Bahlul kukalia kiti cha khalifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bahlul kukalia kiti cha khalifa

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by KABAVAKO, Jul 9, 2012.

 1. KABAVAKO

  KABAVAKO JF-Expert Member

  #1
  Jul 9, 2012
  Joined: Apr 5, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Siku moja Bahlul aliingia katika Qasri ya Khalifa na kukuta kiti chake tupu aliona hakuna mtu wa kumzuia, hivyo alikwenda moja kwa moja akaketi juu ya kiti cha Khalifa.


  Walipotokezea maaskari wa Khalifa, walijaribu kumwondoa Bahlul, lakini alikataa, hivyo waliweza kumwondoa kwa kumpiga. Hapo Bahlul alianza kulia kwa sauti, na alipotokea Khalifa Harun Rashid alimwona Bahlul akilia kwa sauti na aliwauliza maaskari wake sababu. Wao walimwelezea yote yaliyotokea. Hapo Khalifa aliwakemea maaskari hao na kumpa pole Bahlul.


  Kwa hayo, Bahlul alisema: "Mimi sikililii kile kilichonipata, bali ninakulilia wewe Khalifa, kwani mimi nimeteswa kwa kuketi punde tu, je wewe utateswaje kwa kukikalia kiti hiki kwa miaka yote hiyo kwani kiti hiki cha Ukhalifa ni kwa ajili ya watu wengine na wewe umewadhulumu hao, na kukikalia kwa mabavu!"
   
Loading...