detective mfaume
Member
- Dec 23, 2016
- 31
- 69
BACHELOR OF ARTS IN LAW ENFORCEMENT UDSM.
UFAHAMU JUU SHAHADA YA USIMAMIZI WA SHERIA INAYOTOLEWA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
UTANGULIZI
Usimamizi wa sheria kama taaluma inayotolewa katika taasisi za elimu ya juu *UNIVERSITIES* ni taaluma mpya katika nchi mbalimbali duniani. Kwa maana nyingine ni kwamba, usimamizi wa sheria katika kipindi cha nyuma ilikua ni kazi ya polisi pekee, na mfumo wa mafunzo ni ule uliokua unapatikana sehemu maalumu kwa ajili ya mafunzo ya polisi pekee.
Utandawazi na ukuaji wa sayansi na teknologia kwa kasi katika karne ya 20 na 21 ni mambo yaliosababisha ugunduzi na uvumbuzi wa mbinu mpya za kiuhalifu na uvunjaji wa sheria. Hii imepelekea uhitaji wa watu maalumu watakao weza kukabiliana kiurahisi na changamoto zinazo tokana na wahalifu na uvunjaji wa sheria kwa ujumla. Wahalifu kila siku wanagundua mbinu mpya za uvunjaji wa sheria na utekelezaji wa matukio ambayo yanavuruga na kuondoa amani ya wananchi.
Kuongezeka kwa majukumu ya serikali katika karne hizi mbili(20 na 21), kutoka katika *LAW AND ORDER STATE* kwenda katika ustawi wa wananchi ambao kitaalamu tunaita *EMERGENCE OF WELFARE STATE* pia ni sababu iliyo sababisha serikali kujigawanya zaidi kimatawi ili kuongeza ufanisi wakiutendaji katika secta mbalimbali, moja wapo ikiwa ni nyanja ya usimamizi wa sheria. Majukumu haya kwa kiasi kikubwa yameambatana na mipango, mikakati yakiutendaji na sera mbalimbali za serikali zinazolenga shabaha ya maendeleo. Sera na mikakati hii imeambatana na utungwaji wa sheria mbalimbali zinazo gusa maeneo husika mfano afya, elimu, chakula, biashara, kilimo n.k.
Kwa upande wa Tanzania hili linajidhihirisha kwa uanzishwaji wa mamlaka ambazo zinahusika na usimamizi wa sheria katika maeneo tajwa, Mf. TFDA, PCCB, TBS, TRA, SUMATRA, TPA, na TCRA.
Maeneo haya yote yanahitaji wataalamu makini wenye ujuzi wa sheria na usimamizi wa sheria, na pia wenye uzalendo na uwezo wakukabiliana na changamoto zinazo jitokeza katika ulimwengu huu wa sayansi na teknologia.
Haya ni mingoni mwa mambo yaliyopelekea kuanzishwa kwa shahada maalumu inayohusu usimamizi wa sheria chuo kikuu Dar Es Salaam inayojulikana kama Bachelor of Arts In Law Enforcement (BA. LE).
NINI SHAHADA YA USIMAMIZI WA SHERIA.
Shahada ya usimamizi wa sheria ni kati ya programu tatu zinazotolewa shule kuu ya sheria chuo kikuu Dar ES Salaam UDSM. Shahada hii inayojulikana kwa kifupi kama BALE, imelenga kutengeneza wataalamu wa masuala ya usimamizi wa sheria, watakao weza kukabiliana kiurahisi na changamoto mbalimbali zinazo jitokeza katika nyanja ya usimamizi wa sheria.
Programu hii ilianzishwa mwaka 2009, kulingana na ombi maalumu kutoka kwa mkuu wa jeshi la polisi,(IGP Mstaafu) Inspecta generali Saidi Mwema.
Kozi inatolewa kwa kipindi cha miaka mitatu na inadahili wanafunzi kutoka mashuleni yaani waliomaliza kidato cha sita na watumishi kutoka vyombo mbalimbali vya usimamizi wa sheria kama vile polisi na majeshi mengine, (wenye stashahada zinazohusiana na usimamizi wa sheria.)
Mwanzoni mwa kozi hii wanafunzi wengi walitoka katika Jeshi la Polisi hata hivyo kadri siku zilivyokuwa zikienda wanafunzi kutoka Jeshi la Polisi walianza kupungua hadi kufikia kipindi cha karibuni wanafunzi wengi ni *freshers* kutoka mashuleni. Mwaka wa masomo 2016/2017 wanafunzi pekee waliodahiliwa ni kutoka kidato cha sita. Mabadiliko haya katika udahili yanaweza kuashiria lengo maalumu, la kuifanya kazi na ujuzi wa usimamizi washeria kuhusisha, wananchi wakawaida, nyanja na taasisi mbalimbali, ukiachia jeshi la polisi, ambao ni mfumo pekee uliokua ukitumika zamani.
MAUDHUI YA PROGRAMU
Wanafunzi wa usimamizi wa sheria wanafundishwa kozi mbalimbali ambazo zinawajenga kiuwezo na kiufahamu kuhusiana na mambo mbalimbali yanayohusu usimamizi wa sheria za kitaifa na zakimataifa.
Masomo Yanayofundishwa
Miongoni mwa masomo yanayofundishwa kwenye programi hii ni yale ya kisheria kabisa kama vile Sheria ya Utawala (Administrative Law), Sheria ya Katiba (Constitutional Law), Sheria ya Ushahidi (Evidence Law), Sheria ya Makosa ya Jinai na Mwenendo wa Makosa ya Jinai (Criminal Law and Procedure), Sheria zakimataifa (Public International Law), Sheria zakivita zakimataifa (International Humantarian Law), Sheria za wakimbizi (International Refugee Law) n.k
Masomo mengine ni yale yanayohusu uhalifu wa kisasa kama vile Uhalifu wa Mitandaoni (Cybercrimes), Uhalifu wa kifedha (Financial Crimes), Sheria dhidi ya utakatishaji wa fedha (Ant-Money Laundering) Sheria za Kuzuia Ugaidi (Anti-Terrorism Law), Sayansi ya Kutambua Uhalifu (Forensic Science), Makosa ya Kimataifa (Transnational Crimes)
Pamoja na masomo mengine kama vile Uongozi katika usimamizi wa sharia (Leadership In Law Enforcement), Elimu ya Takwimu (Statistics), Sheria za Haki za Binadamu (Human Rights Law), na Sheria za haki za watoto (Juvenile Justice Law).
SEHEMU ZA KAZI KWA WAHITIMU
Programu hii ni multidisciplinary kwa maana ya kwamba inagusa maeneo mengi yanayohusu sheria na usimamizi wa sharia. Hii inawajengea uwezo wahitimu kuweza kutumikia nafasi mbali mbali, katika mamlaka, mashirika na taasisi za serikali na zisizo zakiserikali, kitaifa na kimataifa.
Baadhi ya maeneo ni kama ifuatavyo.
1. Criminal Investigation Departments.
2. Immigration Department.
3. Private and Public Financial Institutions,
4. Audit Companies and Forensic Companies.
5. Financial institutions such as banks
6. Tanzania Intelligence Security Services (TISS) and Tanzania Military Intelligence (TMI)
7. Organizations relating to Legal Affairs,
8.Insurance Companies and Social Security Fund.
9. Regulatory Authorities such as TFDA, PCCB, PPRA, TBS, SUMATRA, TANROADS, TCRA, TRA etc.
10. Private Security Companies.
11. Embassies.
12. United Nations and the Specialized Agencies such as UNESCO, UNHCR, UN HABITAT, UNDP etc.
13. Tanzania Financial Intelligence Unit
MAKALA HII IMETOLEWA NA;
Mfaume Hassani Hamadi
Mwanafunzi wa mwaka wapili
Shahada ya usimamizi wa sheria
Chuo kikuu Dar es salaam (Mlimani campus)
mfaumehassan@gmail.com
0745-624-754
24/07/2018