Habari za saizi WanaJF
Baada ya matokeo ya kidato cha sita kutoka,Nina dogo alichukua HKL na kwa balaka za Mungu katunukiwa Div 1.9 yani
History-D
Kiswahili-B
English-C
Gs-E
Asa kwa ufaulu huo anatak kuchukua kozi ya ualim
Sasa mkanganyiko umetokea achukue BA.ED au B.ED
Kwa ushauri wenu WanaJF wajuvi ni programme ipi nzuri na inanumafaa kwake
Ikiwezekana na ushauri wa chuo kizuri kusomea moja ya programme
MSAADA WENU TAFADHARI
Ningemshauri achague kozi tofauti na hizo. Kusomea ualimu ni kusoma uwe masikini hapa TZ.
Hutalala njaa ila maisha yako yatajaa mikopo kuanzia ya benki hadi kule bayport na saccoss.
Aidha, ni kazi ambayo kila kiongozi wa kisiasa akijisikia kudhalilisha mtu au kutukana, anaenda kuwatukana walimu iwe diwani, mbunge, dc/ rc na waziri; hata akitamani kupiga viboko anawafuata walimu na kupiga.
Ni kazi dhalili, mtaani utatambulishwa kwa udhalili mno. Mathalani, watatambulishana kwa heshima na taadhima, utasikia huyu ni Lawyor Abc, yule pale ni Marketing Officer Def, yule pale ni Engineer Ghi, wakija kwako mwalimu watakutambulisha hivi, na huyu mwenzet ni mwalimu Jkl.
Ni kazi pekee ambayo jamii inaona wanasomea ma-failier, "Utasikia hata ualimu umekosa?" Yaani, ualimu ni kazi iliyojalala la kutupia mafailier wo wote wale.
Siku zote mwalimu anakuwa ngazi ya kupandia juu lakini yenyewe haipandi juu.