Habari za mchana wana jf wenzangu!!!!!!
Wengi tumeamini katika tiba anazozitoa BABU!!! Saratani, ukimwi, kisukari, shinikizo la damu.
Nimekaa hapa ofisini nimewaza hivi, kuna hili tatizo kubwa na sugu namaanisha tatizo la ndoa/mapenzi, mwanzoni watu wanakuwa na mapenzi moto, moto, kidogo, kidogo mkishazoeana penzi linaanza kuchuja na mwisho kuisha kabisa. Jamani tupelekeni maombi kwa babu aongee na Mwenyezi Mungu, kama alivyompa huu upako wa kutibu haya magonjwa mengine, apate basi upako wa kutibu na hili gonjwa sugu la ndoa/mapenzi.
Katika mazingira tunayoishi sasa hivi, kama sio mama yako mzazi kukusimulia kuhusu baba, basi dada, kama sio dada, kaka, shangazi, mjomba, wifi, jirani, bosi, secretary, yaani hakuna amani kabisa katika hiki kitu kinachoitwa mapenzi kwa sasa. Mimi nikifanikisha kwenda kwa babu na katika sala zangu kuanzia sasa hivi nitamwomba Mwenyezi Mungu amwonyeshe babu mzizi mwingine maalumu kwa ajili ya hili gonjwa na gonjwa hili akinywa mama na baba anakuwa ameponyweshwa na akinywa baba basi na mama atakuwa ameponyeshwa na hii iwe maalumu kwa wanandoa tu. Nadhani sijajichosha, wala kuwachosha.