,495
Rais wa Jamhuri ya watu wa Kenya leo amepokea ripoti ya namna ya kukuza kilimo cha mirungi ili kiongeze faida na kuchangia pato la Wakenya na kutoa ajira kwa watu wake.
Katika bajeti iliyopendekezwa wiki iliyopita, Serikali nchini humo imetenga KSh 1.2 Bilioni sawa na zaidi ya Bilioni 20 za Kitanzania katika kukuza sekta hio ya kilimo cha mirungi.
Pamoja na hilo Kenyatta amewahakikishia wakulima wadogo na wa kati kuwapatia mikopo kupitia taasisi mbali mbali za kifedha na kuwawezesha kwa mitaji ya kuanzia ili kuboresha kilimo hicho.
" I have Received a report containing recommendations to improve the profitability of miraa farming.
I Directed release of Sh1.2 billion to promote miraa after task force presented report."
Ni wakati sasa Watanzania kuangalia upya sera yetu ya dawa za kulevya na kujifunza kutoka kwa majirani zetu.