cenzo
Senior Member
- May 7, 2015
- 124
- 28
Wazee wa JF Habari za leo,
Hivi hii nchi ni wapi tunaelekea?
Swali langu, hivi kweli hawa waandamaji wa miaka hii ni kweli wanatafuta haki zao au ni vibaraka tu wanaotumiwa na Wanasiasa? Nimeshuhudia leo pale Karume, jijini Dar es salaam walemavu wakiandamana na kudai haki zao zitekelezwe.
Swali langu; je, hapo miaka ya nyuma wananchi wa Tanzania hatukuzijua haki zetu?
Na kama ni kweli kuwa miaka ya sasa watu wamefunguka macho na masikio kwa kuzijua haki zao tofauti na zamani, basi ni vyema tukampongeza mheshimiwa rais kwa kutupa uhuru huu tulioukosa kwa miaka mingi.
Lakini pia nina wasiwasi na haya maandamano ya sikuhizi na hii migomo huenda tu ni chochezi au kampeni za wanasiasa fulani ili kuja kujikombea kura za uchaguzi.
Kwanini migomo na maandamano yamelipuka sana wakati huu tukielekea kwenye uchaguzi mkuu?
Mungu ibariki Tanzania na watu wake, dumisha upendo na umoja.