Hili la kuondoa kodi ya leseni ya bajaji na bodaboda naona wanaongeza majanga badala ya kupunguza
Filamu ya kisiasa hiyo,hamna kitu hapo
Hili la kuondoa kodi ya leseni ya bajaji na bodaboda naona wanaongeza majanga badala ya kupunguza
kodi za kwenye simu binafsi nazikubali kwani hazina direct impact na maisha ya kawaida ya mtanzania. Isitoshe matumizi holela ya simu na sms yamezidi mno, pengine hii italeta nidhamu kidogo.
kasheshe ni kwa ndg zangu mawakala wa m-pesa, tigopesa n.k, ilivyo tu walikuwa wanalalamika commission ndogo, sasa tena kodi, nahisi hali itakuwa tete zaidi
Binafsi nahisi unafuu ni mdogo mno kwani ukigusa mafuta hata kwa kiwango kidogo namna gani repercussion yake itagusa sehemu nyingi.Uwe mzalendo pia! mafuta ya magari juu, road licence juu, simu ukimtumia mwanafunzi laki mbili lazima serikali ichukue Tzs.20,000/=!!!!!, kumbuka usafiri umepanda mwezi uliopita!!, Insurance companies nazo zimeongeza kodi zao!!.
Hiyo tshs.mbili unayosema sio kidogo na hivyo gharama za mazao na bidhaa nyingine juu!! uwe unatafakari kwanza sio kwa kuwa una laptop mbele yako tu unaweza kuleta viroja!!!!
Kwa gharama hizo za mafuta umeme lazima utakuwa juu na hivyo gharama za uzalishaji viwandani juu!!
Mkuu naona unakwenda mbele halafu unarudi nyuma.Uliposema uwepo wa kodi katika simu hautaleta madhara ya moja kwa moja nilitarajia ungekuja na hoja ya kitafiti kutetea hoja yako,Umeniacha hoi pale ulipodai kodi hizi zitaongeza nidhamu kwasababu matumizi holela ya simu.Kwahiyo ndiyo sababu ya kuweka hiyo kodi yaani uwaadhibu watu kwaajili ya matumizi holela ya simu?Zaidi ya yote pia unakiri kile kitakacho tokea ktk huduma M-pesa,Tigo-pesa,nk,Wateja wa hizi huduma watapungua,Vijana wengi waliojiajiri kuendesha hizi huduma huko mitaani watafunga biashara zao.Hapa hamumkomoi mtumiaji wa simu ila mtaathiri biashara za vijana wengi mitaani.