Lyambalyetu
JF-Expert Member
- Apr 6, 2021
- 302
- 295
Hawa wote wameongoza taasisi ambazo malalamiko hayakomi dhidi ya Taasisi hizo. Badru amwewahi kulalamikiwa sana kuhusu utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.
Huyu amekuwa akilindwa sana na Sheria husika kwani haina hata utaratibu wa kujua kwanini wengine huwa hawapati mikopo.
Badru kumpata kwa simu yake ni ngumu sana sana, lakini pia Menejimenti yake hajawahi kuwa nayo vizuri sana ndiyo maana baadhi ya Wakurugenzi aliwachomoa sana kabla hajatoka na yeye.
Huyu anaenda PSSSF kwa ajili tu ya network yake aliyoweka na Mama Ndalichako ilimradi Waziri huyu naye anataka ajinufaishe kwa kupitia Mfuko huo kupitia mtu wake kama ilivyokuwa Waziri Mhagama na Kashimba.
Kashimba kwa ujumala wake, pia ni Mtendaji mzuri sana.
Kwa fani yake ya ukaguzi wa ndani yupo makini sana katika kudhibiti fedha za Taasisi. Huyu pamoja na kuwa na ngozi ngumu yaani kutosikiliza sana malalamiko ya wanufaika na Mfuko lakini kuna wakati huonesha huruma na kuhakikisha malalamiko yanatatuliwa na wanaonufaika wanapata haki yao.
Hawezi kusemwa sana kuwa ndiyo chanzo cha kikokotoo kilicholalamikiwa kwani katika wakati wake angalau alishauri na kuifikisha ile 33? ya malipo ya mkupuo kutoka 25%.
Huyu haijulikani atapelekwa wapi ingawa naye pia baada ya kuingia pale PSSSF alichukua asilimia kubwa ya Menejimenti ambao walikuwa ni washikaji wake. Hata hivyo haifikiriki kama atawekwa benchi taratibu taratibu kwani ni Mtendaji mzuri pia.