ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 620
- 1,543
Utekelezaji Duni wa Bajeti ya 2016/17 na Kasma Ndogo ya Bajeti ya 2017/18 Unaua Ndoto ya 'Tanzania ya Viwanda'
[Sehemu ya 1 ya Hotuba ya ndugu Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto (MB) kuhusu Bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa mwaka 2017/18]
Mheshimiwa Spika
Leo Bunge lako tukufu, kwa mara ya pili tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani, linajadili na hatimaye baada ya mjadala wa siku 2 kuidhinisha fedha kwa ajili ya kuwezesha Wizara ya Viwanda, Biashara ya Uwekezaji kutekeleza majukumu yake kwa mwaka ujao wa fedha.
Kwa Serikali ya awamu ya tano, Wizara hii ndiyo wizara mama, ahadi ya msingi ya serikali hii ilikuwa ni 'Tanzania ya Viwanda', sisi humu bungeni tunao wajibu wa kuhakikisha tunaibana serikali ili itimize ahadi yake hii ya msingi.
Kipimo sahihi cha kuangalia mwenendo wa utekelezaji wa ahadi hiyo ni kuangalia utekelezaji wa bajeti ya wizara hii na pia mwelekeo wa hali ya uchumi, hasa kwenye eneo la uzalishaji viwandani. Mwaka jana, wakati wa kikao cha bajeti ya kwanza ya serikali hii (bajeti ya 2016/17), Wizara hii iliomba jumla ya shilingi bilioni 81. Shilingi bilioni 40 zikiwa ndio fedha za miradi ya maendeleo.
Kwa masikitiko makubwa kabisa, nimevunjwa moyo mno na hali ya utekelezaji wa bajeti ya wizara hii 'mama', hali hii inakatisha sana tamaa mno, na inafuta matumaini yote waliyokuwa nayo wananchi wetu juu ya ujio wa 'Tanzania ya Viwanda'. Kwa mujibu wa taarifa ya Kamati, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji imepata asilimia 18 tu ya fedha zote ilizopitishiwa katika bajeti ya 2016/17. Utekelezaji huu wa bajeti wa serikali kwa asilimia kiduchu hauonyeshi kabisa uwezekano wa kuifikia Tanzania ya Viwanda katika siku za karibuni.
Si hivyo tu, hata kasma ya bajeti ya wizara hii kwa mwaka huu mpya wa fedha wa Serikali (mwaka 2017/18) haileti matumaini, katika wakati ambao utekelezaji wa bajeti ya mwaka jana umekuwa ni aslimia 18%.
Kwangu utekelezaji huu kiduchu wa bajeti ya mwaka jana, pamoja na kasma hii ndogo ya bajeti ya mwaka huu ni ishara ya ugumu wa utekelezaji wa ndoto ya Tanzania ya Viwanda. Ni vema serikali ilieleze bunge juu ya hali hii ya utekelezaji duni wa bajeti ya wizara hii nyeti pamoja na kushuka kwa makadirio ya matumizi kwa kiwango hiki, nataraji Serikali itakuwa na maelezo ya kutosha kuhusu hili.
Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Mbunge - Kigoma Mjini (ACT Wazalendo)
Bungeni Dodoma
Mei 17, 2017