Badala ya kuichoma bhangi yetu, tuichakatie kiwanda cha mkonge. Kuichoma tukiwa high nchi nzima?

Uhakika Bro

JF-Expert Member
Mar 29, 2022
2,398
3,074
Nishawahi kumtania Mkurya mmoja kwamba: 'Unajua ni kwa nini nyie kwenu (huko ukuryani) mna hasira sana bro? Ni kwa sababu serikali kila mara inawavutisha bangi maana ikikamata na kuchoma mabangi ma tani kwa mahekari basi ule moshi unasambaa mkoa mzima ndo unakuta wote ni kama wavuta bhangi tu (enzi hizo kimakosa niliamini bhangi huleteleza hasira kumbe sio). Bhangi hujenga tu focus ya kile mtu anaaamini basi.

Kila mara tunasikia mashamba na ma kilo na ma tani ya bhangi yameteketezwa.

Hivii; bangi ikichomwa haitoi moshi? ivi hivyo vipande havirudigi kweli hata na mvua kuja kutulewesha baadae? Utashangaa tu ka mvua kakinyesha watu wanafurahii, mood zinakuwa smooooth🤗. Wengine wanarelaax hadi hamu za kuchakatana zinakuja😁😁.

Onaa tuwe siriazi, achana na hiyo high, ni kama kusubiria mvua inyeshe idondoshe samaki (myth sijui kweli!). Lakini CBD na THC etc ni molekyuli ndogondogo tu hazifanani na samaki au mayai yake. Anyways.

Nilisema tuwe siriazi, ona. Badala ya kuchoma bhangi tuichukue tuichakate tupate nyuzinyuzi zenye matumizi kede wa kede.

Na kama hizi bhangi zetu hazitoi hiyo bidhaa basi wakulima watafutiwe mbegu bora zenye kuzaa zaidi.

Nimeona mahala kuwa hizi nyuzi ni imara sana, na zinaweza hata kuzuia sauti na joto kupenya.

Sasa kwa kuzijua sifa hizo mainjinia wetu watatuboreshea maisha kwa;

Kuweka kwenye kuta za kumbi za starehe ili sauti zisitoke nje

Wabunifu wa majiko wapate kuzuia joto kupotea kuongeza ufanisi

Nguo za kuzuia moto

Majumba yasiyoruhusu majanga ya moto kusambaa

Sijui na mengine mengi tu tafiti zitasema. In fact tafiti zitachunguza hata hayo matumizi yaliyoandikwa hapo juu kama ni feasible?

Screenshot_20231011-090157_Chrome.jpg
 
Asee maoni yenu wa bhangi na marastaman pia yanatakiwa hapa hii mada hamuioni, eeh watunga sera mpo wapi?

Mi nawawakilisha wanasayansi wanamageuzi.
 
Back
Top Bottom