Babu wa Loliondo sasa yuko hatarini...

mediaman Hatudanganyiki ng'oooooooooooooooooooooooooooo:crutch:
 
wivu tu!!!!!!!!!!! wameshindwa kuwaponya watu na miujiza yao feki wanaanza majungu...........
 
Baada ya kuzidiwa na Tanesco sasa Katotoize amehamishia majeshi kwa babu bango
 
Mediaman,

Mungu ni mmoja. Unataka amtaje Yesu ili iweje? Yeye amesema ameoteshwa na Mungu. Mungu alimuumba mwanadamu kwa mfano wake. Kutokana na kutenda dhambi Mungu alimtuma mwokozi Yesu ili aje kuwaepusha wanadamu na dhambi. Naam, vivyo hivyo Mungu alipoona binaadamu wanateswa na magonjwa na kwa kuwa Yesu alikufa na kufufuka na kupaa mbinguni na kuwa atakuja tena siku ya hukumu kuwahukumu wazima na wafu... akamtokea Ambilikile Mwasapile kule Samunge na kumpa maono ni jinsi gani anaweza kuwaponya wanadamu na magonjwa sugu yanayowasumbua.

Kwa hivyo basi, Yesu kazi yake kubwa ilikuwa ni kuwaokoa wanadamu dhidi ya dhambi. Ambilikile Mwasapile kazi yake ni kuwaponya wanadamu dhidi ya magonjwa yanayowasumbua. Kwanini basi usiamini kuwa kila mmoja ana kazi yake aliyotumwa na Mungu?

Ukuweza kwenda kwa Ambilikile Mwasapile ukapona maradhi yako na ukamfuata Yesu ukaacha dhambi zako utauona ufalme wa mbinguni siku Yesu atakapokuja kutoa hukumu.

Kumtibu mtu kwa kutumia jina la Yesu kwangu naona sio sahihi. Kwa kuwa Yesu kazi yake ni kukuondolea dhambi na magonjwa sio dhambi...

Elewa hivyo katika jina la Mungu.
 
Hivi ni kwanini haya makanisa ya kilokole yanamuandama sana babu? ok kama siyo ya kimungu kwahiyo afanyeje? watu bw waliozoea kuibia watu kutokana na ujinga na umasikini wao ni hatari sana,
 
[QUOTE=mediaman;1773242]Pole sana. Stefano alipowahubiri wale watu katika Matendo ya Mitume na kuwaambia ukweli, walimsagia meno wakamtupia mawe na kumuua. Bwana Yesu akusamehe maana hujui ulisemalo na akuwezeshe kuurithi uzima wa milele maana uzima wa sasa ni wa kitambo tu. Amina[/QUOTE]


Huna Yesu hata kidogo,unafaa kutupwa kwenye lile ziwa la moto
 
Ungeanza kwanza na manabii, mitume, na maaskofu wa uongo waliojijengea mahekalu ya kufanyia biashara kwa kisingizio cha kuhubiri injili na kuponya na kufufua wafu.

Ungeanza na wanaojitangaza kwenye TV kila siku eti fika kanisani kwetu uponywe, upate mali, upate amani n.k

Ungewakumbusha kuwa Yesu hakujitangaza kwenye TV wala redioni wala kuweka vibao mabarabarani. Ungewakumbusha kuwa Yesu hakuishi maisha ya starehe, na pale alipoamua kupanda mnyama aliamua kupanda punda, na sio farasi. Ungewaambia wauze ma VX na ma Prado yao wanaotembelea kutokana na 'sadaka' za waumini wanaoibiwa

Bwana Yesu alisema kuwa 'Asiye kinyume chetu, yupo upande wetu'.

Wewe ni mzima wa afya kwa sababu unakula vizuri, unalala vizuri, huna stress kutokana na pesa unazovuna kutokana na 'sadaka' kutoka kwa waumini wako maskini.

Wapo wengine wenu tunaofahamu kuwa kisima cha kubatiza mlichojenga mbele ya kanisa lenu kina ushetani mkubwa, na inasemekana wanaoingia kubatizwa 'kwa maji mengi' wanaona humo joka, tumeamua kukaa kimya kuwasitiri, leo mnaona Babu kawanyima riziki ya siku chache, mnaanza kupagawa.

Msiogope kuyumba kwa uchumi wenu kutokana na wateja wenu kwenda kwa 'Babu', mbona hata uchumi wa dunia huwa unayumba? Kazeni mikanda, ongezeni 'upako wa uongo' mahekaluni mwenu, uchumi utatengamaa, sio kuja kuwadanganya watu hapa. After all huko kwenye TV mnalipia matangazo, hapa JF mmelipia?
 
Mathayo 9, 1-8

...watu walimleta mtu aliyeparalyze aliyekuwa amelazwa kwenye kitanda, Yesu akamwambia, "...umesamehewa dhambi zako..." wakaanza kunong'onezana, iweje mtu huyu asamehe dhambi ? anafanya kufuru. Yesu alipowasoma fikra zao, akawauliza, ni kipi rahisi, kusema umesamehewa dhambi zako au kumwambia nyanyuka uende zako ? Then akamwambia yule kiwete, nyanyuka, chukua kitanda chako na uende nyumbani, kiwete akanyanyuka na kuenda zake, watu walipoona kiwete kanyanyuka, wakaogopa, na kumtukuza Mungu.

Pointi ni nini hapa, wakati kwa uwezo wa kibinaadamu tunachoweza kuona ni physical healing, na ndio ambacho tunaweza kusadiki, lakini unapoambiwa spiritual healing huwezi kuona hapo unachotakiwa ni kuamini, so kama hayo makanisa yenu mnasema mnatoa spiritual healing ambayo hatuwezi kuiona, kwanini hamtoi physical healing ili watru waweze kusadiki? Na je kwanini mnapoteza muda wenu mwingi kumsema babu ambaye pamoja na kuombea, anatoa physical healing ?

Yesu alisema, usipompenda jirani yako ambaye unamuona, utawezaje kusema unampenda Mungu ambaye humuoni ? Hapo Mediaman unaargue vitu ambavyo havionekani, ni vitu vya kusadikika tu.

Mediaman, kama unataka kusaidia watu, kwanini usiende Loliondo na kumuombea babu ? Km una imani ya kweli, maombi yako yatafanya hiyo unayoita ''tiba ya kishetani'' ya babu isifanye kazi na pia babu ''ataokoka'' na kutubu na kueleza ukweli. The time you are spending to argue on jamii forums is useless.
 
Serikali ni watu wa ajabu sana Babu aliwaomba msaada mapema na serikali kama serikali na Intellijensia yao walipasa kujua mahitaji ya kule mapema na kutoa taaarifa ni nini kifanyike muda ule leo hao TISS wanakuwa makada siku za uchaguzi kwenye mambo muhimu kama hayo wao hawahusiki kabisa

Ona sasa kumefumuka miugonjwa ya ajabu huko Loliondo watu wana harisha Damu. serikali ina uzembe mkubwa sana ila wakati wa kampeni huwaga wanatoa pesa nyingi sana kila mikoa kuhakikisha CCM inashinda sasa sielewi iweje tu hapo kwa Babu walishindwa ku provide huduma ya muda ya jamii kwa watanzania ??
 
Toa upuuzi wako hapa jamvini, inaonekana umezoea mambo ya kupiga ramli wewe. Shindwa na ulegee nenda kwenye utabiri kwa sheikh yahaya - nyani wewe.
 

kakobe ND MWINGIRA AT WORK
 
Nditu na Siyenda mko juu sana maana mmesema ukweli mtupu na Mungu aitwaye "JEHOVAH" awabariki sana. Kuna mgonjwa alipelekwa India kwa matibabu ya figo alipopimwa na kukutwa na ngoma akarudishwa Bongo. Last week kapelekwa na Babu jana kaendesha gari mwenyewe wakati alikuwa wa kubebwa. Acha Yesu aitwe Yesu. Amen
 


Mediaman anachofanya ni kuokoa dini yake ya kipentekoste dhidi ya kkkt na mengineyo. Umechemka. Mbona kina mwingira wanafanya mambo mengi lakini hulalamiki? Ushindwe na ulegee
 
Mbona mnamshambulia wakati yeye katoa hoja kimaandiko?? kwanini na nyie msitoe ya kwenu, mmekuwa wagumu kuelewa, mnataka mteremko kuwa mpone kisha mrudie dhambini/kuendelea na maisha yaleyale, watu hamtaki kumwabudu Mungu ila mpone afu mkae pembeni mkiwa kama watazamaji.
 
In every society, there is a natural rate of people who are persmistic & antagonistic in whatever happen!

Kutokana na uwepo wa hawa watu ambao wana doubtful & dead conciousness, Hata Yesu Mwenyewe walimpinga na kumuua msalabani japo ilikuwa kutimia kwa maandiko na kudhihirisha uwepo wa hili kundi!

Umenistaabisha ulivyohusisha wasomi wenye shahada za elimu ya juu na Wazungu ambao unawatukuza kwa ustarabu kufuata matibabu kwa Babu,
Yawezeka hujajua nini maana ya "Imani" kinachowapeleka kule si ustarabu na elimu bali ni Imani, Na wale ambao imani yao hafifu juu ya Babu na Mungu kama wewe hata wakaenda yawezekana wasipone! Kumbuka Yesu alikuwa akiwaambia Imani Yako imekuponya!

Kama babu alivyosema kaoteshwa na Mungu wenye Imani watamtukuza Mungu kwa uponyaji wake na si Shetan! Yesu aliulizwa, "Rabi kuna watu wanaponya kwa jina lako, Je hao nao ni wako au Washetan? Alijibu ikiwa wanaponya kwa jina langu ni wetu maana hakuna tawala mbili zinazopingana zikatawala pamoja! Pia Kuna mtu aliomba aonane na Mungu naye akahidiwa hvyo akafanya maandalizi usafi wa uhakika chaajabu alienda kichaa mwenye utindio wa ubongo yule mtu alimtimulia mbali! Nawasiwasi kwa vigezo vyako ngumu sana kupokea muujiza wa Mungu! Usitake kumpangia Mungu miujiza yake na wala haipimwi kwa vigezo vya kibinadamu!

Usimuhuku binadam mwezako ili nawe usije ukahukumiwa katika yeye! Ahukumuye ni mmoja tu Mwenye enzi na mamlaka yote naye ni Mungu!
 
huu bwana ni ka-tortoise au mwingi wa ngawira au mama rwakwa raaaaa taliiiiiiii katumwa huyu kuvuruga mambo humu naomba tumtie ban ss wenyewe hakuna kuchangia mada zake hana hoja za maana wala za maendeleo akaanzishe kanisa nchi nyingine labda atawapata waumini wajinga.
 
 
Tokea hadharani,tena kule Loliondo kama una hoja nzito kwanini kujificha huku JF tena nakushauri uende ukafanye mkutano kule watakusikiliza vilevile usisahau kumsomesha na Babu tutakuchangia na vipaza sauti hata nauli ukitaka,hatutaki utuletee tena huku,tunachotaka kusoma huku ni ushuhuda wa wale waliopona au wanaoendelea kuumwa hata baada ya kugonga Kikombe cha babu:embarassed2::embarassed2::embarassed2:
 
<p>
 


Sasa Babu si hataki jamani???? nenda ujaribu kumpa gari kama atakubali ...............amesema Mungu wake kamkataza!!!!!!!!!!! Mungu gani anayekukataza usifanikiwe????? Mungu wa Kweli anabariki na kuinua; anabadilisha maisha ....sasa anayemkataza Babu ni Mungu kweli au ni mungu yupi???? nauliza!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…