Bafu la maji moto

JMF

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
1,758
2,769
Habari zenu wakuu?
Naombeni ushauri kwa wenye experince na mabafu yenye kuogea ya maji moto. Ni vitu gani hasa vinahitajika kuweza kubadili bafu la kawaida liwe na option ya maji moto. Bafu tayari lipo na umeme upo ndani.

Pia naomba kujuzwa gharama kwa anayejua kwa sababu kila fundi nikimuuliza ananitajia mlolongo wa vitu ambavyo nashindwa kujua kama ni kweli au laa na wanatofautiana sana.

NB: Siyo bafu la nyumba ya kupanga wala ya biashara, ni bafu la matumizi ya kawaida nyumbani. Asanteni.
 
Kwanza inabidi uwe na hiko kifaa cha kuyafanya maji yawe yamoto (heater). Halafu utafute mafundi 2 mmoja mtalaam wa umeme akufikishie umeme hapo utakapofunga hiko kifaa cha kuchemshia maji, halafu uwe na fundi bomba ambae utakuuingia mabomba hutoka kwenye hiko kichemsha maji hadi kwenye bomba lako. Lakini pia bomba lako lazima liwe linauwezo wa kuchanganya maji; yale yatokayo kwenye kichemsha maji na maji yatokayo moja kwa moja kwenye bomba kuu. kichanganya maji moto na baridi kinaitwa (mixer).
1. Vichemsha maji vimbo aina mbali mbali inategemea na ubora na ujazo pia bei makadirio kuanzia Sh. 100,000 nakuendelea
2. Itabidi ununue mabomba (pipes) kwa ajili ya kuunganishia pamoja na vifaa vyote ambavyo fundi atakuelekeza
3. Kichanganya maji (mixer) pia inategemea na ubora bei makadirio sh. 70,000 nakuendelea hata vya milioni moja vipo
4. Waya za umeme. mita chache tu.
5. Inawezekana ukauchimba ukuta kuweka mambomba, na kama kuna vigae vya ukutani hapo ndio kazi maana kama kuna kuchimba ukuta itabidi hivyo vigae kuvivunja na ununue vipya.
6. Ghalama za mafundi - maelewano
 
solar heater ni bora zaidi especially kuna hizi za kisasa ambazo mwanga mdogo tu zinapasha maji moto..unaepukana na gharama za umeme kwa muda mrefu,japo heater za solar kwa bongo inabidi ujipange kimfuko.
Wastani wa bei mkuu
 
Kama unataka solar water heaters waone Ensol Tanzania hapo Ubungo plaza. Lakini zipo pia showers zenye heater kabisa unafunga tu kwe pipe inayomwaga MAJI bafuni unaunganisha na umeme moja kwa moja. Mimi nilifunga moja aina ya Liper mpaka Leo inagonga mzigo bila wasiwasi! Gharama yake ilikuwa Tsh.45,000/=
.
 
Habari zenu wakuu?
Naombeni ushauri kwa wenye experince na mabafu yenye kuogea ya maji moto. Ni vitu gani hasa vinahitajika kuweza kubadili bafu la kawaida liwe na option ya maji moto. Bafu tayari lipo na umeme upo ndani.

Pia naomba kujuzwa gharama kwa anayejua kwa sababu kila fundi nikimuuliza ananitajia mlolongo wa vitu ambavyo nashindwa kujua kama ni kweli au laa na wanatofautiana sana.

NB: Siyo bafu la nyumba ya kupanga wala ya biashara, ni bafu la matumizi ya kawaida nyumbani. Asanteni.
Mkuu kama upon dar na unahitaji funding aliyebobea kwenye hiyo ishu ntakupa mamba
 
Kama unataka solar water heaters waone Ensol Tanzania hapo Ubungo plaza. Lakini zipo pia showers zenye heater kabisa unafunga tu kwe pipe inayomwaga MAJI bafuni unaunganisha na umeme moja kwa moja. Mimi nilifunga moja aina ya Liper mpaka Leo inagonga mzigo bila wasiwasi! Gharama yake ilikuwa Tsh.45,000/=
.
Mkuu naomba ufafanuzi kidogo kuhusu hiyo Liper. Inapatikana wapi na inafanyaje kazi.
 
Kiongozi hiyo bei 45k ni ghalama ya ufundi au ndio bei ya mtambo wenyewe?
 
Ndo bei ya kifaa chenyewe,, siyo mtambo mkubwa kama unavyofikri mkuu, ni shower tu zinazomwaga maji ya mvua ila inakuwa imeunganisha na heater kabisa kwa ndani yake. Hivyo ukifungulia tu maji halafu unawasha switch ya umeme pale ukutani maji yanachemka hapo hapo. Ukitaka yatoke yasiyokuwa na moto mkali unaongeza pressure ya maji tu! Ila imekuwa siku nyingi yawezekana kuwa vimepanda (miaka mnne iliyopita).
 
Asante mkuu. Hiko kifaa kinaitwaje kitalaam? Maana nimesearch kwa jina 'liper kama ulivyodekeza juu, lakini sipati majibu sahihi'
 
upload_2017-4-5_20-11-26.png

Kako design hii mkuu! Lakini siyo lazima kawe kutoka liper, kuna aina nyingi za design hii, sasa sijui wenyewe wanaita "tank less water heater"
 
Mkuu naomba ufafanuzi kidogo kuhusu hiyo Liper. Inapatikana wapi na inafanyaje kazi.
Mkuu angalia post #13 nimeweka na sampuli yenyewe jinsi hicho kifaa kinavyoonekana!
 
Shukrani mkuu. Nilipata aina ya Lorenzete kama hiyo hapo juu kwa 50,000Tsh na inapiga kazi vizuri. Ubarikiwe.
Enjoy it ng'wana wane!! Ila kama una watoto changamoto itakuwa unit za umeme. Wa kwangu walikuwa wanatamani kulala huko wakati wa baridi!
 
Kwani wewe kila siku una umeme ambao ni mdogo kila siku? Basi kama ni mdogo hata ile ya tank haiwezi kufanya kazi! Vingine labda uende solar!
Ya tank ndo bomba zaidi.

Over!!!!
 
Back
Top Bottom