Bado natibu Majeraha

Bado natibu Majeraha

Mentor

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2008
Posts
20,334
Reaction score
23,945
Bado natibu majeraha


​
Simu yangu iliita nami nilipoitoa mfukoni nilikuta ni rafiki yangu tunayefanya naye kazi pamoja kwenye kampuni moja ya mitandao hapa hapa mjini, sema yeye yupo upande wa utawala. Ni rafiki yangu pia kwa kuwa tunaishi wote jirani.

Mentor: “Oyo niambie”
Fredy: “Uko wapi, nina mzigo wako”
Mentor: “Nipo data centre ya floor ya nne”
Fredy: “Poa nakuja, Nina mzigo wako”

Nikakata simu na kuendelea na kazi zangu huku nikimngojea. Alifika na kunikabidhi simu huku akiniangalia kwa jicho la kutaka kuelezwa nini zaidi. Ni simu ile ile niliyokuwa nimemnunulia baby G (wifi/shemeji yenu alipenda kuitwa hivyo)

22 February 2013, Ijumaa – JNIA

Nilikuwa narudi kutoka kozi fupi ya mawasiliano ya kimitandao jimbo la Guangzhou, China. Baby G alikuja kunipokea uwanjani pale, kipenzi changu G. Ilikuwa furaha isiyo kifani kwani kwa takribani miezi minne tulikuwa tukiwasiliana kwa kupitia facebook pekee tena akiwa ofisini kwani hakuwa na hizi ‘smart phone’. Tulirudi hadi chumba nilichopanga huku akiwa na shauku ya hadithi za yaliyojiri pindi nilipokuwa huko China. Tuliongea mengi sana pamoja na kumuonesha picha hadi mida ya usiku sana ambapo tulilala kutokana na uchovu wa safari.

Asubuhi na mapema nilimwamsha G na kumzawadia zawadi ya simu Samsung SIII niliyomnunulia wakati nipo nchini China. Ilikuwa pia ni kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa. Alifurahi sana nami pia nilifarijika kuona ameifurahia zawadi ile. Ulikuwa ni mwisho wa kuwasiliana kwa sms za kawaida na kuelekea kwenye ulimwengu wa dijitali. Sasa tunaweza kutumiana hata picha, jambo ambalo lilikuwa likinipa huzuni wakati nipo mbali naye kwani unatamani kuona hata picha yake lakini ndo hivyo tena anatumia Nokia Jeneza!

Maisha yaliendelea na siku zikageuka wiki na hatimaye miezi tangu nirudi bongo.

May 2013

Kwa muda mrefu, mpenzi wangu huyu alikuwa na tabia ya viuongo vidogo vidogo ambavyo mimi kwa kweli vilinikera na ama hakika nilikuwa nikimwambia kila nikivigundua. Viuongo ambavyo havikuwa hata na haja ya kuvisema maana havibadili chochote.

Kuna siku tulikutana na rafiki yake mmoja wa kike. Katika kupiga soga zao nikamsikia akimwambia, ‘Yani wewe G hujaachaga tu uongouongo wako!’ Nilishtuka ila moyoni niliendelea kutafakari nini mustakabali wa uongoungo wake.

Ilifika kipindi tulikubaliana kuwa kila atakapotaka kwenda atakuwa ananitaarifu kabla ya muda ili kumuepusha yeye kunidanganya inapotokea nampigia simu na kumuuliza. Hii ilitokea baada ya mwenendo wake wa uongo kuwa mwingi na mimi kugundua nyakati zote bila yeye kufahamu nimegunduaje.

Ukweli ni kuwa, wakati nimeinunua simu niliyompa baby G nilikuwa nimeifanyia ‘settings’ zote kupitia barua pepe yangu. Nilifanya pia ‘backup’ kwenda kwa barua pepe yangu, mambo ambayo baby G hakuyafahamu. Hivyo, wakati akifanya yote hayo na kunidanganya, nilikuwa nikijua na kwa hiyo ninapomuuliza na kumbana anashindwa kukataa.

May 2013, 10[SUP]th[/SUP]…Alhamisi

Jana yake baby G alinitaarifu kuwa tarehe ya leo angeenda kumsalimia mama yake mkubwa huko Mikocheni kwani alifiwa na baba mkwe na hakuwa ameenda kumsalimu. Nilimwambia itakuwa sawa na amsalimie akifika.

Jana yake hiyo hiyo, baby G alianza kuwasiliana na mume wa rafiki yake. Walikuwa wakipanga mipango ya kukutana leo. Kwa nilivyokuwa nikifahamu, huyu bwana ameoa na mkewe alikuwa safarini mkoani Mbeya alikokwenda kujifungua. Nilikaa kimya kama sifahamu chochote.

Alianza safari mida ya saa tatu asubuhi kuelekea kwa mama yake mkubwa. Alinitaarifu kuwa yupo njiani huku ujumbe huo huo ukitumwa kwa ‘mchepuko’ wake huo. Walianza kuelekezana jinsi ya kufika safari ambayo kupitia google map nikiwa ofisini ilichukua njia ya Kilwa road.

Akiwa huko kwa mama mkubwa nilimwomba tu anitumie picha ya mandhari ya kwa mama mkubwa naye bila hiyana alimwomba ‘mama mkubwa’ ampige picha kisha nikatumiwa. Picha hii niliitaka kama ushahidi atakapokana kuwa hakuwa kwa ‘mama mkubwa’ bali alikuwa kwa mama mkubwa.

Kufupisha mkasa…

Mida ya kutoka kwa mama mkubwa iliwadia ambapo alinitaarifu. Nilimtega kumuuliza kama angepitia barabara ya Morogoro au Ali Hassan Mwinyi. Alinijibu kuwa angepitia Ali Hassan Mwinyi. Kimshale kwenye kompyuta yangu nacho kikaanza kusonga kutokea huko Kilwa road kilipokuwa kimesimama kwa takribani masaa sita kuelekea Posta.

Akiwa safarini nilimwomba akifika kituo cha Red Cross kukaribia Posta aniambie. Hapo ndipo ugomvi ulipoanzia. Alianza kulalamika kuwa amechoka na alitaka kupitiliza kwenda nyumbani. Nilimwambia kuwa akifika kituoni hapo ashuke kwani nilikuwa nikimngojea twende wote nyumbani. Baada ya kutoa visingizio vingi vilivyoshindikana hatimaye alikata tama kuendelea kubishana na kuamua kukubali kuja.

Alifika kwa pikipiki kituoni hapo nilipokuwa nikimngoja na nilipoanza kumuhoji kisa cha kuja na pikipiki ulianza ugomvi mwingine wa “Unafanya yote hayo kwa kuwa huniamini tu”. Nilikuwa nina hasira sana juu yake lakini nilijitahidi kuzizuia. Kama kuukoleza moto, tukiwa katika kubishana uliingia ujumbe kwenye simu yake. Nilimpokonya simu na kuusoma. Ulitoka kwa yule ‘mama mkubwa’ wa Kilwa Road ukisema, ‘Umemuwahi huyo mchepuko wako?’

Nimekuwa peke yangu tangu wakati huo.

Wasalaam wapendwa,
Mentor.

NB: Mwezi mmoja baadaye ilikuja kugundulika kuwa hata yule mtoto aliyezaliwa hakuwa wa ‘mama mkubwa’ wa Kilwa Road na baba halisi wa mtoto alikuwa huko huko Mbeya mama mtoto alikokwenda kujifungua.

 
One of my favourite quote ,It is impossible to go through life without trust, That is to be imprisoned in the worst cell of all, oneself
 
Mentor
You got what you deserved for violating the poor girl's privacy! You had no right copying and backing up her stuff ! That said maisha is nothing but choices! In your case you have an option to either accept then deal with the consequences of her lies/cheating or move on and find a trustworthy lady. Achana na mambo ya kuplay detective while you know your heart cant handle the truth!!!
 
Du umeikatiza pabaya
hii simu ulimnyang'anya siku hiyohiyo
au mliachana kwanza du sijui alienda oga
au alichukua Bodaboda na nguo zake?
Pole Mentor
 
Last edited by a moderator:
Wazee hawakuwa wajinga waliposema 'ukimchunguza kuku hutomla'

Wahenga hao hao walisema, 'forewarned is forearmed'

I saw the signs...nikimwambia anabisha..nikampatia proof! I guess kwa kuwa nilikuwa Polisi ndio maana nilikuwa na akili hizo!


Pole sana,asante Mentor kwa story nzuri,kila siku unatendwa tu?

Asante everlenk, '..ipo siku nitafanikiwa...'

pole Mentor kila siku unatendwa nasubiri story yako na mwallu lol

hiyo itakuwa special edition!

IM HAPPILY MARRIED! I quoted!

It's a wish my dear lara 1 ...it's a wish. And one day, yes! Nitakuwa kama Matola na wewe!!!
 
Last edited by a moderator:
Mentor
You got what you deserved for violating the poor girl's privacy! You had no right copying and backing up her stuff ! That said maisha is nothing but choices! In your case you have an option to either accept then deal with the consequences of her lies/cheating or move on and find a trustworthy lady. Achana na mambo ya kuplay detective while you know your heart cant handle the truth!!!

You said it all...! Truth is hard to swallow..
 
Fred ndio mama mkwe!!??? Ila umesema ni jirani.....simu kaitoa wapi??

- Fred ni rafiki yangu tunafanya naye kazi
- Fred tunaishi naye kigamboni
- Fred alipewa simu anirudishie kisa we broke up! (x)mpaka hapo?(x)

haamini katika mapenzi ya kweli.

Naamini!

Hello miss neddy.....nakumiss na kaka zangu nawamiss sana.....wacha tulale .....atahadisiaga tukiachana labda

Mh! Mbona watangoja sana juu ya hilo my wife??

One of my favourite quote ,It is impossible to go through life without trust, That is to be imprisoned in the worst cell of all, oneself

KANDIRI, trust is earned! Tangu mwanzo sana nilipata wasiwasi. I just had to prove to her that I know.

Mentor
You got what you deserved for violating the poor girl's privacy! You had no right copying and backing up her stuff ! That said maisha is nothing but choices! In your case you have an option to either accept then deal with the consequences of her lies/cheating or move on and find a trustworthy lady. Achana na mambo ya kuplay detective while you know your heart cant handle the truth!!!

My heart managed to handle it perfectly well. Kwamba sijawa na mwingine since then haimaanishi sijaweza, ni kwamba tu am taking my time finding the right one...

Mmh aisee majanga!

Sema wewe jembe afrika! Nikisema mimi naambiwa nilimuonea...

Du umeikatiza pabaya
hii simu ulimnyang'anya siku hiyohiyo
au mliachana kwanza du sijui alienda oga
au alichukua Bodaboda na nguo zake?
Pole Mentor

hNilimrudishia baada ya kusoma meseji! Na ukawa mwisho maongezi kwa siku hiyo. Baadaye ndio alimtafuta Fred akampa anirudishie!
 
Last edited by a moderator:
Hello miss neddy.....nakumiss na kaka zangu nawamiss sana.....wacha tulale .....atahadisiaga tukiachana labda

tunakumiss pia my dada hahhahaa kuachana kwenu haiwezi kutokea mpe ruksa atuhadithie mlivyokutana lol
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom