Babu wa Loliondo,ACACIA na media zetu

Toka jana baada ya Magufuli kukutana na CEO wa Barick vyombo karibu vyote vya habari vimejaa 'habari za pongezi' kwa Rais kwa 'kuweza kufanikisha kulipwa' tulichokuwa tunaidai hiyo kampuni.

Taarifa za habari za TV karibu zote na magazeti habari ni hizo hizo.

Licha ya ukweli kuwa jana hiyo hiyo Barrick na ACACIA wote wametoa taarifa za kukataa kulipa chochote sisi vyombo vyetu ni kama hiyo taarifa 'haituhusu' kabisa tuko bize na pongezi.

Inanikumbusha wakati wa Babu wa Loliondo jinsi ambavyo media zoote zilivyokuwa zinaripoti 'miujiza' ya babu huyo huku zikiwa hazitaki kabisa kuripoti taarifa za wagonjwa waliokuwa wanakufa baada ya kutoka huko Loliondo.

Hata taarifa za wataalam wa nje waliofika na kusema 'hakuna tiba' huko Loliondo wagonjwa wasiache dozi za hospitali zilipuuzwa.

Tulikuwa nchi nzima tuko excited na babu wa Loliondo na kikombe chake.

Yeyote aliongea vingine alionekana 'msaliti' na sio 'mzalendo'

Wapo waliotaka Babu wa Loliondo apewe tuzo maalum na kadhalika na kadhalika.

Vyombo vyetu vya habari ndo viligeuza habari ya 'kuuza' na kuwajaza watu ujinga uliopelekea hata watu wengine kupoteza maisha la kusikitisha hii tabia haijawahi kukemewa.

Sasa tuko na kupongezana na kuambiana uwongo mtupu licha ya wahusika kutoa ukweli wao kuwa hakuna walichokubaliana kulipa sisi ndo kwanza na wengine wanataka tuzo kwa tume na Rais aongezewe muda kwa 'haya mafanikio ambayo siyo ya kawaida'.

Sisi hatujifunzi kitu kwa kweli.

The Boss hili ni tatizo la muda mrefu la vyombo vya habari na waandishi wa habari wa Kitanzania kwa ujumla.

Utamaduni uliojengeka nchini tangu enzi za "chama kushika hatamu" na "zidumu fikra za mwenyekiti" ni kwa vyombo vya habari siku zote kutukuza watawala kwa kuwaimbia mapambio ya sifa.

Ikumbukwe kuwa hadi mwishoni kabisa mwa miaka ya 80 vyombo tu vya habari vilivyokuwepo nchini vilikuwa ni vile vya "chama" na serikali. Utaratibu uliokuwepo wakati huo ilikuwa ni kuwapatia mafunzo waandishi wote wa habari waanndamizi katika chuo cha "chama" Kigamboni namna ya "kuchagua na kuripoti" habari kwa maslahi ya "chama" na serikali.

Itakumbukwa kwamba magazeti ya kwanza huru na binafsi kuanza kuchapishwa nchini kama Fahari la Jim Ndoe, Radi la Ndimara Tegabwange na Michapo yaliingia matatani na hayakudumu. Gazeti la kila wiki la Kiingereza la Family Mirror (ambalo mhariri wake alikuwa Anthony Ngaiza na baadaye Hillal Sued) lilikuwa linaichahafya sana serikali lakini halikuonekana ni tishio kubwa kutokana na lugha yake. Hii ilikuwa ni wakati wa utawala wa awamu ya pili.

Watawala pia wanatumia mbinu chafu ya "stick and carrot" kwa waandishi wa habari kwa kiasi kikubwa. Wanahabari wanaoonekana "wanafanya kazi yao vizuri" kwa kujikomba kwa watawala kwa njia ya kuwapa sifa za kinafiki wasizostahili (flattery) wamekuwa wanazawadiwa teuzi za kisiasa kama u-DC. Kwa upande mwingine wale wanahabari wachache wanaothubutu kufanya kazi yao kwa weledi, uhuru na kujiamini wanaishia kukamatwa na kushtakiwa kwa uchochezi na magazeti yao kufungiwa kama ilivyotokea leo kwa Mawio.
 
You re one of the great thinker
 
Mleta mada roho inamuuma kweli kuona Magu yuko front fegi ya kila gazeti, tv na redio!
 
Weka hapa tamko la Barrick
 
....
.....Ujinga ni Maradhi Mkuu

Mkuu,

Tatizo kubwa siyo ujinga, ni upumbavu, na katika huo wapo wasiosoma, wenye elimu, wakulima, wafanyakazi na viongozi.
Usishangae kumuona doctor, engineer, lawyer, teacher na hata professor mpumbavu.
Elimu haiondoi upumbavu bali hufuta ujinga
 
Wasipojikomba kwa bwana mkubwa watafungiwa kama mawio
 
Hapo kwenye red, Mkuu umenikumbusha mbali sana, Nakumbuka kipindi kile wakati hili vugu vugu la KIKOMBE limepamba moto, kuna jamaa alishushwa kwenye dala dala baada ya kupingana na abiria wengine kuhusu Mzee wa KIKOMBE, yeye huyu jamaa alikuwa ni akili kubwa wa enzi hizo, akawa anasema wazi kuwa Kikombe cha BABU ni magirini.

Ndivyo ilivyo sawa na hili suala la ACACIA, Profesa Mzungu kasema wako tayari kwa mazungumzo, ambayo yataamua nini kifanyike,

  1. Lakini tayari UVCCM wameshaandaa maandamano ya kumpongeza Rais kwa kufanikisha malipo ya Trilioni 108.
  2. Wabunge wa CCM na wawili wa CUF wameshapitisha Azimio la kumuunga Mkono Rais.
  3. Mashirika ya UMMA yameshaanza kutoa waraka wa kumpongeza Rais kwa kufanikisha malipo ya Trilioni 108.
  4. Makampuni Binafsi kupitia kwa wakurugenzi wao wameshatoa matamko ya kumpongeza Magufuli kwa kufanikisha kurudishwa kwa matrilioni.
  5. Vyama Rafiki wa CCM kupitia wenyeviti wao akina MREMA, CHEYO na DOVUTWA nao hawakubaki mbali.
  6. Vyombo vya habari ndio vimegeuka wapotoshaji wakuu katika hili suala.
Wakati mnafikiria hivyo, nawashauri msome na maneno haya aliyoyasema Rais Putin wakati wa kipindi cha maswali na majibu huko nchini mwake, June,2017.
===
“I am prepared to talk to anyone whose goal is to improve people’s lives, to solve the problems that the country is facing, as opposed to use the problems, which always exists anywhere, to score political points, to profit from such problems while making them worse,” Putin said. “Peoplesuggesting solutions deserve utmost attention and deserve a dialogue with the government.”
 
The Boss hili ni tatizo la muda mrefu la vyombo vya habari na waandishi wa habari wa Kitanzania kwa ujumla.

Utamaduni uliojengeka nchini tangu enzi za "chama kushika hatamu" na "zidumu fikra za mwenyekiti" ni kwa vyombo vya habari siku zote kutukuza watawala kwa kuwaimbia mapambio ya sifa.

Ikumbukwe kuwa hadi mwishoni kabisa mwa miaka ya 80 vyombo tu vya habari vilivyokuwepo nchini vilikuwa ni vile vya "chama" na serikali. Utaratibu uliokuwepo wakati huo ilikuwa ni kuwapatia mafunzo waandishi wote wa habari waanndamizi katika chuo cha "chama" Kigamboni namna ya "kuchagua na kuripoti" habari kwa maslahi ya "chama" na serikali.

Itakumbukwa kwamba magazeti ya kwanza huru na binafsi kuanza kuchapishwa nchini kama Fahari la Jim Ndoe, Radi la Ndimara Tegabwange na Michapo yaliingia matatani na hayakudumu. Gazeti la kila wiki la Kiingereza la Family Mirror (ambalo mhariri wake alikuwa Anthony Ngaiza na baadaye Hillal Sued) lilikuwa linaichahafya sana serikali lakini halikuonekana ni tishio kubwa kutokana na lugha yake. Hii ilikuwa ni wakati wa utawala wa awamu ya pili.

Watawala pia wanatumia mbinu chafu ya "stick and carrot" kwa waandishi wa habari kwa kiasi kikubwa. Wanahabari wanaoonekana "wanafanya kazi yao vizuri" kwa kujikomba kwa watawala kwa njia ya kuwapa sifa za kinafiki wasizostahili (flattery) wamekuwa wanazawadiwa teuzi za kisiasa kama u-DC. Kwa upande mwingine wale wanahabari wachache wanaothubutu kufanya kazi yao kwa weledi, uhuru na kujiamini wanaishia kukamatwa na kushtakiwa kwa uchochezi na magazeti yao kufungiwa kama ilivyotokea leo kwa Mawio.

Wote wakisimama wahesabiwe hawawezi kufungiwa wote
 
The Boss uko sahihi. Wanahabari wakiwa na umoja ni kundi lenye nguvu sana. Kuna ule usemi unaosema, "Kalamu ni kali kuliko sime (The pen is mightier than the sword)".

Katika jamii wanahabari ni mabosi in their own right. Kama Steve Biko alivyosema: "The most potent weapon of the oppressor is the mind of the oppressed", kosa kubwa wanalofanya wananhabari wa Tanzania ni kujishusha kwa wanasiasa kwa kuwasifu isivyostahili na kuwatukuza. Na wanasiasa wanatumia hiyo fursa kuwadhibiti waandishi wa habari kwa maslahi yao.

Wanahabari amkeni!
 
i wish wakusikie
 
Back
Top Bottom