RAHA KAMILI
JF-Expert Member
- Dec 5, 2014
- 203
- 83
Chemba ya biashara, viwanda na kilimo( TCCIA) inatarajia kufanya ziara ya kibiashara nchini Italy na Uturuki ambapo Chemba inapenda kuwakaribisha wafanyabiashara walio wanachama na wasio wanachama kuungana nasi kwenye mkutano huu wa wawekezaji. Chemba inawakumbusha kwamba, imabaki siku moja kwa wafanyabiashara wa Italy kuthibitisha ushiriki wao ambapo mwisho ni tarehe 3 March 2017. Kwa 3wafanyabiashara wa Uturuki wana muda mrefu ambapo muda wa mwisho wa kuthibitisha ushiriki wao ni tarehe 30 March 2017. Ziara hii inatarajia kufanyika mwanzoni mwa mwezi May.
Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TCCIA Ndugu Gotfrid Muganda alisema “Lengo kubwa la ziara hii ni kuwawezesha wafanyabiashara wa Tanzania kutanua wigo wa masoko na fursa za kibiashara na kubadilishana ujuzi”. Akizungumza juu ya ziara hiyo Mkurugenzi wa EAG Group ambao ni washauri wa biashara na masoko wa TCCIA Imani Kajula alisema “Ukuzaji wa masoko ya nje ni mkakati endelevu ambao sio tu utaongeza soko nje lakini pia kuleta urari mzuri wa biashara na hivyo kusaidia kuimarisha thamani ya shilingi”. Aliwaambia wafanyabiashara ambao ni wanachama na wasio wanachama wanakaribishwa kijiandikisha ambapo mwisho kwa wanaoenda Italy ni tarehe 3 March 2017.