Leonard Waziri
Member
- Aug 15, 2013
- 55
- 23
SIRI YA MAFANIKIO YA KUWA TAJIRI.
Hii ni siri ambayo nimekuwa nikiitumia katika maisha yangu binafsi na wengine wengi waliofanikiwa huitumia pia na imewasidia sana kufikia malengo makubwa waliyojiwekea. Kama siri hii ya kupata utajiri imefanya kazi kwao na kwako pia itafanya kazi. Ukiweza kuitumia siri hii vizuri katika maisha yako itakujengea uwezo mkubwa wa kumudu kufanikiwa kwa chochote unachofanya katika maisha yako.
Watu wengi wenye mafanikio wanaijua vizuri siri hii na ndiyo inayowafanya wawe juu siku zote. Wengi wanaoshindwa kufanikiwa na kujikuta mbio zao nyingi zinaishia kati katika maisha yao ni kutokana na kushindwa kuitumia siri hii vizuri, nami sitaki uwe miongoni mwao nataka uwe mshindi ili tuwe pamoja katika kilele cha mafanikio.
Pengine unajiuliza ni siri ipi hasa unayoweza kuitumia na kuleta mafanikio makubwa kwako. Siri hii unayotakiwa kuwa nayo ni siri ya kujikubali mwenyewe na kuamini unaweza kufikia malengo makubwa uliyojiwekea.
Wataalamu mbalimbali wa elimu za mafanikio akiwemo Dr. Vicent Norman Pealle wameeleza hili sana ili uweze kuwa na mafanikio yoyote makubwa ya kimaisha hatua ya kwanza unayotakiwa kuchukua ni kujikubali mwenyewe na kuamini kuwa uwezo huo wa kufanikiwa unao.
Haijalishi watu wengine wanasema nini juu yako iwe kwa mabaya au mazuri, udhaifu fulani au ubora kinachotakiwa ni kujikubali mwenyewe na kuamini unaweza kufikia mafanikio yoyote bila ya kuzuiliwa na kitu chochote kumbuka ndani yako una uwezo mkubwa sana kuliko unavyofikiri.
( Soma Kama Unafikiri Umechelewa Na Umekosea Sana Katika Maisha Yako )
Wengine wanasubiri mpaka wasifiwe katika nyanja fulani ya maisha ndipo wajikubali wenyewe kuwa wanaweza kufanikiwa na wanapokuwa wanaacha kusifiwa basi kujikubali huanza kufifia pole pole na pengine kufa kabisa. Kitu usichokijua unaposhindwa kujikubali mwenyewe na kuamini kuwa unaweza kufanikiwa unakuwa unazuia mafanikio mengi sana ambayo yangeonekana kwako. Hiyo inakuwa ni sawa na kupoteza maisha yako.
Tatizo walilonalo watu wengi kutokana na mazoea yao au malezi waliyokulia huwa sio rahisi kujikubali wenyewe na kuamini kuwa wanaweza kufanikiwa na kufikia mafanikio makubwa kabisa katika maisha yao. Ni wepesi sana kuwakubali wengine kutokana na yale wanayoyafanya kuliko kujikubali wenyewe.
Watu wa namna hii mara nyingi huwa sio rahisi kusimama peke yao kwenye maisha na kufanikiwa, kwani wao wanaamini wapo watu wanaoweza zaidi yao kufanikiwa na kujikuta ni watu wa kujishusha tu na kujiweka pembeni na kusubiri hao wanaoweza waweze. Ni kweli kutokana na kutokujikubali kwao hao wanaoweza hujikuta wakiweza kweli huku wenyewe wakijikuta wakiwa ni watu wa kushindwa katika mambo mengi katika maisha yao.
Jiulize mwenyewe binafsi unajikubali na kujiamini kwa kiasi gani kwamba unaweza kufikia ndoto na malengo yako uliyojiwekea bila ya kuzuiwa na kitu chochote kile. Kama hujiamini ujue kabisa kwako itakuwa ngumu kufikia ndoto zako. Chukua hatua ya kujiamini ili uweze kuishi maisha ya mafanikio unayo tamani kila siku kuyafikia.
Hii ndiyo siri kubwa ya mafanikio unayopaswa kuitumia katika maisha yako. Nakutakia ushindi mkubwa katika safari yako ya mafanikio.