Bachelors Club: Tuzungumze

Utafiti unasema chanzo #1 cha mmigogoro ndani ya ndoa
ni suala la upatikanaji na matumizi ya pesa ndani ya nyumba:
nani anatafuta, anatafuta kwa njia gani? nani anatumia,
anatumia kwa kupata vitu gani? nani anaset priorities?
Kuna mengine pia, ngoja niwapishe wana ndoa wataje,
mi nimeleta hili ambalo limesha fanyiwa utafiti (source)

Asante kwa source...........but ningependa kusikia wewe unalionaje hili....najua bado wewe ni mwali lakini utakuwa una uzoefu wa kuishi na kuona au si sivyo umashayasikia mkoleni
 
Kuna ukweli hapa ila mimi nadhani hizi monetary problems hutumiwa kama ngao ya kuhalalisha tu hizo divorce lakini underneath huwa kuna sababu halisi imejificha.
Ohh!!!Let me declare interest kwanza kabla ya kusema mengi Super-Bachelor..

Kwenye chama chetu wewe ni "Senetor"...........hebu funguka zaidi
 
madame gfsonwin, mzee Mtambuzi na mito naomba niwashukuru kwa niaba ya mabachelor na mabachelorette wote wa humu jf. mnatutia moyo sana ili tuwe waangalifu na makini kuingia ktk chama kubwa la TAMU (TAnzania Marriage Union). naomba kuongezea point ndogo sana. wanandoa wanapaswa kuchuliana madhaifu yao na sio kuyafanya yale madhaifu kuwa kigezo cha kumnyanyasa / kumdharau mwenzi wako. bali kumrekebisha kwa upendo kwan hakuna binadamu mkamilifu. . .

Naomba nimtambue kwanza mabachelorette charminglady kwenye club yetu.............Hebu funguka kidogo ni changamoto gani za msingi ambazo unahisi utakutana nazo kwenye ndoa?........unafanya maandalizi gani kukabiliana nazo?
 
Last edited by a moderator:
changamoto ninazohis ama nizionazo ktk jamii inayonizungu ni kama
1. mawasiliano baina ya mke na mume-utakuta mke/mume anaondoka home bila kuaga na pia hasemi ni wapi anakwenda. ni vyema kumuaga mwenzi wako
2.kutoshirikishwa-unakuta mke/mume anafanya jambo bila kumshirikisha mwenzi wake.mf.kujenga nyumba,kununua vitu vya thamani km furniture nk. ndoa ni mwili mmoja inatakiwa kuwekana wazi kwa kila kitu.
3.utatuzi wa matatizo-wanandoa wanapaswa kutumia busara ktk kutatua matatizo ya kifamilia co kutangaz
https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/299499-bachelors-club-tuzungumze-new-post.html
 
Habari wana jukwaa:
Awali ya yote naomba niseme mimi pia ni mseja.
Nikirudi kwenye andiko/mada kuu nitaanza kwa kuchangia kwa jinsi maswali yalivyoulizwa:
1.Katika maandiko matakatifu tunaambiwa;mungu alipoumba ulimwengu, pia alimuumba na mwanadamu(Adamu),baadaye aliona ya kuwa Adamu huyu ni mpweke hivyo akamletea mwanamke (Eva/Hawa) ili akawe mfariji wa Adamu.lakini tunaambiwa kila mtu awe na mume/mke wake.Kwahiyo kutoka maandiko matakatifu naweza kusema ndoa ni zawadi toka kwa mungu,hivyo tunao/kuolewa kutimiza maandiko ya mungu,na katika zawadi hioy ya mungu kwa wanandoa akawapa tendo la ndoa ili wanandoa wapate kufurahi.
2.Changamoto zipo nyingi ambazo mtu anayetarajia kuingia katika ndoa anatakiwa azifahamu;kwangu changamoto kubwa ni kujua kuwa ndoa inajumuisha watu wawili(kwa ndoa za kikristu),kwavile binadamu tunatofautiana kitabia,kihisia,kimapokeo na mengine mengi ni shurti kujua matatizo mbalimbali yanaweza kujitokeza kutokana na tofauti hizo,kwahiyo jukumu kwa watu hao kuweka misingi imara itakayowasaidia kuzikabiri changamoto mbalimbali waingiapo katika ndoa.
3.kwasisi wakristu tunaambiwa pindi watu waunganapo na kuwa wanandoa hakuna anayeweza kutengisha ila mungu mwenyewe,hii inamaanisha mkubalipo kuingia katika ndoa mmekubali kusameheana wenyewe katika makosa mbalimbal na kuifanya ndoa idumu mpaka kifo kitakapowatenganisha.so kwangu mimi hakuna kinachoweza kuvunja ndoa nasisitiza NDOA na si mahusiano ya girlfriend na boyfriend.
Kwa machache hayo naomba kuwasilisha.
 
Aisee mjadala wa side comments upo sredi gani?: Nahisi nitakuwa huko!

Utakuwa humuhumu.........mleta sredi atajua namna ya kutofautisha the rest wewe changia.............Au waonaje senior bachelor
 
Utakuwa humuhumu.........mleta sredi atajua namna ya kutofautisha the rest wewe changia.............Au waonaje senior bachelor

apo senior bachelor nani? gfsonwin humwoni akitiririka huku? khaaa!

kwa ninyi mabachelor nawashauri msiingie kwa vile kila mtu anaingia. Ingia ukiwa unajua kuwa kuna raha na changamoto zake. Muhimu ni kuchukulia changamoto kama njia ya kuboresha zaidi mahusiano yenu ya ndoa na sio kutumika kuifirigisa.
 
Siajelewa hapo kwenye red
 
Nilisoma mahali watu walikuwa wanachangia Yahoo baada ya mmoja kati ya ma superstar kutangaza divorce...moja ya michango mpaka leo naukumbuka...jamaa alisema ndoa za sasa hazidumu kama zamani kwa kuwa baba na mama zetu, babu na bibi zetu walikuwa wana 'collect brocken pieces'...sisi wa kizazi hiki tuna 'throw them away'.

Najua wanaume wengi wanasema kuna kosa ambalo hawawezi samehe, nalo ni uzinzi. Lakini leo hii 90% ya wanawake either walisamehe au wana propensity to forgive cheaters. Nadhani ni sababu ya mfumo dume na ego ya wanaume..kwani kwa nchi za wenzetu wapo wanaume wanaosamehe hilo kosa. Na kama wewe unasamehewa kwa kosa hilo hilo ni kwa nini usisamehe?

Anyway point ni kuwa ndoa ni challenge kwani mmekutana ukubwani lazima kuna lots of differences. Hao ndugu wa tumbo moja tu tuna differ sana sembuse mtu kakulia na kulelewa familia nyingine.

Badala ya nyie mabachelor kukimbia challenges..nawashauri muwe na moyo wa kuzi face...ni kitu kizuri kuwa risk taker na mtu unayependa challenge...kwani hata kwenye usingo cheating zipo...brocken hearts za kumwaga...sioni mnakimbia nini. At least marriage ni commitment unaweza ku claim ownership ya ulonaye. Lol. kwa hiyo kwangu naona kuna less challenges na less risks kulinganisha na u single.
 
Nimekupata nyumba kubwa...............Hebu turudi kwenye huo usingo, ndio kuna cheating, broken hearts n.k lakini usisahau hapo hakuna commitment ya maana na unaweza kusema X ameni-cheat naumia but ikifika jioni naenda kwangu angalau napata muda wa kutafakari na pengine uhuru mkubwa wa kutafuta/kupata ushauri na hata kama linafikia hitimisho la kuachana haligharimu sana (hatuna watoto, mali tulizochuma, ndugu waliounganishwa na ndoa yetu n.k), kwa maana nyingine uhuru ni mkubwa na challenge zipo lakini zinabebeka!

Wakati kwenye ndoa ni hali tofauti kabisa kwa kuzingatia hayo hapo juu
 
Last edited by a moderator:
NIimekupata mito....sasa tuseme ndio hivyo umegundua mapungufu ya mwenzi wako mechanism gani inayotumika ku-solve tatizo ama inategemea utakalofikiria wakati huo?

Samahani nilikuwa kwa kanisa platozoom

Kama nilivyosema wakati najaribu kuchangia mada kuhusu sababu za kuvunja ndoa, mapungufu mengi yanazungumzika na yanarekebishika. Kwa hiyo njia kubwa ni kukaa chini na kuelezana mapungufu yetu kwa nia ya kurekebishana. Hapa sasa cha kuangalia ni approach na lugha utakayotumia. Nadhani huwa unasikia hapa jamvini watu wanashauri kwamba 'mtoa out halafu ukazungumze naye kwa upole uko'. Hii ni approach ambayo wengi tunaitumia, and normaly it works (of course depending on the issue itself). Katika mazungumzo yenu mnaweza kuwa wenyewe tu au mkahusisha ndg, jamaa na marafiki especially kama mmeshindwa kufikia muafaka nyie wenyewe.

Changamoto kubwa ni approach ya mazungumzo yenyewe. Baadhi wanashindwa kufikia muafaka kwa sababu ya jazba, ubabe, na dharau. Uzuri ni kwamba mkishajenga upendo wa dhati (kumbuka upendo unaongezeka au unapungua kadri mnavyoendelea kuishi pamoja) basi ni rahisi sana ku-solve matatizo au mapungufu yenu. Hii ni kwa sababu kila mmoja wenu anakuwa hataki kumkwaza mwenzake, hivyo ni rahisi kurekebisha na kuondoa mapungufu yenu.

Ila usisahau kuwa kuna mapungufu ambayo hayarekebishiki. Njia ya ku-solve tatizo kama hili ni kulikubali kwani hakuna binadamu aliyemkamilifu. Ikitokea kwa mfano unamfundisha au unamuelekeza mwenzio kitu fulani pengine, lakini unakuta hawezi japokuwa unamuelekeza kila mara. Hapo huna hapa ya kuumiza kichwa. Kinachotakiwa ni kukubali kwamba mwenzangu hiki hawezi, then maisha yasonge mbele.
 
Watoto hawafanyi challenges kuwa ngumu ila wanapunguza uzito wa challenge. Mi jamaa akiniboa ninakuwa na sababu ya kuendelea kumvumilia kwa kuwa nimezungukwa na vijana wanaonipenda (wanangu) ambao siwezi kuwatoa kwa baba yao na baba yao hawezi kuwatenga nami. Watoto ni sababu inayofanya kusamehe kuwe possible kwenye ndoa.

Hivyo siwezi kuwa na stress kihivyoooo...nina wafariji wangu (my sons) ambao wanafanya nitabasamu muda wote na hiyo tabasamu nadhani inamfanya jamaa nae hata kama tumenuniana arudishe majeshi.

Nimekupata nyumba kubwa...............Hebu turudi kwenye huo usingo, ndio kuna cheating, broken hearts n.k lakini usisahau hapo hakuna commitment ya maana na unaweza kusema X ameni-cheat naumia but ikifika jioni naenda kwangu angalau napata muda wa kutafakari na pengine uhuru mkubwa wa kutafuta/kupata ushauri na hata kama linafikia hitimisho la kuachana haligharimu sana (hatuna watoto, mali tulizochuma, ndugu waliounganishwa na ndoa yetu n.k), kwa maana nyingine uhuru ni mkubwa na challenge zipo lakini zinabebeka!

Wakati kwenye ndoa ni hali tofauti kabisa kwa kuzingatia hayo hapo juu
 
Ndio maana ndoa zisizo na watoto hazidumu...ni kwa kuwa inachukua muda mwingi kuchekeana pale mnaponuna kama watoto hakuna. Ndani ya huo muda mrefu unakuta mmoja anaamua kuondoka jumla.

Mi mwanangu nikikasirika kidogo tu ameshajua na anataka nimwambie sababu...hivyo hata nikigombana na hubby...nalazimika ku smile mbele ya mwanangu na automatically nakuwa kivutio kwa mume wangu. Ugomvi unaisha bila msamaha. (kama ni ugomvi mdogo)
 
Nilisoma mahali watu walikuwa wanachangia Yahoo baada ya mmoja kati ya ma superstar kutangaza divorce...moja ya michango mpaka leo naukumbuka...jamaa alisema ndoa za sasa hazidumu kama zamani kwa kuwa baba na mama zetu, babu na bibi zetu walikuwa wana 'collect brocken pieces'...sisi wa kizazi hiki tuna 'throw them away'.

Najua wanaume wengi wanasema kuna kosa ambalo hawawezi samehe, nalo ni uzinzi. Lakini leo hii 90% ya wanawake either walisamehe au wana propensity to forgive cheaters. Nadhani ni sababu ya mfumo dume na ego ya wanaume..kwani kwa nchi za wenzetu wapo wanaume wanaosamehe hilo kosa. Na kama wewe unasamehewa kwa kosa hilo hilo ni kwa nini usisamehe?

Anyway point ni kuwa ndoa ni challenge kwani mmekutana ukubwani lazima kuna lots of differences. Hao ndugu wa tumbo moja tu tuna differ sana sembuse mtu kakulia na kulelewa familia nyingine.

Badala ya nyie mabachelor kukimbia challenges..nawashauri muwe na moyo wa kuzi face...ni kitu kizuri kuwa risk taker na mtu unayependa challenge...kwani hata kwenye usingo cheating zipo...brocken hearts za kumwaga...sioni mnakimbia nini. At least marriage ni commitment unaweza ku claim ownership ya ulonaye. Lol. kwa hiyo kwangu naona kuna less challenges na less risks kulinganisha na u single.

unaikumbuka ahadi yetu?five years from last year
tukutane hapa jf au popote nikuulize kuhusu
ndoa na misimamo yako ya sasa....
usisahau....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom