Mr Bean.
Senior Member
- Jan 25, 2015
- 185
- 128
Wadau kuna hii mentality iliyojengeka miongoni mwetu kwamba kila likicho cha china ni fake. Hadi imezoeleka kwamba kila kitukibaya au kisicho na ubora huitwa cha China hata kama hakiusiani kwa namna yeyote na Jamuhuri hiyo. Ukifuatilia kwa makini sasa utagundua barabara nzuri ni zile zinazojengwa na Kandarasi za kichina. Hali hiyo ipo ktk kila sekta hata majengo mazuri ni wachina. Nguo tunazovaa na kuonekana watashat ni wachina. Simu za viganjani zenye majina makubwa now zinatoka China ikiwemo IPhones. Mimi binafsi nina Laptop Sony made in China miaka mitano sasa no problem. Madaktari wazuri China Now hata samaki (Vibua)nk tunakula wanavuliwa na wachina. Majumbani kwetu vifaa tunavyotumia kuanzia kijiko hadi mashuka ni China. Hii mentality ya wachina na vitu fake inatoka wapi. Nawasilisha.