SILVANUS MUMBA
Senior Member
- Aug 22, 2015
- 149
- 55
Awali ya yote niwasalimu na kuwatakia Pasaka njema, Ndugu zangu jamaa na Marafiki nyote, mlioko Tanzania na nje ya mipaka ya Tanzania.
Ni matumaini yangu kuwa nyote mko sawa, na mimi kwa unyonge wangu lakini na Fikra zangu pevu nasema niko “NGANGARI”.
Leo niliwiwa kuifuatilia report juu ya kuimarika kwa hali ya kiuchumi Tanzania, wakichuchukulia mifano ya matumizi ya fedha na uboreshwaji wa maisha kwa Watanzania kwa jitihada binafsi.
Report ile ilireflect maisha ya mwaka 2012, na kutoa aggregate ya 1700 Tanzana shilling au 1 Dollar kwa siku. Nimeshangaa kuona mtu anajitokeza mbele na kusema uchumi unaimarika kwa kigezo cha Dola 1 kwa siku. Hiki ni kichekesho cha karne ambacho hata tumbili ukiwasimulia pale kwenye kona za kitonga watakucheka.
Wakati Wenzetu wanapima Economic sustainability kwa real natural and magnified indicators, sisi tunafanya aggregate za kuimarika kwa uchumi kwa kutumia matumizi ya vyandarua, eti watumiaji wa simu za mikononi na ujengaji wa nyumba zenye kuta imara. “are we Tanzanians serious about economic sustainability? Do we know the concept?
Hofu yangu ni kuwa Si kweli kwamba Tanzania kiuchumi tumeimarika kwa kiasi hicho. Lakini pia shilingi 1700 ya mwaka 2012, haiwezi kuwa sifa kubwa kwa watanzania ambayo tunaweza kutoka front na kusema uchumi umeimarika.
Lets say hii 2016, labda pato letu liwe 2,000 kwa siku, still Watanzania wanamaisha magumu, kwasababu the living standard ya Watanzania iko juu sana, na hii inatokana na Kodi za nyumba, Bill za umeme, bei ya vyakula, huduma mbalimbali mfano za simu, na mawasiliano kwa ujumla.
Serikali imeshindwa kuvimaintain hivi vitu vyote, huku wakishindwa kutengeneza mikakati mizuri ya kukusanya kodi kupitia biashara kama ya upangishaji wa vyumba. Huku wakiacha vyumba kwa mikoa kama Dar es Salaam akipangishwa kwa 250,000 shilingi hadi 500,000 shilingi kwa mtanzania huyu mwenye pato la kawaida.
Watanzania wengi hulazimika kupanga kwa sababu mbalimbali, huku zikiwepo pato lao kutotosheleza kujenga nyumba zao binafsi, Gharama za kupata Ardhi ya kujenga, rushwa na urasimu wake, lakini Eneo la kazi ni Dar au Mwanza.
Serikali imeshindwa kusimamia haki za wapangaji kufikia hatua wapangaji wananyanyaswa, Watumiaji wa Umeme wananyanyaswa, lakini pia watoaji wa huduma mbali mbali kama za Maji pia kuwanyanyasa Watanzania, hili wamelifumbia macho na kujifanya hawaoni kinacho endelea.
Hivi ni kweli Serikali imeshindwa kabisa kutoa bei elekezi kwa Biashara ya upangishaji? Au imeshindwa kupunguza gharama za Umeme kwa Watanzania ili waweze kupambana na changamoto za joto na mambo mengine mfano Dar es Salaam.
Matumizi ya Simu, Serikali imeshindwa kutoa bei elekezi kwa matumizi ya muda wa mawasiliano kwa mitandao ya simu ili kupunguza umiliki wa sim cards zaidi ya moja kwa wananchi wake? Inamaana hao watu hawana msaada kwa watanzania, au uwezo wao wa kiutendaji umeishia hapo tu.
Tuzungumziapo economic sustainability sio ule wa up and down, it is stable economic, ndio maana nikazungumzia gharama anazo tumia mtanzania. Huwezi kupata 100,000/- leo ukatumia 90,000 ukasema the economy is stable utakuwa punguwani. We are talking about savings. Watanzania wengi wanakufa kwa kushindwa kufikia gharama za matibabu, and this is becase we are not stable. Nachelea kusema tokea mwaka 2005, hakuna economic development niliyo iona tanzania.