Baina ya CUF na CHADEMA kipi CCM-B? - hoja ya matusi

Calipso

JF-Expert Member
Mar 25, 2009
284
15
Baada ya malumbano marefu na ya siku nyingi tena ikiwa ktk maeneo tofauti na mada ya hapo juu ama ktk thread nyengine ambazo hazihusiani na kadhia hiyo,leo nimeona niweke thread maalum kwa kadhia hii baina ya Cuf na Chadema ipi ni CCM-B,ambapo humu hasa itakuwa ndio sehemu yake na kupeana point muhimu na matukio yalotokea nyuma baina ya vyama hivi..

Muhimu ni kujenga hoja na kuweka ushahidi,hii itasaidia kuwaweka wazi wadau na kuweza kujadili kwa kina,lkn si hivo tu bali itavisaidia vyama hivi kuangalia wapi wamekosea..

Matusi hayatojenga wala hayatosaidia na itakuwa ni mwisho wako wa kufikiri umefika hapo.

Nataraji tukifanikisha mada hii,nitaleta thread nyengine kuonesha ushirikiano wa chadema na cuf ulivyokuwa na ulivyoyayuka ghafla na kilichotokea baada ya hapo lkn pia itaonesha umuhimu wa kuungana kwa vyama hivi pamoja na kuonesha maeneo ya TZ ambayo Cuf inakubalika na Chadema inakubalika na wana JF mtatoa mawazo yenu kwa vyama hivyo nini vifanye

NAAMINI USHIRIKIANO WA VYAMA VYA UPINZANI NDIO UTAKAOWAONDOA CCM MADARAKANI. Jaribu kufikiri CCM imejipanga vipi na kila kitu kipo chini ya CCM NA MKUU M/KIJIJI KAELEZA KATIBA INAYOKUJA..

LENGO 2015 CCM IWE BAIBAI HAPA NA ZNZ - UMIMI - UWEWE UWEKE PEMBENI.

INAWEZEKANA IKAWA NIMEWEKA MADA MBILI KWA WAKATI MMOJA.

UWANJA WAKO
 
Ulipofikiria kutukanwa ndio umejitukana tayari!!!!
Andaa sabuni na dodoki, utayakoga matusi ile mbaya, kama unadhani onyo lako litasaidia subiri uone!
 
Umeshajipima na kuipima mada yako ndio maana ukajua kuwa inastahili matusi. CHADEMA kuungana na CUF kwa faida ya nani?

Na kama unazungumzia upinzani, mbona usivitaje na vyama vingine ambavyo mimi naamini ni vya upinzani zaidi ya CUF ambayo tayari imeolewa na CCM kule ZNZ?

Mimi naona wewe ni mmoja wa wakina yakhe, sasa unaongea kwa manufaa ya CUF. CHADEMA haina haja ya kuungana na U-Maalim ili kufanikisha lengo. Sanasana kwa kufanya hivyo itawaudhi watu walio serious kwa kuwa tunaamini CUF ni watu wasiojua wanachofanya.

Na haya maneno yako ya kuungana yanakuja baada ya kuona mafanikio ya CHADEMA kwa hiyo sasa umeshabaini kuwa mmekufa na unatafuta pa kuinukia. Uzini CCM 5200, CDM 269, CUF 217.

Arumeru mmekimbia kabisa, sasa nani ana hamu ya kuungana na failure?
 
Mie naona CCM-B ni chadema kwa sababu sera za chadema ni kujipimia kwa CCM. Pia ukichunguza vizuri mfumo mzima wa uongozi ndani ya chadema utaukuta ni mfumo endelevu wa CCM. Na mwisho naweza kusema Chadema ni CCM-B kwa kutizama hata viongozi wanaotoka CCM wanahamia CCM-B kwa kuwa wanajua kule ndiko kuliko pia mianya ya kuendelea kula mali za watanzania. hivi ndivyo nionavyo
 
Baada ya malumbano marefu na ya siku nyingi tena ikiwa ktk maeneo tofauti na mada ya hapo juu ama ktk thread nyengine ambazo hazihusiani na kadhia hiyo,leo nimeona niweke thread maalum kwa kadhia hii baina ya Cuf na Chadema ipi ni CCM-B,ambapo humu hasa itakuwa ndio sehemu yake na kupeana point muhimu na matukio yalotokea nyuma baina ya vyama hivi..

Muhimu ni kujenga hoja na kuweka ushahidi,hii itasaidia kuwaweka wazi wadau na kuweza kujadili kwa kina,lkn si hivo tu bali itavisaidia vyama hivi kuangalia wapi wamekosea..

Matusi hayatojenga wala hayatosaidia na itakuwa ni mwisho wako wa kufikiri umefika hapo.

Nataraji tukifanikisha mada hii,nitaleta thread nyengine kuonesha ushirikiano wa chadema na cuf ulivyokuwa na ulivyoyayuka ghafla na kilichotokea baada ya hapo lkn pia itaonesha umuhimu wa kuungana kwa vyama hivi pamoja na kuonesha maeneo ya TZ ambayo Cuf inakubalika na Chadema inakubalika na wana JF mtatoa mawazo yenu kwa vyama hivyo nini vifanye

NAAMINI USHIRIKIANO WA VYAMA VYA UPINZANI NDIO UTAKAOWAONDOA CCM MADARAKANI. Jaribu kufikiri CCM imejipanga vipi na kila kitu kipo chini ya CCM NA MKUU M/KIJIJI KAELEZA KATIBA INAYOKUJA..

LENGO 2015 CCM IWE BAIBAI HAPA NA ZNZ - UMIMI - UWEWE UWEKE PEMBENI.

INAWEZEKANA IKAWA NIMEWEKA MADA MBILI KWA WAKATI MMOJA.

UWANJA WAKO

Unaposema ushirikiano wa vyama vya upinzani, unataka kumaanisha Tanzania kuna vyama vya upinzani zaidi ya kimoja??
 
Kila chama kina sera zake. Wakiungana itatumika sera ya nani? Suala la msingi sio kukiondoa CCM kwa "njia yoyote", bali ni kuhakikisha inakufa kifo cha kawaida kama dalili zinavyoanza kuonesha. Muungano unaopendekeza ulifanyika Kenya, lakini yaliyotokea umeyaona. Waache wananchi wawe ndio chachu ya mageuzi, hata kama itakuwa hivyo baada ya kizazi kilichopo kuisha. Kumbuka ANC ilianzishwa mwaka 1912 na imefanikiwa kuikomboa Afrika ya Kusini baada ya miaka zaidi ya 80.

Watu hawakichukii CCM ati kwa kuwa vyama vya upinzani ni vizuri sana; na wala hawakuipenda kwa kuwa ni nzuri sana. Itafika wakati Mungu atawainua watu wake wataiongoza nchi hii na neema zitawafikia watanzania wote kuanzia aliye chini mpaka wa juu. Namuomba Mungu asinichukue kabla ya kuiona siku hiyo; na hata akinichukua, wanangu na wajukuu wangu wataiona. Amina.
 
Mie naona CCM-B ni chadema kwa sababu sera za chadema ni kujipimia kwa CCM. Pia ukichunguza vizuri mfumo mzima wa uongozi ndani ya chadema utaukuta ni mfumo endelevu wa CCM. Na mwisho naweza kusema Chadema ni CCM-B kwa kutizama hata viongozi wanaotoka CCM wanahamia CCM-B kwa kuwa wanajua kule ndiko kuliko pia mianya ya kuendelea kula mali za watanzania. hivi ndivyo nionavyo
Viongozi wanaotimka kutoka ccm, wanaondoka kwa kuwa wanaona mwelekeo wa ccm ni mbovu na kule wanakoenda washaona mwelekeo mzuri, ni sawa umepanda gari linapelekwa pelekwa tu, dereva na konda hawaelewani, konda anamwambia dereva simamisha gari, yeye anakanyaga mafuta, abiria wanampigia kelele dereva hataki kuwasikiliza.
Sasa kukitokea gari lenye Ustaharabu si abiria wote watatimkia kwenye hilo gari? Watabaki wale waliopanda bure, au wasio na nauli (hawa ni sawa na waliofirisika kimawazo kama Kingunge)
Wenye pesa zao watapanda gari jingine ambalo litawafikisha kule waendako (hawa ndio wenye mtaji wa kisiasa kama Millya)

Mie naona CCM-B ni chadema kwa sababu sera za chadema ni kujipimia kwa CCM. Pia ukichunguza vizuri mfumo mzima wa uongozi ndani ya chadema utaukuta ni mfumo endelevu wa CCM. Na mwisho naweza kusema Chadema ni CCM-B kwa kutizama hata viongozi wanaotoka CCM wanahamia CCM-B kwa kuwa wanajua kule ndiko kuliko pia mianya ya kuendelea kula mali za watanzania. hivi ndivyo nionavyo

Huyu nae katokea wapi?????????
 
kwa maoni yangu cdm ndio haswaa ccm b, vipo viashiria vingi vinavyo thibitisha cdm ni ccmb, naanza na mambo madogo uwepo wa shibuda, na mahusiano ya lowassa. Mtindo wakugawapesa ktk chaguzi. Kama igunga hiv karibuni kata ya vijibweni walimwaga pesa ili kuikomoa cuf ambayo ndio diwani aliekufa katoka chama hicho cha cuf . Sehemu kama hiyo unajua fika diwani ni cuf wa upinzani. Kusimamisha mgombea kwa cdm nikusaidia ccm kushinda kushinda nandio ilivyotokea mgombea wa ccm kushinda
 
mie naona ccm-b ni chadema kwa sababu sera za chadema ni kujipimia kwa ccm. Pia ukichunguza vizuri mfumo mzima wa uongozi ndani ya chadema utaukuta ni mfumo endelevu wa ccm. Na mwisho naweza kusema chadema ni ccm-b kwa kutizama hata viongozi wanaotoka ccm wanahamia ccm-b kwa kuwa wanajua kule ndiko kuliko pia mianya ya kuendelea kula mali za watanzania. Hivi ndivyo nionavyo

humu hapakufai kaka you are not a great thimker usitupotezee muda
 
kati ya ANNA KILANGO NA ANNA ABDALA NI NANI MKE WA MALECHELA?

UKISHAJIBU HILI UTAKUWA UMEPATA JIBU LA SWALI LAKO.

ASUBUHI NJEMA.
 
Mimi nitaka kukusaidia kidogo hapo.
1. Awali ni kuwa unatakiwa kujua kila chama katika ulivyo vibainisha hapo juu kimewekwa kisharia kabisa kwa kufuata taratibu na kaanun ikiwemo pamoja na kusajiliwa na msajili wa vyama vya siasa huko Tanzania.
Hivyo kila chama kina Katiba, Dira, malengo, Ilani yake na mengine mengi.

2. Ukiangalia CCM ni chama mama na karibu viongozo wote wakubwa wa vyama vingine ni zao la CCM ila kwa namna moja au nyingine wakaaamua kujitoa na kuanzisha vyame pinzani.

3. Ukiitazama Chadema ni chama chenye mvuto zaidi bara hususan sehemu za Uknda wa Ziwa na chimbuko lake ni kanda ya mashariki.

4. CUF ni chama chenye mvuto mkubwa sana sehemu za Kusini na Pwani ya tanganyika kikiwa na chimbuko lake likiwa Znz hususan pemba.

Kwa mantiki hiyo napenda kumaliza kwa kusema.
Mosi. Hakuna CCM B labda useme CCM B ni ile UVCCM.
Pili. hauwezi hata siku moja kuviunganisha CUF na Chedema kwani hawa wana asli tofauti ni sawa na kuchanganya sukari na chumvi. Labda waungane kimkataba kama ilivyyoungana Tanganyika na Znz

Hayo ni maoni yangu.
 
Back
Top Bottom