Wakati ule ilikuwa ni sawa tu kujifanyia mambo tunavyopenda, liwe ndani au nje ya maadili au sheria. Bahati nzuri zaidi aliyekuwepo pale juu hakuwa na mikakati wala weledi wa kutosha wa kutuongoza kwenye mstari unaokubalika (pamoja na kelele zoote za wakati ule...rushwa! mafisadi! ubadhirifu, nk,). Huenda hata muda hakuwa nao wa kujiuliza je tunayoyafanya yana athari zipi? Au pengine alizidiiwa na shinikizo la kuhitaji apendwe na kila mtu basi mambo yakawa hivyo. Lakini, hivi na sisi tuliamini kabisa kuwa mambo yatabaki hivyo hivyo milele? Mwalimu mzuri ni wakati, na amekuja tupa somo la nguvu, kupitia mabadiliko ya wakati, tukubali viboko vyake ! Hatuwacheki, maana si ajabu hata wengi wnanaowazodoa leo wangefanya hayo hayo mlioyafanya nyinyi wangelikuwa katika nafasi zenu, na bado wengine watawafuateni......ni mambo ya nyakati!