Badada ya Manji kuondoka, Yanga ilikopa 500M

Fredwash

JF-Expert Member
Oct 27, 2009
1,041
1,377

Kaimu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga baada ya kusema wakati Manji yupo ndani ya uongozi wa klabu hiyo alikuwa anachangia pesa kama mfadhili, inawezekana swali linalokuja akilini mwako sasa hivi Yanga inapata pesa kutoka wapi?

“Wanachama na wapenzi wa Yanga lazima watambue nguvu na mchango wa uongozi ambao upo madarakani, katika kipindi cha miezi 18 tumeweza kulipa mishahara ya miezi 16.”

“Wakati tunaingia tulijikuta tuna changamoto nyingi sana kuhusu suala la mishahara, tayari kulikuwa na madeni wakati huo tulikuwa tunatakiwa kushiriki michuano ya SportPesa. Tulichokifanya tuliwaambia hatuwezi kushiriki mashindano hayo kwa sababu wachezaji wengi walikuwa wamefikia mwishoni mwa mikataba yao.”

“Baada ya kuzungumza nao (SportPesa) walikubali kutukopesha pesa ambazo zipo kwenye mkataba wetu kiasi cha shilingi 500M tukaweza kulipa mishahara ya nyuma na hela nyingine tukaingiza kwenyr usajili.”

“Baada ya hapo tumekuwa tunatumia mbinu mbalimbali za kupata pesa za kulipa mishahara mbinu ambazo si vizuri sana kuzizungumzia kwenye vyombo vya habari lakini nitawaeleza wenye timu ambao ni wanachama siku ya mkutano.”

Maisha ya Yanga kabla na baada ya kuondoka Manji


Kwenye kipindi cha Sports Xtra cha Jumanne Juni 4, 2018, kaimu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga alizungumza mambo mengi yanayohusu klabu hiyo.


Miongoni mwa mambo ambayo aliyadadavua upana ni maisha ya Yanga kabla na baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuf Manji.

Tunashukuru kwa alichofanya Manji katika kipindi chote ambacho alikuwa madarakani na kabla ya kuwa madarakani wakati huo akiwa mdhamini wa klabu, amekuwa ni msaada mkubwa.


Kila mwanachama na mpenzi wa Yanga anajua maisha tuliyokuwa nayo wakati huo, Manji alikuwa mpiganaji na timu iliweza kufanya vizuri kwa kipindi chote ambacho alikuwepo.


Katika kipindi cha hivi karibuni wakati Manji yupo Yanga tuliweza kusafiri nje ya nchi kwa ajili ya kambi mbalimbali hakukuwa na tatizo la kulipa mishara, ilikuwa inalipwa kwa wakati.



Aina ya wachezaji na benchi la ufundi lilikuwa ni zuri sana katika vipindi vyote ambavyo alikuwepo na hakukuwa na dosari.



Tulikuwa na kipindi cha neema kipindi hicho Manji yupo. Alikuwa analipa mishahara ya wachezaji, benchi la ufundi na secreriat kiasi kisichopungua Tsh. 125M kwa mwezi.



Ishu za usajili kwa wastani tulikuwa tunaweza kusajili wachezaji kwa kiasi cha Tsh. 500 hadi 600M.



Kwa hiyo unaweza kuona ni gape kubwa kwa yeye kutokuwepo ndani ya uongozi na kama mfadhili wa klabu ya Yanga.



Alipotangaza kujiuzuli ilikuwa kama mshtuko na katika hali ya kawaida huwezi kutafuta njia ya kukimbia badadala yake unajipanga na kutulia ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.



Tunashirikiana na kamati ya utendaji kwa pamoja na mazingira yaliyoliyopo, tangu Manji ameondoka tulikuwa na deni kama miezi mitatu mapaka leo ni wastani wa miezi 18 ambayo pia nimekuwa nikikaimu nafasi yake.



Katika miezi hiyo 18 uongozi huu uliobaki umeweza kulipa mishahara kwa miezi 16, tuna deni la mishahara ya miezi miwili ambalo tunaendelea kulifanyia kazi kuhakikisha tunakamilisha. Changamoto ni moja, kwamba mishahara ilikuwa haiji kwa wakati katika kipindi chetu lakini kwa kifupi tuna deni la mishahara ya miezi miwili.



Sanga amesema wakati Manji yupo kulikuwa na mfumo kwanza yeye kama Mwenyekiti na mfadhili wa timu alikuwa anaweza kuchangia kwa atakavyoona inafaa kwa wakati huo kwa hiyo alikuwa anasimama kama mwenyekiti na mfadhili wa timu kwa wakati mmoja.



Ndiyo maana waliokuwa wanabeza mpango wa mabadiliko ya uendeshaji alipojaribu kuomba akodishwe nembo ya Yanga wakasema aondoke atakuja mwekezaji mwingine, tangu ameondoka hajaja mtu zaidi ya watu kukimbia.



SOURCE: ShaffihDauda | Sports News and Scores

My take: Ukiangalia hiyo picha ya Manji wakati anaingia ukumbini utaona kuna tatizo. kwani hao wote waliomzunguka Manji unaona hawako kimaendeleo zaid ya tumbo.. Manji alikosea jinsi alivyokuwa anaiendesha Yanga. alitakiwa atumia influence yake ili aibadili Yanga iwe ya kisasa, ili hata kama akiwa hayupo basi yasitokee haya ya leo.. nilitegemea sababu ni mfanyabiashara wa kimataifa mwenye uzoefu angeileta chachu ya yanga kuwa brand ya kimataifa kwa kuiingiza katika mabadiliko ya kimfumo wa biashara .

hivi yule sijui kiongoz wa matawi ya yanga aliekuwa analalamika kuwa wanaonewa na TFF ama sijui wanahujumiwa. alikuwa anayajua haya. maana majibu ya TFF yalikuwa kuwa waliwakopesha yanga... na ss kumbe hata sport pesa wanaidai yanga walikopeshwa nje ya zile fedha za udhamini.

kuna haja ya hawa mifumo ya hiz club zetu kubadilikka, ikibidi zife ilizifufuke zikiwa na sura mpya maana wakiambiwa mabadiliko ya kisasa wanajifanya timu zao...

sasa kama msimu uliopita yanga walikopa kwa ajili ya usajili.. bahat mbaya hawajafikia lengo.. sasa hv je watakopa tena ama ?... ndo hakuna usajili.. nilitegemea ipigwe harambee ya chap chap hapo ndo tutajua nani wana moyo wa maendeleo na hiz club wapi wapiga kelele wakidai timu yao.. sio kuja kutaka TFF iwahurumie bila kuleta mipango..

Mi ningeshaur kama vip walau kina Bin kleb na kina Mr Mengi waichukue yanga kwa hisa kama Mo. hata ikibidi mzee JK atie ubani pia ..
 
Back
Top Bottom