Wale jamaa wa wizara waliotumwa lazima watakuwa walibeba dondoo zao za kiukiritimba zaidi. Kwanza wangemchunguza kama amejiunga na CHAWATIATA ambacho kinakubalika pale wizarani, kama anacho kibali cha serikali kuendesha shughuli zake, kama madawa anayotumia yamepitia TBS, kama Kituo cha tiba asilia Muhimbili wameruhusu aendelee, kama bodi ya madawa ya taifa imeridhia mazingira ya tiba kutumika, kama mabwana afya wameruhusu, kama analipa kodi kwa serikali, kama anatoa risiti kwa pesa anayopokea, kama kuna ukaguzi wa mahesabu na ripoti wangetaka kuiona, .....
Kadhalika, katika hao waliokwenda kule, najua ni lazima wakuu wa vitengo vinavyoshughulikia tiba mbadala wangekuwamo, ambao kusema kweli wapo kikazi zaidi kwa maana ya policies za wizara kwenye makaratasi lakini hawana msaada wowote kuendeleza tiba mbadala, maana shughuli zao zaidi ni kuzunguka mikoani na kupata perdiem na hawana lolote wanaloweza kujivunia tangu kitengo kianze enzi za Prof wa Mifupa wa Rorya ambaye ndiye pioneer wa kitengo hicho. Hawasikii ushauri na wana viburi ajabu. AAmefanya vizuri Ambilikile kuwatolea nje jamaa hao, maana waganga wengi sasa hivi wanawakwepa watu hao kwa ulaliaji.
Watu kibao wametamka bayana kwamba walikuwa wanaumwa na sasa wamepona kwa dawa hiyo, sasa wanachunguza mganga au dawa? Kwa nini wasifanye utafiti mwepesi kabisa kwa kupeleka dondoo kwa wanaohudhuria wanaumwa nini na tangu lini na sasa wanayo maoni gani juu ya magonjwa yao baada ya kutibiwa? Huhitaji kuingia darasani kutafuta ukweli huo. Kama mzee wa watu angekuwa anatengeneza vidonge wangetafiti kwenye maabara kisayansi ya sasa. Lakini dawa ya mzee huyo inapoteza nguvu ukienda mbali naye, tena huwezi hata kumchukulia nduguyo nyumbani ila anaitoa yeye mwenyewe kwa mkono wa kushoto na maombi kwa Mungu. Waende kwa Askofu Laizer wa Arusha akawaambie uzoefu wake yeye mwenyewe na tiba hiyo kama hawaamini nkwamba watu wa kawaida watakuwa wakweli. Na yule Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro tuliyemwona kwenye picha akichukua dawa kwa nini hawamwamini? Wanatengeneza mazingira ya ulaji hawa, hawana lolote.