Babu wa Loliondo,ACACIA na media zetu

Mwakyembe hana haya
Nipashe kawaogopa

View attachment 524606
Nipashe linamilikiwa na Tycoon Mengi, kwa kumbukumbu zangu Mengi hajawahi kushindwa vita na wote waliomjaribu waliangamia, ni swala la muda tu ndio huwa kwenye timing zake.

Ukitaka kumjuwa vizuri Mengi waulize Wahindi, muulize Masha, muulize Malima au muulize yule Profesa mjivuni aliyesoma kuliko mtanzania yeyote aliyemuita Mengi ni dalali tu na biashara anayowezakufanya ni ya maji na juice tu, na je leo yuko wapi?

Mengi ni taasisi kama Gwajima alivyo taasisi, ukitaka kuwekeana msuli na watu hawa ujuwe wazi unadeal na invisible defectors.
 
Mkuu The Boss kaa tayari kuitwa mtetea majizi pia kuambiwa sio mzalendo. Unajua vyombo vya habari imebidi viwe na unafiki tu kwa kuhofia fedhea kama anayoipata yule mbunge wa upinzani
tapatalk_1497522863749.jpeg

Hawa ndio wazalendo na mashujaa wa Taifa hili, ambaye walimkabidhi chenge wino wa kutuandikia katiba mpya. Sisi hata shetani anatuogopa.
 
Kama hawako huru vya kutosha baso bora wasikubali
kushirikishwa maigizo huku wanajua kabisa haya ni maigizo

Kuliko wao kushiriki kwenye hii 'praise and worship' mode...
Nadhani wanaangalia biashara pia. Ni vigumu sana kuonekana mzalendo kipindi hiki kama hauimbi wimbo wa rais kwenye madini-hakuna mtu atakuelewa.

Video clip ya jana ilikuwa wazi kabisa kwamba rais anaongea yake na mwenyekiti wa barrick anaongea yake. Mtu yeyote makin hakuhitaji Barrick waseme hawajakubali kulipa fidia maana mwenyekiti kazungumzia majadiliano na rais kazungumzia fidia. Ila kwakuwa rais alikuwa amefurahi sana 'kulipwa fidia' ilikuwa lazima media iende na uelekeo wa upepo. La sivyo wangekutana na hasira ya mkuu. Kama jambo dogo lile la kwenda bandarin kukamata mchanga aliwaambia waandishi 'hawako huru kiasi hicho' baada ya kutomuandika, itakuwaje kwa jambo kubwa kama la jana ambako 'tutalipwa fidia ya matrilioni'?

Kutomsifia rais kwa jambo ambalo yeye anaona ni kubwa ni sawa na kumponda rais. Ukitishiwa (you are free, but not to that extent) na rais lazima utii, maana ana njia milioni moja za kukushughulikia-na mahakama ndio njia ya milioni moja. Kuna zingine nyingi ambazo sio za kimahakama:p:p.
 
Inasikitisha taifa la watu zaidi ya milioni 50 baada ya miaka zaidi ya 50 ya uhuru
tupo hapa ukweli unaogopwa kupita kiasi
 
Naked na yuko juu ya meza...na wote tunaambiana 'kapendeza'
Nilikuwa bungeni wakati wa break AG alimuita Msigwa kumuonya watumie lugha ya heshima kwa Rais, niliogopa sana, JK ametukosea sana lakini jamaa ni Gentleman, huwezi kuminya uhuru wa watu kuongea mpaka wabunge wanajazwa hofu, vipi mimi na wewe raia wa kawaida

Yani tulipofikia Mtanzania ambaye yupo huru ni Mange tu, Tundu Lisu ni gwiji wa sheria lakini simu yake inadugukuliwa na mungu wetu anatamba kabisa kudukuwa simu ya Lisu ambacho ni kitendo kinyume na sheria.

Siku hizi imefikia hatuwa ni lazima ufuatilie kila siku kuna amri ipi mpya kutoka kwa mungu wetu ili usije kujisahau ukaingia matatani.
 
Utasema tuko North Korea
 
Toka jana baada ya Magufuli kukutana na CEO wa Barick vyombo karibu vyote vya habari vimejaa 'habari za pongezi' kwa Rais kwa 'kuweza kufanikisha kulipwa' tulichokuwa tunaidai hiyo kampuni.

Taarifa za habari za TV karibu zote na magazeti habari ni hizo hizo.

Licha ya ukweli kuwa jana hiyo hiyo Barrick na ACACIA wote wametoa taarifa za kukataa kulipa chochote sisi vyombo vyetu ni kama hiyo taarifa 'haituhusu' kabisa tuko bize na pongezi.

Inanikumbusha wakati wa Babu wa Loliondo jinsi ambavyo media zoote zilivyokuwa zinaripoti 'miujiza' ya babu huyo huku zikiwa hazitaki kabisa kuripoti taarifa za wagonjwa waliokuwa wanakufa baada ya kutoka huko Loliondo.

Hata taarifa za wataalam wa nje waliofika na kusema 'hakuna tiba' huko Loliondo wagonjwa wasiache dozi za hospitali zilipuuzwa.

Tulikuwa nchi nzima tuko excited na babu wa Loliondo na kikombe chake.

Yeyote aliongea vingine alionekana 'msaliti' na sio 'mzalendo'

Wapo waliotaka Babu wa Loliondo apewe tuzo maalum na kadhalika na kadhalika.

Vyombo vyetu vya habari ndo viligeuza habari ya 'kuuza' na kuwajaza watu ujinga uliopelekea hata watu wengine kupoteza maisha la kusikitisha hii tabia haijawahi kukemewa.

Sasa tuko na kupongezana na kuambiana uwongo mtupu licha ya wahusika kutoa ukweli wao kuwa hakuna walichokubaliana kulipa sisi ndo kwanza na wengine wanataka tuzo kwa tume na Rais aongezewe muda kwa 'haya mafanikio ambayo siyo ya kawaida'.

Sisi hatujifunzi kitu kwa kweli.
Hapo kwenye red, Mkuu umenikumbusha mbali sana, Nakumbuka kipindi kile wakati hili vugu vugu la KIKOMBE limepamba moto, kuna jamaa alishushwa kwenye dala dala baada ya kupingana na abiria wengine kuhusu Mzee wa KIKOMBE, yeye huyu jamaa alikuwa ni akili kubwa wa enzi hizo, akawa anasema wazi kuwa Kikombe cha BABU ni magirini.

Ndivyo ilivyo sawa na hili suala la ACACIA, Profesa Mzungu kasema wako tayari kwa mazungumzo, ambayo yataamua nini kifanyike,

  1. Lakini tayari UVCCM wameshaandaa maandamano ya kumpongeza Rais kwa kufanikisha malipo ya Trilioni 108.
  2. Wabunge wa CCM na wawili wa CUF wameshapitisha Azimio la kumuunga Mkono Rais.
  3. Mashirika ya UMMA yameshaanza kutoa waraka wa kumpongeza Rais kwa kufanikisha malipo ya Trilioni 108.
  4. Makampuni Binafsi kupitia kwa wakurugenzi wao wameshatoa matamko ya kumpongeza Magufuli kwa kufanikisha kurudishwa kwa matrilioni.
  5. Vyama Rafiki wa CCM kupitia wenyeviti wao akina MREMA, CHEYO na DOVUTWA nao hawakubaki mbali.
  6. Vyombo vya habari ndio vimegeuka wapotoshaji wakuu katika hili suala.
 
Kwani aliyesema wamekubali kulipa si mheshimiwa mwenyewe!! Ina maana nimesikia vibaya au ameamua kusema uongo wa wazi kabisa?
 
Media zisilaumiwe kilawakati maana taarifa nyingine wanafanya kipewatu ili waufikishie umma
 
Tatizo hii nchi hatupo huru ijapokuwa Ni nchi huru, inahitajika elimu kubwa kuanzia kwa Wananchi na waandishi.
Waandishi WA siku hizi Sio sawa na wale WA zamani,
Waandishi WA siku hizi wapo kimaslahi zaidi na sio kufikisha ujumbe uliokisudiwa kwa jamii.
 
Kwani aliyesema wamekubali kulipa si mheshimiwa mwenyewe!! Ina maana nimesikia vibaya au ameamua kusema uongo wa wazi kabisa?
Hata kama Mheshimiwa alisema hivo Ni haki ya mwandishi kubalance story yake upande WA pili, .
Sio unasikia upande mmoja basi unaenda kutuma story. Matokeo yake ndo hayo kumbe ndivyo sivyo.
 
Back
Top Bottom