Babu wa loliondo atuombee kwa mwenyezi mungu kuhusu ndoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Babu wa loliondo atuombee kwa mwenyezi mungu kuhusu ndoa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Safina, Mar 16, 2011.

 1. Safina

  Safina JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2011
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 498
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari za mchana wana jf wenzangu!!!!!!

  Wengi tumeamini katika tiba anazozitoa BABU!!! Saratani, ukimwi, kisukari, shinikizo la damu.

  Nimekaa hapa ofisini nimewaza hivi, kuna hili tatizo kubwa na sugu namaanisha tatizo la ndoa/mapenzi, mwanzoni watu wanakuwa na mapenzi moto, moto, kidogo, kidogo mkishazoeana penzi linaanza kuchuja na mwisho kuisha kabisa. Jamani tupelekeni maombi kwa babu aongee na Mwenyezi Mungu, kama alivyompa huu upako wa kutibu haya magonjwa mengine, apate basi upako wa kutibu na hili gonjwa sugu la ndoa/mapenzi.

  Katika mazingira tunayoishi sasa hivi, kama sio mama yako mzazi kukusimulia kuhusu baba, basi dada, kama sio dada, kaka, shangazi, mjomba, wifi, jirani, bosi, secretary, yaani hakuna amani kabisa katika hiki kitu kinachoitwa mapenzi kwa sasa. Mimi nikifanikisha kwenda kwa babu na katika sala zangu kuanzia sasa hivi nitamwomba Mwenyezi Mungu amwonyeshe babu mzizi mwingine maalumu kwa ajili ya hili gonjwa na gonjwa hili akinywa mama na baba anakuwa ameponyweshwa na akinywa baba basi na mama atakuwa ameponyeshwa na hii iwe maalumu kwa wanandoa tu. Nadhani sijajichosha, wala kuwachosha.
   
 2. Desidii

  Desidii JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 1,212
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hizi thread za Babu zinachosha kweli
   
 3. NILHAM RASHED

  NILHAM RASHED JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 1,629
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wallah maana hata na mimi najiuliza kila kukicha huyu babu loliondo ndio naani???
   
 4. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,138
  Trophy Points: 280
  Sasa hivi babau atakuwa Mungu au Mtume au Nabii, of course wa uongo.
   
 5. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,522
  Likes Received: 1,005
  Trophy Points: 280
  Babu sio Nabii ni mtu tu kama sisi, tusifilisike kiimani kiasi hiki ni bora matumaini yetu tukiyaweka kwa Mungu Mwenyezi. Babu ana mwisho siku yake ikifika naye atakufa tu! Hana ujanja wa kupambana na mauti lakini Mungu wetu hafi, haumwi yupo MILELE na MILELE.
   
 6. Safina

  Safina JF-Expert Member

  #6
  Mar 16, 2011
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 498
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Matumaini yetu tumeyaweka kwa Mungu na ndo maana nimesema atuombee tupewe kikombe kingine, sikusema yeye ni nabii wala yeye ni Mungu.
   
 7. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #7
  Mar 16, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mhh!! Safina unapenda kuombewaaaaaa???? si ujiombee mwenyewe????
   
 8. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #8
  Mar 16, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Kama ndoa yakushnda jitoe au kama hujaingia na wahs itakucost usitie mguu
   
 9. S

  Societa Jesuit JF-Expert Member

  #9
  Mar 17, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hilo kweli ila nawe kwanini ukae ofisini ukiwaza juu ya babu tu wakati huo muda ni wa mwajiri wako okey hata wewe unaweza kuomba ili Mungu akuonyeshe ingawa babu yeye hakuomba apewe hiyo dawa.

  Tusimjaribu Mungu ......labda kwa sadaka na zaka tu.
   
 10. S

  Societa Jesuit JF-Expert Member

  #10
  Mar 17, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  kwani wewe huwezi kuomba......au huyu Mungu wa babu tu.
   
 11. S

  Societa Jesuit JF-Expert Member

  #11
  Mar 17, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  where are u da beautiful one ?... on earth or in earth...okey he is a pastor wewe kanywe tu kama unataka natural hina.
   
 12. S

  Societa Jesuit JF-Expert Member

  #12
  Mar 17, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  kanuni ya kuchoka ni kupumzika na uchovu ukitoweka karibu tena nadhani ushauri with no payment
   
 13. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #13
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Mi nafikiri kila mtu na matatizo yake kikombe kimoja tu kinaponya kuna mdada mmoja kaenda kunywa apate mume kashuhudia, kanywa mwaka jana sasa hivi ana mchumba keshatoa mahari. mimi nikipata tu nafasi na mungu akipenda lazima niende loliondo sitaki kupitwa maana hawakawii kumpoteza watu wa madawa ya kizungu
   
 14. CPU

  CPU JF Gold Member

  #14
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mwisho tutaomba Babu aonyeshwe mizizi ya utajiri na kufaulu bila kusoma
   
Loading...