Bado natafuta jambo moja tu la maana ambalo serikali awamu ya tano wamefanya

MWAKITWINO

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
227
121
Wanajamvi mimi binafsi sijui nyinyi wenzangu bado najaribu kutafuta walau jambo moja tu la kupigiwa mfano ambalo serikari hii pamoja na mh mkuu Jpm wamefanya tangu waingie madarakani. Watu wengi ukiwauliza utasikia; 1) kanunua ndege au 2) Tzr fly over au wengine utasikia watu walikuwa wanapiga sana bwana jamaa kakomesha!
Mimi binafsi na wazarendo wengi tunaona huu ni upofu mkubwa ngoja tuende mojamoja
1) NDEGE; Mimi sioni lolote la maana mpaka sasa kwanza ndege kila siku zina safiri empty kwani gharama zake ni kubwa kuliko ndege nyingine wewe google nauli za kesho mashirika yote ya ndege utaniambia!
Pili kwani tz shida ni ndege??? Nauliza tu.
2) TZR fly over, sijui nisemeje! ni hivi; katika fly over za kizamani na zilizo pitwa na wakati ni hiyo tzr fly over Je unajua kwamba fly over ile haina matoleo ya juu? Yaani ukitaka kwenda buguruni toka mjini ni lazima usubiri foleni ya magari toka buguruni! Hivyo hivyo viceversa. Maana yake ni kwamba fly over ina msaada kwa mtu anaye toka au kwenda Airport tu! Hivyo taa bado ziko palepale maana yake foleni bado itakuwa palepale. Nitaweka video hapa uone ukweli au nenda you tube utaona ukweli huu. Najiuliza ni nani alitushauli ujinga huu? Kwa maana kalne hii kuna hata roud about za kisasa ambazo zime dizainiwa magari yanapishana bila kusubiriana sasa hii yetu unaondoaje foleni?? chunguza!!
3) WATU WALIKUWA WANAPIGA SANA!
Hili mi najiuliza Mbona bajeti imeongezeka kwa mwezi Mfano mishahara ya wafanyakazi wote kutoka Billion 520 kwa mwezi wakati wa kikwete mpaka Billion 578 kwa sasa??? Majibu rahisi tulipata pale ikulu siku ile na waandishi eti tunalipa malimbikizo ya walimu, kweli? Mbona ktk bajeti wizara ya fedha wametenganisha matumizi?? Mbona imepanda licha ya kuondoa wafanyakazi hewa hakuna posho, safari wala etc?? Pili tumeambiwa wafanyakazi hewa 17000 lakini hakuna hata mtu mmoja aliyekamatwa mpaka leo kwa kula mishahara miwili! Kweli hata mmoja mahakamani! wakati wizi ni kosa la jinai!! Jamani niambieni jambo moja tu ambalo serikali hii imefanya jamaniii
 
Attachments

  • BKqYvI2Aeid.jpeg
    BKqYvI2Aeid.jpeg
    49.9 KB · Views: 118
Hata hii ya madawa ya kulevya ni propaganda kubwa ya kufunika nakisi/mapungufu makubwa ya pesa ndani ya serikali ....mambo yamekwama kabisa na hayatekelezeki.

Wameamua mwezi wote wa pili waimbe bangi,kokeni,heroin,cha ajabu waliowakamata wote wameachiwa.

Bado kuna sakata la unga wa sembe ambao sasa unaelekea Tsh 2000 na hakuna anayetolea kauli,kumbuka ugali ni chakula cha kila siku kwa kila familia.....natabiri ifikapo April bei ya sembe itakuwa 2500-3500 kwa kilo,

Bado hakuna anayetoa kauli,wote wako bize na bange na kokeni ambayo kimsingi sio dharura kwa taifa kwa kuwa si tatizo la jana au juzi,lina karne nzima,kokeni sio kama kipindupindu au Ebola.
 
Mmeachana na Makonda sasa mmehamia kwenye mambo ambayo pengine yanawazidi upeo katika kuyachambua.

Mkuu Tanzania yetu inafunguliwa kila kona. Usitazame abiria wachache wa leo hii ukasahau kwamba ndani ya miaka michache mtu atatoka Ulaya na kuja Dar halafu akaenda mikoani kufanya utalii na biashara nyinginezo.

Fly overs huenda na ukuaji wa miji mikubwa, zinahitajika sana Dar kuliko mleta mada anavyojaribu kuondoa umuhimu wake.

Fedha haiwezi kuingizwa kwenye mfuko wangu na wa mleta mada. Yanatengenezwa mazingira ya watu wa kawaida kuweza kufanya mambo makubwa kiuchumi.

Wananchi huko vijijini wanakabidhiwa hati za ardhi kila kukicha. Idadi ya watumiaji umeme na maji inaongezeka kila kukicha, ukikaa Dar mbele ya laptop yako ni vigumu kuutambua ukweli huo.

Ndio maana upinzani huwa unashindwa halafu watu wanabaki kutafuta sababu za kushindwa. Mazungumzo mengi ya ukosoaji wa kinachofanywa na serikali hufanywa na watu ambao siku za uchaguzi huwa hawana impact yoyote kwenye upigaji kura.
 
MWAKITWINO vipi hilo la kukufanya uanze kutafuta jambo la maana walilofanya sio jambo la maana
Natambua katika kutafuta jambo la maana waweza kukuta na mambo ya kipuuzi, ya kuudhi, ya kufurahisha na ya kuchekesha pia na kukufanya ujifunze kitu kipya katika utawala huu...
 
bkqyvi2aeid-jpeg.473410

mimi nilidhani unapongeza kuwa kwa miezi, tumeleta huyu bombadia, na nyingine zinakuja. Hii picha ni uthibitisho unamatatizo ya kuona vitu vizuri
Mkuu hivi bombadia nauli kiasi gani hadi mwanza ? Isije kuwa unashangilia pasipo kufaidi ujio wake. Mimi sijapata kauwezo ka kuzitumia hivyo manufaa yake kwangu na jamii inayonizunguka ni 0
 
bkqyvi2aeid-jpeg.473410

mimi nilidhani unapongeza kuwa kwa miezi, tumeleta huyu bombadia, na nyingine zinakuja. Hii picha ni uthibitisho unamatatizo ya kuona vitu vizuri
Yaani kutoka kutumia Jet engine kwenda mapangaboi ya feni ndio kitu cha kupongeza?

Kijana wangu nikimnunulia feni mbili,moja akashika kushoto ingine kulia halafu akakimbia,anaweza kupaa,atafanana na bombadia kabisa
 
Kijana wangu nikimnunulia feni mbili,moja akashika kushoto ingine kulia halafu akakimbia,anaweza kupaa,atafanana na bombadia kabisa[/QUOTE]
Hapo ndipo ulipokwamia kufikiri mkuu.
Tanzania Buying New Planes for Troubled National Airline to Boost Tourism
Bombardier Wins Orders for Two CS300 and One Q400 Aircraft from Tanzania - Bombardier
http://www.bizjournals.com/seattle/...-orders-a-new-boeing-787-8-dreamliner-to.html
Boeing_787-8_Dreamliner,_All_Nippon_Airways_-_ANA_AN2064627.jpg

hii nayo siku ikitua utamfunga mtoto wako mitungi ya gesi makwapani umuite DeamLiner acha kumdhalilisha mtoto wako mkuu
 
Mwasita Moja

Mkuu;
Sijui ni kutokukuelewa au nini. Huyu mtu aliuliza jambo zuri tu ila tatizo la ccm tunashindwa kutetea kile tulicho weza. Badala ya kumjibu kuhusu ujinga wao, hebu tumjibu kuhusu hata hayo hayo anayo tunanga nayo kwani si ni kweli tumefanya hayo?? Onyesha matunda mkuu achana na kuwananga wenzio.
Ningemwambia kuwa, hakuna kiongozi yeyote aliyewahi kutumbua majipu makubwa ka JPM. Tena bila hata ganzi. Hayo tu ni mafanikio kwa mda huu mfupi alokalia kiti
 
Mkuu hivi bombadia nauli kiasi gani hadi mwanza ? Isije kuwa unashangilia pasipo kufaidi ujio wake. Mimi sijapata kauwezo ka kuzitumia hivyo manufaa yake kwangu na jamii inayonizunguka ni 0
Sio lazima watanzania wote wapande ndege chief, muulize ndugu yako kama enzi za hiyo boing dar nzima walienda mwanza kwa ndege. Akipanda mtalii kuna economic multiplier ambayo itakufikia wewe hukohuko ufipani. Inabidi utanue uwezo wa kuona vitu kwa kina.
Ombea mafanikio, Usiwe nabii wa maangamizi au mabaya
 
Mmeachana na Makonda sasa mmehamia kwenye mambo ambayo pengine yanawazidi upeo katika kuyachambua.

Mkuu Tanzania yetu inafunguliwa kila kona. Usitazame abiria wachache wa leo hii ukasahau kwamba ndani ya miaka michache mtu atatoka Ulaya na kuja Dar halafu akaenda mikoani kufanya utalii na biashara nyinginezo.

Fly overs huenda na ukuaji wa miji mikubwa, zinahitajika sana Dar kuliko mleta mada anavyojaribu kuondoa umuhimu wake.

Fedha haiwezi kuingizwa kwenye mfuko wangu na wa mleta mada. Yanatengenezwa mazingira ya watu wa kawaida kuweza kufanya mambo makubwa kiuchumi.

Wananchi huko vijijini wanakabidhiwa hati za ardhi kila kukicha. Idadi ya watumiaji umeme na maji inaongezeka kila kukicha, ukikaa Dar mbele ya laptop yako ni vigumu kuutambua ukweli huo.

Ndio maana upinzani huwa unashindwa halafu watu wanabaki kutafuta sababu za kushindwa. Mazungumzo mengi ya ukosoaji wa kinachofanywa na serikali hufanywa na watu ambao siku za uchaguzi huwa hawana impact yoyote kwenye upigaji kura.
We nawe ni mtetezi feki usiye jua kitu biashara yeyote huwa na viashiria vya au kuendelea au kufa au kudumaa sasa kwa mtaalamu wa uchumi yeyote ana majibu ya nini kinacho enda kutokea mbeleni kuanzia kwenye dier bomba,viwanda na uchumi kwa ujumla ,ila ukiwa shabiki huwezi kuyaona haya na utawaona wanao yaoina kama wajinga na ni desturi wa mashabiki wajinga kupingana na ukweli halisi
 
Yaani kutoka kutumia Jet engine kwenda mapangaboi ya feni ndio kitu cha kupongeza?

Kijana wangu nikimnunulia feni mbili,moja akashika kushoto ingine kulia halafu akakimbia,anaweza kupaa,atafanana na bombadia kabisa
Hayo ni maneno ya kwenye kanga, ni aibu kuona mwanaume mwenye akili timamu akiyatumia mbele za watu.
 
We nawe ni mtetezi feki usiye jua kitu biashara yeyote huwa na viashiria vya au kuendelea au kufa au kudumaa sasa kwa mtaalamu wa uchumi yeyote ana majibu ya nini kinacho enda kutokea mbeleni kuanzia kwenye dier bomba,viwanda na uchumi kwa ujumla ,ila ukiwa shabiki huwezi kuyaona haya na utawaona wanao yaoina kama wajinga na ni desturi wa mashabiki wajinga kupingana na ukweli halisi
Mkuu pale kigamboni eneo la ekari 1500 limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vidogo, kuliko kupiga kelele za ukosoaji, cha muhimu ni kuunganisha nguvu ili fursa kama hiyo isitupite.

Kukaa chini na kukosoa halafu anakuja mhindi au muarabu anatajirikia fursa ambazo kwa haki kabisa ni za kwetu, ni jambo ambalo halipaswi kuendelea kuwa sehemu ya maisha yetu.
 
Mkuu;
Sijui ni kutokukuelewa au nini. Huyu mtu aliuliza jambo zuri tu ila tatizo la ccm tunashindwa kutetea kile tulicho weza. Badala ya kumjibu kuhusu ujinga wao, hebu tumjibu kuhusu hata hayo hayo anayo tunanga nayo kwani si ni kweli tumefanya hayo?? Onyesha matunda mkuu achana na kuwananga wenzio.
Ningemwambia kuwa, hakuna kiongozi yeyote aliyewahi kutumbua majipu makubwa ka JPM. Tena bila hata ganzi. Hayo tu ni mafanikio kwa mda huu mfupi alokalia kiti
Unajua kwamba wengine wa hao majipu ni mabalozi nje??
 
Back
Top Bottom