Bahari mfu (dead sea) na uhalisia wa msomi wa tanzania

Apr 18, 2012
95
213
DSCN9552-1024x640.jpg

Mimi ni Mwl wa GEOGRAPHY pia na nilijifunza hili toka Bahari hii hadi ikaitwa hili jina.
BAHARI hii iko Mashariki ya kati, Inaitwa BAHARI YA CHUMVI ama BAHARI MFU kwa sababu hakuna Uhai ndani yake.

BAHARI Hii inapokea maji yake toka MTO YORDANI, Mto huu hupeleka Maji pia ZIWA GALILAYA.

Hii Inaitwa BAHARI MFU (DEAD SEA) kwani hakuna UHAI ndani yake, Hakuna KIUMBE kinaweza KIKAISHI humo kwenye Bahari hii.

Shida ya BAHARI hii ni Kwamba inakiwango kikubwa sana cha KUPOKEA MAJI (INLETS) toka mto yordan, Na ASILI ya MIAMBA yake (Bahari) ni ya chumvi.

BAHARI MFU maji yake Yana kiwango kikubwa sana cha CHUMVI, DENSITY yake Ni kubwa sana kiasi kwamba Unaweza Ukadumbukia humo na USIZAME ukaanza KUSOMA GAZETI uko juu ya maji😂

Bahari haina MIFELEJI ya KUTOA MAJI na KIASI kikubwa cha MAJI yake yanapotea Kwa MVUKE,

Hali hiyo hupelekea CHUMVI nyingi sana Kubaki Kwenye BAHARI kitu ambacho kinakuwa ni SUMU ndani yake na Kukosekana kwa MAISHA humo, ndo maana dead Sea.

Naomba UJUE kwamba Unajitahidi sana KUJIFUNZA (Unaingiza maarifa mengi sana) kuhusu Jambo flani, ni sawa kabisa.

Huna OUTLET yoyote ya Kutoa Hicho kitu KIWASAIDIE WENGINE, Hatimae vitu ulivyojifunza ama ulivyopata VINAPOTEA kwa MVUKE (Kusahau na Kuibiwa)
Vinaacha ndani yako UCHUNGU mkali (CHUMVI) ambayo haisurpot maisha ya wengine kabisa.

Ulishakuwa HUNA UHAI ndani yako ungali unatembea kwani HUNA cha KUWASAIDIA WATU na wewe vimekuachia SUMU kali hivyo vitu.
hapa MAJUNGU na WIVU vinakujaa Hakuna tena hali ya kitu KUINGIA KWAKO Kikaishi kinachotakiwa KUISHI HUMO

Unapokuwa na INLETS (Unapopata vitu) Ni vyema Ukawa na OUTLETS (Kutoa vitu kwaajili ya kusaidia) zitakulinda na CHUMVI NYINGI.

UNAJIFUNZA sana neno hutaki sasa KUFUNDISHA/KUHUBIRI, Umepata FEDHA hutaki KUSAIDIA, Hii ni HATARI. You're a Dead man.

Nadhani Umejifunza, Usibaki na Vitu UTAUMIA, Kama ni MUDA wa KUVITOA basi TOA usaidie wengine kupunguza kiwango cha CHUMVI ndani yako.

•Utoshelevu
📞 e-SBO
 
Mi niendelee hapa huo usia wako ngoja niweke pembeni. Hivi maja yakiwa na chumvi nyingi yanaongeza density? Ngoja nije nifanye jaribio kwenye beseni nione!!!
 
Ulianza vizuri sana, na nilijifunza kitu kwa nini inaitwa dead sea, lakini umeharibu kabisa ulivyomalizia.

Kwanini haujiamini mpaka unanza kujihami kwa mawaidha marefuuu! Hapo ulitakiwa utenganishe nyuzi, wengine huwa hatupendi nyuzi za mawaidha
 
Ulianza vizuri sana, na nilijifunza kitu kwa nini inaitwa dead sea, lakini umeharibu kabisa ulivyomalizia.

Kwanini haujiamini mpaka unanza kujihami kwa mawaidha marefuuu! Hapo ulitakiwa utenganishe nyuzi, wengine huwa hatupendi nyuzi za mawaidha
Mwandiko wake wenyewe ni wa Google translate, Mimi hata movie tu ukishaingiza maneno ya kutafsiri umeshanikoroga tayari.
 
Wewe hamna kitu hivi kuna bahari gani duniani yenye outlet ya kutapisha maji kwenye source nyengine? Bahari kazi yake ni kupokea maji kutoka vyanzo vyenine.
 
Back
Top Bottom