Bado nakulilia Tanzania

boyson onlye

JF-Expert Member
Sep 13, 2015
1,103
1,382
Tanzania bado nakuwazia sana katika kichwa changu hasa kipindi hiki cha uchaguzi na mambo jinsi yanavyoendaa mmmh nazidi kuumizwa na Tania zako Niemani ukitaka kumtawala mtu utakavyo mnyime vitu viwili;

1: Elimu
2: Chakula

Vitu hivi utamfanya mtu vyovyote utakavyo.

Tanzania nakumbuka ule mwaka ambao wewe Tanzania na china uchumi wenu ulikuwa sawa (sikumbuki vizuri mwaka gani) lakini Leo unamuomba China msaada na huyo China uchumi wake unaipita America bado Tanzania unafurahi kwa hapo ulipo.

Tanzania unakumbuka wewe na Kenya. Wewe ndiye ulianza kuwa huru kujitegemea Leo hii Kenya anakuja kuwekeza kwako bado unafurahia Tanzania.

Tanzania watu wako nazidi kuwashangaa kila nikiwatafakari hasa pale napokumbuka kuwa tuna kila aina ya malighafi watu wako hawakumbukii na wanakosa uchungu jinsi malighafi izi zinavyotumika. Watu wako wanapenda watu wao baada ya kuipenda nchi yao.

Tanzania labda MFUMO wa elimu yetu haufundishi uzalendo kama vile nchi nyingine. Nilijiuliza kwa nini mtoto wa Korea anaichukia Marekani nikagundua kuwa wanafundishwa na kuambiwa madhaifu ya Marekani dhidi ya Korea.

Lakini mtanzania anajua madhaifu ya kile anachokipenda bado anajifanya amesahau ili amkomoe yule anaemuona mpinzani lakini mtu huyu angejiuliza kile anachokipenda kimemtesa kiasi gani asingekipenda.

Tanzania watu wako wanasifika kwa kujitetea na kuongea sana na ujanja mwingi lakini wanashindwa kuitetea nchi yao na ikawa na viongozi wenye uzalendo na uchungu wa maendeleo.

Tanzania unajua kuwa jirani yako anakuja kwa kasi kimaendeleo? Jina lake Rwanda na ukizubaa tu anakupita najua utasema ningepata kiongozi kama yule ningekuwa mbali sasa ila ndo ivyo kashakupita na itabidi ujikongoje maana huo usafili umeuchagua mwenyewe.

NITAENDELEA KULILIA TANZANIA WANGU..
 
Pole,,, japo naona machozi yako ni sawa machozi ya samaki ndani maaji,, "maskini nchi yangu Tanzania"
 

Machozi yemenilengalenga baada ya kusoma ujumbe wako.

SIKU MOJA MAKABURI YETU YATACHIMBULIWA KWA MAKOSA TUYAFANYAYO LEO, INAUMA SANA JAMANI
 
Back
Top Bottom