Babu wa Loliondo ametoa onyo.

Giddy Mangi

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
830
184
Juzi tarehe 18th April 2011 majira ya saa moja na robo asubuhi babu Mchungaji Ambilikile Mwasapila amewatahadhari wale wote wanaombeza na kumchukia wakiwemo Mchungaji Kakobe na Madaktari nchini na kuwataka waende Samunge kunywa dawa kwani yeye anafanya kazi ambayo Mungu amemwelekeza kufanya."wananichukia sana mimi babu lakini wanakosea kwani Mungu ndio wanayemchukia mimi ni mtumishi tuu.Mimi sitoi miti shamba bali Mungu ameniagiza nichemshe dawa ambayo ni mbadala wa neno lake niwapatie watu wapone maradhi yao.
 
Mapato!! mapato baba revenue imeshuka kwao hao watu coz watu wengi wanakimbilia samunge sasa hakuna cha kanisani wala kwa doctor, sasa wasimchukie kwa nini?
 
Mhhh Mungu atusaidie, kupima kila roho zijazo kwa jina lake.
 
kaka nitafute nikupeleke ukapate Kikombe kwani wewe ni kichaa hakika Mungu wa mbinguni amekusamehe kwani wewe umemkosea tena sana kwa kumwita Kichaa.

wewe ndio zuzu na zumbukuku wa mwisho kabisa!u-mnafiki mno!nani aliyekuambia babu katumwa na mungu?
Nasikia kichefuchefu kuona mtu mwenye uwezo wa kublog anashindwa vipi kung'amua kwamba babu ni msanii.binafsi ninafuatilia kwa karibu wagonjwa kutoka samunge,its nothing and people are dying.ukiniambia babu ni israili mtoa roho ntakubali.
Acheni kusuport usanii na upuuzi!hata desi mlibisha hivi hivi!
 
........Huu uchafu wa nini hapa JF? Jamani kama hamna ya kupost tusome na tuchangie vya wenzetu................
 
Huyu 'Babu' nae hana sera. Anatengeneza mazingira ya watu kwenda kuchafua mazingira tuu kule loliondo kwa kutupa taka hovyo na kuchangia mbolea asilia kwa vinyesi. Upuuzi mtupu na hakuna mtu anaepona. Kama kweli anania yakusaidia kwa dawa yake ambayo muarobaini afadhali atengeneze sumu ya kuua wadudu wa mazao. Hizi imani za kipuuzi ndio zinatufanya hatuendelei. Aibu watu wazima, viongozi nao wanaimani za-bronze age goat herding societies.
 
Bab wa loliondo hana tofauti na wachawi wengine .suala la kikombe ni kuwapumbaza watu wajadili uchawi badala ya kujadali mambo ya maana. Hapo mwanzo shehe yahaya alikuwa anatumiwa kutabili ndoyo na sasa wanamutumia babu . Babu akisema inatuhusu nini ???



Babu ni nani mpaka anaposema watu wanashangaa , huu ni ujinga mkubwa kwa watu wanao amini mambo ya kishirikina na uchawi!!!!


Kumushabikia babu ni sawa na kumshabikia shehe yahaya na wachawi wengine
 
Back in the days nakumbuka kusoma kitabu cha James Hadley Chase kinaitwa "Believe This, You'll Believe Anything" .
 
Mapato!! mapato baba revenue imeshuka kwao hao watu coz watu wengi wanakimbilia samunge sasa hakuna cha kanisani wala kwa doctor, sasa wasimchukie kwa nini?

Yaani kama ulikuwapo! Umegonga msumari mlangoni, BANGO LIMEWEKWA WAZI! Sasa hakuna kukimbilia, sio kwa Kakobe wala kwa Mwingira wala kwa Rwakatare! Walizoea kukomba mafweza ya wajinga (waliwao), sasa wajinga wamejanjaruka, Babu kawaletea kikombe, kwanini wasimchukie?

Fid Q ameimba watu wanatumia dini kujipatia kipato... ndio hawa, Mapacha Watatu (Kakobe, Mwingira na Rwakatare), ambao wamezoea sana kula VYA BURE! Sasa walie tu! Kwani wanaweza kucheza na Mungu? Hili game KALI! Mungu keshawashinda! Wao wanajidai wanamtukuza Mungu! Utamtukuzaje Mungu kwa kutumia USHIRIKINA? Khaaaa! Nani asiyejua Kakobe, Mwingira na Rwakatare ni WASHIRIKINA? Makafara yao wanayoyafanya usiku wa manane, wakiwa na waganga wao wa Nigeria, NANI ASIYEJUA? Walidhani itakuwa siri daima? IMEKULA KWAO!
 
Nakubaliana kabisa. Na hata hao wanaomuunga mkono huyo babu akili zao zinabidi kuchunguzwa!

afande unachunguza?umeshaonja cha arusha nini? Mambo ya imani magumu!achia wenye uwezo waendelee nayo ila km utaki si utulie.
 
Kweli viumbe wa MUNGU wanaangamia kwa kukosa maarifa,huyo babu kamfanya MUNGU mjomba wake wa kuonana naye anapotaka yeye,leo kaoteshwa dawa kesho ataoteshwa awacharaze viboko wote! kwa akili za kawaida mnafikiri dawa ni shs.500/= lakini hamjui mmepoteza kiasi gani kuipata hiyo dawa. Watu wameuza vitu vya thamani kwaajili ya kupata dawa ya shs.500/= (Nauli+Chakula+malazi x siku ) kuna watu wamepoteza mamilioni lakini hali zao bado ni mbaya wamerudi kwenye dozi zao za zamani.kisa eti imani hiyo imani ipo Samunge pekeyake? wapendwa mtaamka lini? mbona huyu mtu kawafunika vibaya?
 
Babu ni mganga wa kienyeji kama waganga wengine tu. Inanisikitisha sana kuona bado kuna watu wanashabikia udanganyifu huu mkubwa. Kisayansi, dawa haijathibitishwa na watu wanaendelea kufa. Kiimani anadai eti kaoteshwa na Mungu, uongo mkubwa. Mungu hawezi akafanya jambo kinyume na Biblia. Katika agano jipya Mungu haponyi kwa kutumia miti. Anatumia Neno lake tu. Na Mungu haweki neno kwenye miti, anaweka neno mioyoni mwa watu (Soma Rumi 10:17), hii ndio imani.
Inasikitisha watanzania tumekuwa wepesi mno wa kudanganyika kirahisi namna hiyo bila kufanya utafiti wowote wa kisayansi au kiimani
 
Back
Top Bottom