ibanezafrica
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,261
- 6,552
Yaani kinachoendelea ndani ya bunge tumekua tukisikia juu juu tu au watu wakiongelea mitaani, au mtandaoni, kwa kifupi habari za bunge sasa twazipata kwa kuungaunga, hili si sawa. Wananchi ndio tumechagua wawakilishi wetu na ndio sauti zetu ni muhimu tuone na tuusikie uwakilishi wao kwetu kwa 100%.
Juzi tumefuatilia uchaguzi wa wabunge wa EA walipokusanya kura spika akatangaza kuwa watarudi baada ya Dk 20, TBC wakaweka taarifa ya habari, lakini ilipoisha taarifa ya habari hawakurudisha tena bunge Live wakaweka vipindi vingine huku bunge kule likiendelea. Bado sijajua tatizo hasa nini, kodi tunalipa, tunaomba wabunge wote mpiganie hili, wizara ya habari mlitafakari jambo hili hasa kuelekea bunge hili la bajeti.