Bajeti hii inamsulubu mwananchi wa kawaida

Getstart

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
6,658
2,235
Serikali jana iliwasilisha Bungeni mapendekezo yake kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2013/14. Katika mapendekezo hayo, Serikali imepanga kutumia Sh18,248,983 trilioni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na ya maendeleo. Kwa tafsiri yoyote ile, bajeti hiyo inaonyesha bayana kwamba sio endelevu, kwani kati ya fedha hizo, Sh12,575 trilioni zitakuwa za matumizi ya kawaida wakati Sh5,674 trilioni tu ndizo zitatumika katika miradi ya maendeleo.

Matumizi hayo ya kawaida yanajumuisha shughuli zisizo za uzalishaji, zikiwamo mishahara ya watumishi wa Serikali, taasisi na wakala za Serikali, Mfuko Mkuu wa Serikali na kile kinachoitwa “Matumizi Mengineyo” ya Sh4.5 trilioni. Kwa maneno mengine, hii ni bajeti ya matumizi na sio ya maendeleo na haionyeshi dhamira ya Serikali ya kumkwamua mwananchi wa kawaida kutoka katika dimbwi la umaskini.

Matarajio makubwa ya Watanzania yalikuwa kuona bajeti ya kuwaletea unafuu katika maisha yao ya kila siku, bajeti yenye mwelekeo wa kuwapunguzia umaskini na kukuza hali ya kiuchumi kwa mtu mmojammoja, makundi mbalimbali na taifa kwa jumla. Watanzania wengi walitegemea bajeti hiyo ilenge katika kufungua fursa za kiuchumi na kijamii kwa ajili ya maendeleo endelevu kupitia mfumo mpya uliowekwa na Serikali wa utekelezaji wa miradi ya kipaumbele inayotegemewa kuleta matokeo makubwa kwa haraka.

Matumaini hayo makubwa yalitokana na ukweli kwamba Bajeti hiyo iliyowasilishwa jana Bungeni ni ya kwanza katika utekelezaji wa Mpango wa kwanza wa Maendeleo ya Miaka Mitano. Mpango huo umeweka kipaumbele katika maeneo makuu sita ambayo ni Maji, Nishati, Elimu, Uchukuzi, Kilimo na Kuongeza Mapato.

Hata hivyo, Bajeti hiyo haionyeshi kuweka mkazo katika utekelezaji wa vipaumbele hivyo kwa vitendo wakati imetenga zaidi ya asilimia 60 kwa matumizi ya kawaida, huku miradi ya maendeleo kama barabara ikipewa fedha kidogo tu. Hotuba ya Bajeti hiyo kwa kiasi kikubwa imejaa siasa na maelezo matamu ya jumlajumla tu. Uchambuzi wa haraka wa hotuba za Bajeti za miaka ya hivi karibuni unaonyesha kwamba Bajeti hiyo iliyosomwa Bungeni jana haitofautiani sana na hizo zilizopita isipokuwa katika maeneo machache tu.

Kwa mfano, Serikali inasema Bajeti ya mwaka 2013/14 ina shabaha na malengo ya uchumi manane, ikiwa ni pamoja na kuwa na akiba ya fedha za kigeni zitakazokidhi mahitaji ya uagizaji wa bidhaa kutoka nje. Hata hivyo, haisemi lolote kuhusu mkakati wa kupata fedha zaidi za kigeni kutokana na kuongeza uzalishaji wa bidhaa zetu nje kwa lengo la kuweka ulinganifu wa kibiashara (Balance of trade). Hivyohivyo, Serikali inasema ina shabaha ya kupunguza mfumuko wa bei hadi digitali moja, lakini haisemi itatumia mkakati gani wakati mwaka uliopita mfumuko wa bei uliongezeka kwa asilimia 16 kutoka asilimia 12.7 mwaka 2011.

Mikakati mingi ya kuimarisha ukusanyaji wa mapato haitekelezeki na ndio maana Bajeti hii inaendeleza utamaduni wa kupandisha kodi katika maeneo yaleyale tulioyazoea kama bia, sigara, vinywaji baridi, leseni za magari, mafuta na kadhalika. Kupanda kwa bei ya mafuta bila shaka kutapandisha bei za vyakula na gharama za huduma mbalimbali. Kichekesho kikubwa ni pale ambapo Kodi ya Mapato kwa wafanyakazi imepunguzwa kwa asilimia moja tu kutoka asilimia 14 hadi 13.

Source: Mwananchi 14 Juni 2013
 
Ninafikiri ni muhimu kuweka utaratibu utakaolazimisha Serkali kupunguza matumizi ya kawaida ili kuongeza bajeti ya miradi ya maendeleo. Hivi kweli kwa bajeti hii tunaweza kujenga reli yetu ya kati ambayo kwangu mimi naona ni kichocheo kikubwa sana cha kukuza uchumi wetu na pia kuleta maendeleo? Je tuliweke ili katika katiba ya Tanganyika kwa sababu ndiye mtumiaji mkubwa?

Ukitilia maanani pia kuwa mapato ya matumizi haya mengi yatatokana na kupanda kwa mafuta ya petroli na dizeli, nafikiri mfumuko wa bei utapanda badala ya kushuka.
 
Nimeipenda bajeti ya Kenya na Uganda kuliko ya Tanzania. Wenzetu wamejipanga jamani hawana pekepeke mingi:yell::nod:
 
Nimeipenda bajeti ya Kenya na Uganda kuliko ya Tanzania. Wenzetu wamejipanga jamani hawana pekepeke mingi:yell::nod:

Unajua wote hawa wamepata mikasa inayofanana, wale waitwao 'wafadhili' au 'mapatina wa maendeleo' wamezira kuwapa misaada. kenya tangu baada ya vurugu za uchaguzi wamekuwa na bajeti ambayo inategemea zaidi mapato ya ndani na Uganda safari hii wanategemea sana mapato ya ndani baada ya wajanja kuzipiga pesa walizokuwa wakizileta.

Ukitumia pesa zako za ndani unakuwa mwangalifu zaidi, unapunguza matumizi yasiyo ya lazima. Hawa 'wafadhili' wanaahidi pesa za maendeleo na baadaye haziji, lakini inatudanganya pesa zetu za ndani zinaishia kwenye matumizi yasiyo ya msingi!
 
Ninafikiri ni muhimu kuweka utaratibu utakaolazimisha Serkali kupunguza matumizi ya kawaida ili kuongeza bajeti ya miradi ya maendeleo. Hivi kweli kwa bajeti hii tunaweza kujenga reli yetu ya kati ambayo kwangu mimi naona ni kichocheo kikubwa sana cha kukuza uchumi wetu na pia kuleta maendeleo? Je tuliweke ili katika katiba ya Tanganyika kwa sababu ndiye mtumiaji mkubwa?

Ukitilia maanani pia kuwa mapato ya matumizi haya mengi yatatokana na kupanda kwa mafuta ya petroli na dizeli, nafikiri mfumuko wa bei utapanda badala ya kushuka.
Jifunze kusema ukweli kama uko wazi na usipende kupotosha kwa makusudi mafuta yameongezwa kodi kwa shilingi mbili tu na hilo ongezeko linakwenda kuboresha shule na umeme vijijini unataka nini zaidi au umetekwa akili na wanasiasa wakurupukaji?
 
watu wa aina hii ni wa kupuuzwa tu,mandevu kawaharibu!
 
Jifunze kusema ukweli kama uko wazi na usipende kupotosha kwa makusudi mafuta yameongezwa kodi kwa shilingi mbili tu na hilo ongezeko linakwenda kuboresha shule na umeme vijijini unataka nini zaidi au umetekwa akili na wanasiasa wakurupukaji?

Uwe mzalendo pia! mafuta ya magari juu, road licence juu, simu ukimtumia mwanafunzi laki mbili lazima serikali ichukue Tzs.20,000/=!!!!!, kumbuka usafiri umepanda mwezi uliopita!!, Insurance companies nazo zimeongeza kodi zao!!.

Hiyo tshs.mbili unayosema sio kidogo na hivyo gharama za mazao na bidhaa nyingine juu!! uwe unatafakari kwanza sio kwa kuwa una laptop mbele yako tu unaweza kuleta viroja!!!!

Kwa gharama hizo za mafuta umeme lazima utakuwa juu na hivyo gharama za uzalishaji viwandani juu!!

Jifunze kusema ukweli kama uko wazi na usipende kupotosha kwa makusudi mafuta yameongezwa kodi kwa shilingi mbili tu na hilo ongezeko linakwenda kuboresha shule na umeme vijijini unataka nini zaidi au umetekwa akili na wanasiasa wakurupukaji?

Soma hapa kwa hisani ya Gazeti la Mwananchi la 14 Juni 2013
...Waziri Mgimwa alisema katika mwaka ujao wa fedha, Serikali itapandisha ushuru wa mafuta ya dizeli kutoka Sh215 kwa lita hadi Sh217 kwa lita, likiwa ni ongezeko la shilingi 2.

"Tumeongeza Sh2 tu kwa kuwa tunatambua tukiongeza ushuru mkubwa kwa magari makubwa ambayo yanatoa huduma kwa jamii, tutawaumiza wananchi," alisema Dk Mgimwa.

Kadhalika, ushuru wa mafuta ya petroli umeongezwa kwa Sh61, kutoka Sh339 kwa lita hadi Sh400. Hata hivyo, imeongeza kiwango cha ushuru wa mafuta (fuel levy) kutoka shilingi 200 kwa lita hadi shilingi 263 kwa lita, sawa na ongezeko la shilingi 63 kwa lita na wakati huohuo mafuta hayo yakiongezewa Sh50 kwa kila lita, fedha zitakazotumika kuchangia mfuko wa kusambaza umeme vijijini....

Pamoja na nia nzuri, Petroli na dizeli ndiyo chemichemi za kujenga uchumi na zinatumika na wengi. Ongezeko lake uliangalie kwa vyote fuel levy, mchango wa umeme, makato ya EWURA (hayakuorodheshwa) na mengine ambayo yatawekwa kwenye hiyo lita ya petroli na dizeli. Vinginevyo labda wewe una mtazamo tofauti, lakini mafuta haya ni kila kitu. Kauli ya kudanganya eti dizeli ndiyo inatumika sana na wasafirishaji si sahihi. Fanya uchunguzi kidogo tu, ni mafuta gani yanatumika sana hapa nchini kama si Petroli!
 
Ikiwa ni mara yangu kupost umu jamvini. Naomba nianze. Na kuwasalimia wanajamvi.Wasalaaaam.
 
Soma hapa kwa hisani ya Gazeti la Mwananchi la 14 Juni 2013
...Waziri Mgimwa alisema katika mwaka ujao wa fedha, Serikali itapandisha ushuru wa mafuta ya dizeli kutoka Sh215 kwa lita hadi Sh217 kwa lita, likiwa ni ongezeko la shilingi 2.

“Tumeongeza Sh2 tu kwa kuwa tunatambua tukiongeza ushuru mkubwa kwa magari makubwa ambayo yanatoa huduma kwa jamii, tutawaumiza wananchi,” alisema Dk Mgimwa.

Kadhalika, ushuru wa mafuta ya petroli umeongezwa kwa Sh61, kutoka Sh339 kwa lita hadi Sh400. Hata hivyo, imeongeza kiwango cha ushuru wa mafuta (fuel levy) kutoka shilingi 200 kwa lita hadi shilingi 263 kwa lita, sawa na ongezeko la shilingi 63 kwa lita na wakati huohuo mafuta hayo yakiongezewa Sh50 kwa kila lita, fedha zitakazotumika kuchangia mfuko wa kusambaza umeme vijijini....

Pamoja na nia nzuri, Petroli na dizeli ndiyo chemichemi za kujenga uchumi na zinatumika na wengi. Ongezeko lake uliangalie kwa vyote fuel levy, mchango wa umeme, makato ya EWURA (hayakuorodheshwa) na mengine ambayo yatawekwa kwenye hiyo lita ya petroli na dizeli. Vinginevyo labda wewe una mtazamo tofauti, lakini mafuta haya ni kila kitu. Kauli ya kudanganya eti dizeli ndiyo inatumika sana na wasafirishaji si sahihi. Fanya uchunguzi kidogo tu, ni mafuta gani yanatumika sana hapa nchini kama si Petroli!

Nashukuru kwa mchango wako mwanajanvi nafikiri tunapaswa kuijadili zaidi bajeti hii kunamambo yamewekwa kwenye hii bajeti lakini ninahofu kubwa na utekelezaji wake pia bajeti hii inaweza kuwa mwanya mzuri wa serekali ya ccm kujipati pesa kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao. Masalani kuwekwa kwa kodi ya 14.5% kwa watumiaji wa simu za mkononi kwa ajili ya kuchangia elimu waweza sema ni sahii lakini je usimamizi wa hayo mapato utakuwaje tutahakikisha vipi pesa sitakazokusanywa zitaenda kweli kwenye elimu na hizi ni pesa nyingi sana. Kwa wastani mtanzania wa kawaida anayemiliki simu ya mkononi anatumia Shs 1,000 kwa siku silimia 14.5% ya shs 1000 ni Shs 145 sasa kama unawatanzania masalani 5,000,000 wenye simu ukizidisha na shs 145 unapata shs 725,000,000 kwa siku ukizidisha mara 30 unapata Tshs 21,750,000,000 ni wastani wa bilion 21.75 kwa mwezi kwa mwaka utakuwa na shs 261,000,000,000 kwa hiyo ni pesa nyingi sana bado ukituma pesa kwa M Pesa au Tigo pesa au Airtel money unatonzwa 10% inamaana ukituma Tshs 10,000 kwa mtu unatozwa Shs 1000, ukituma 100,000 unakatwa Tshs 10,000 je ni pesa ngapi zitakusanywa? si bora sasa elimu ikawa bure hata swala la mikopo ya elimu ya juu lisiwepo?
 
IJUMAA, JUNI 14, 2013 05:47 REVOCATUS MAKARANGA, DODOMA

*Simu, vyakula, vinywaji bei juu

*Wamiliki wa bajaji, bodaboda kicheko

SERIKALI imeongeza ushuru katika baadhi ya bidhaa, kupunguza kodi ya mapato, kutoa msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika baadhi ya huduma, kufuta msamaha wa VAT na kodi kwa huduma nyingine, kuanzisha ushuru kwa baadhi ya bidhaa.Akisoma Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2013/14 mjini Dodoma jana, Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa alitangaza bidhaa ambazo ushuru umeongezeka kuwa ni petroli, dizeli, bia, vinywaji baridi, vinywaji vikali, juisi, mvinyo, sigara na ada ya leseni za magari.

Viwango vipya vya kodi na ushuru, vitaanza kutumika Julai mosi, mwaka huu isipokuwa pale ilipoelezwa vinginevyo, alisema Dk. Mgimwa na kuongeza kuwa Bajeti ya Serikali kwa mwaka ujao wa fedha, itakuwa Sh trilioni 18.24.

Alisema kiwango cha chini cha kutoza kodi ya mapato ya ajira kinapunguzwa kutoka asilimia 14 hadi asilimia 13 na mapato ya jumla ambayo hayatatozwa kodi ni yale yasiyozidi Sh 2,040,000.

Alisema ushuru wa maji ya viwandani na magari yenye ujazo wa injini chini ya 501cc, ambayo ni bajaji na pikipiki za bodaboda, hazitatozwa leseni.

Serikali vilevile, imeanzisha ushuru wa bidhaa wa asilimia 14.5 kwenye huduma zote za simu za mkononi, badala ya muda wa maongezi tu. "Katika ushuru huu asilimia 2.5 zitatumika kugharamia elimu nchini," alisema Waziri.

Alisema msamaha wa VAT, utatolewa kwa wazalishaji wa nguo nchini zinazozalishwa kwa pamba ya ndani, wakati msamaha wa VAT unafutwa kwenye huduma za utalii na msamaha wa kodi ya zuio kwenye ukodishaji wa ndege kwa walipa kodi wasio wakazi.

Alisema ushuru wa petroli, unapanda kutoka Sh 339 kwa lita hadi Sh 400 kwa lita, dizeli kutoka Sh 215 hadi Sh 217 na mafuta ya taa ushuru umebaki Sh 400.30 kwa lita.

Kwa vinywaji baridi, ushuru unaongezeka kutoka Sh 83 kwa lita hadi Sh 91 kwa lita, juisi ya matunda ya nchini kutoka Sh 8 hadi Sh 9 kwa lita na juisi inayotengenezwa kwa matunda ambayo hayazalishwi nchini ushuru unatoka Sh 100 hadi Sh 110 kwa lita.

Bia iliyotengenezwa kwa nafaka ya nchini ambayo haijaoteshwa, ushuru umeongezeka kutoka Sh 310 hadi

Sh 341 kwa lita na bia nyingine zote ushuru unatoka Sh 525 hadi Sh 578 kwa lita.

Alisema mvinyo uliotengenezwa na zabibu ya nchini kwa kiwango kisichozidi asilimia 75, ushuru umeongezeka kutoka Sh 145 hadi Sh 160 na mvinyo uliotengenezwa na zabibu ya nje kwa kiwango kisichozidi asilimia 25, ushuru utaongezeka kutoka Sh 1,614 hadi Sh 1,775 kwa lita.

Alisema vinywaji vikali ushuru umeongezeka kutoka Sh 2,392 hadi Sh 2,631 kwa lita na ushuru wa sigara zisizo na kichungi zinazotengenezwa na tumbaku inayozalishwa nchini utaongezeka kutoka Sh 8,210 hadi Sh 9,031 kwa sigara 1,000.

Sigara zenye kichungi na zinazotengenezwa kutokana na tumbaku inayozalishwa nchini kwa kiwango cha angalau asilimia 75, ushuru wake utapanda kutoka Sh 19,410 hadi Sh 21,351 kwa sigara 1,000, alisema.

Alisema sigara nyingine zenye sifa tofauti na hizo, ushuru umepanda kutoka Sh 35,117 hadi Sh 38,628 kwa sigara 1,000 wakati tumbaku ambayo iko tayari kutengeneza sigara, ushuru utatoka Sh 17,736 hadi Sh 19,510 kwa kilo na ushuru wa "cigar" unabaki asilimia 30.

"Ushuru wa mafuta (fuel levy), unaongezeka kutoka Sh 200 hadi Sh 263 kwa lita likiwa ni ongezeko la Sh 63," alisema.

Alisema katika kutekeleza dhamira ya Serikali ya kusambaza umeme vijijini, itaanzishwa tozo ya petroli ya Sh 50 kwa lita, ambayo itakusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

"Mapato yatakayokusanywa kutoka kwenye tozo hiyo, yatatumika kugharamia mahitaji ya Wakala wa Umeme Vijijini (REA)," alisema.

MAGARI

Kuhusu ushuru wa magari alisema gari la ujazo wa injini 501cc – 1500.cc unaongezeka kutoka Sh 100,000 hadi Sh 150,000 na gari la injini ya 1501.cc – 2500.cc kiwango kitakuwa Sh 150,000 hadi Sh 200,000.

Alisema gari la injini zaidi ya 2501 cc, ushuru utaongezeka kutoka Sh 200,000 hadi Sh 250,000.

Magari yasiyo ya uzalishaji ya umri wa zaidi ya miaka 10, ushuru wake umeongezeka kutoka asilimia 20 hadi 25 na magari ya uzalishaji yenye umri wa miaka 10 sasa yatatozwa ushuru wa asilimia 5.

Ushuru wa forodha kwenye ngano ya HS Code 1001.99.20 na HS Code 1001.99.90, utapunguzwa kutoka asilimia 35 hadi 10, wakati mchele na sukari zinazoingizwa nchini kwa msamaha maalum wa Serikali vitatozwa ushuru wa asilimia 25.

Migahawa ya majeshi ya ulinzi, itaendelea kupata msamaha wa ushuru wa forodha kwa mwaka mmoja, ushuru wa mitambo ya kusafisha uchafu wa maji unapunguzwa kutoka asilimia 10 hadi sifuri, alisema.

Mifuko ya plastiki inayotumika katika uzalishaji wa nishati ya gesi, nayo imesamehewa ushuru wa forodha kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala na kutunza mazingira.

Alisema malipo yanayotokana na huduma mbalimbali kama vile huduma za ushauri wa kitaalamu na nyinginezo, zitatozwa kodi ya zuio kwa kiwango cha asilimia 5.

Bidhaa zinazonunuliwa na Serikali na taasisi zake nazo zitatozwa asilimia 2 bila kujali kama kuna Namba ya Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN) au la, alisema.

Alisema Serikali itaanzisha utaratibu wa kuwakopesha magari watumishi wake, wanaostahili kupunguza gharama kwa Serikali na kuoanisha kanuni za ununuzi wa umma katika Serikali Kuu na katika Serikali za Mitaa.

010812.jpg

sijawahi ona bajeti ya kipumbavu kama hii
utaliii ndo unaingiza pesa nyingi za kigeni unaondoa VAT..

halafu eti unaongeza kodi za simu na soda,na upuuzi mwingine
 
Watanzania wamepumbazwa kwenye bajaji na bodaboda kuanzia bungeni mpaka kwenye jamii.
 
Watanzania wamepumbazwa kwenye bajaji na bodaboda kuanzia bungeni mpaka kwenye jamii.
Bahati mbaya sana haijawi kukataliwa Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha husika huko bungeni.Na hii ya mwaka huu haitakataliwa pia, na hata kufanyiwa marekebisho ndoto. Kilichoandikwa humo ndicho kitakachotekelezwa.

Chakufanya ni kuangalia namna ya kuji'adjust' ili uweze kupita salama mwaka huu.
 
Hili la kuondoa kodi ya leseni ya bajaji na bodaboda naona wanaongeza majanga badala ya kupunguza
 
sijawahi ona bajeti ya kipumbavu kama hii
utaliii ndo unaingiza pesa nyingi za kigeni unaondoa VAT..

halafu eti unaongeza kodi za simu na soda,na upuuzi mwingine

The Boss hii kitu nadhani umeielewa kinyume, hebu isome tena! "Kufuta msamaha wa VAT unaotolewa kwenye huduma za utalii"
 
kodi za kwenye simu binafsi nazikubali kwani hazina direct impact na maisha ya kawaida ya mtanzania. Isitoshe matumizi holela ya simu na sms yamezidi mno, pengine hii italeta nidhamu kidogo.

kasheshe ni kwa ndg zangu mawakala wa m-pesa, tigopesa n.k, ilivyo tu walikuwa wanalalamika commission ndogo, sasa tena kodi, nahisi hali itakuwa tete zaidi
 
BAJAJI NA PIKIPIKI watacheka vipi, mafuta ya petrol bei juu!!!! impact ni kubwa kwa bidhaa za vyakula na nauli. bei zitakuwa juu.

Ila kwa vile watanzania ni wapole na viongozi ni walafu, basi amani amani amani kama mazuzu vile
 
Back
Top Bottom