'Babu’ wa Ifakara arukwa akili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Babu’ wa Ifakara arukwa akili

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mahesabu, Jun 10, 2011.

 1. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #1
  Jun 10, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Na Igamba Libonge, Kilombero

  MKAZI wa kijiji cha Muhola, kata ya Ifakara, Idd Juma (34), aliyekuwa akitoa tiba ya asili kwa kutumia kikombe amerukwa akili. Juma aliyekuwa akitoa tiba ya magonjwa sugu kwa takriban wiki mbili, amerukwa akili na amelazwa katika Hospitali Teule ya Mtakatifu Francis, mjini Ifakara. Mei 28, mwaka huu, Juma alijitangaza kutoa tiba ya magonjwa sugu kwa njia ya kikombe. Pia alikuwa akiwatibu wagonjwa wa akili na wenye pepo. Akizungumza katika kituo cha polisi cha wilaya ya Kilombero, Rashid Kilala, ambaye ni mdogo wa Juma, alisema kaka yake alianza kuugua Juni 6, mwaka huu, ambapo alikuwa kizungumza mambo yasiyoeleweka. Kilala alisema kabla ya kuanza kutoa tiba, Juma alikuwa akijishughulisha na biashara ya kuku wa kienyeji katika Soko
  Kuu la Ifakara, kazi aliyokuwa akiifanya tangu mwaka 2008. Kwa mujibu wa Kilala, kaka yake aliwaeleza ameoteshwa na malaika kuwa atakuwa na kipaji cha kutibu magonjwa sugu na Mei 28, ndipo alipopewa baraka na dawa. Alisema kabla ya kupata matatizo, Juma alitoa tiba kwa watu takriban 1,500, ambao baadhi aliwapa dawa bure na wengine aliwatoza fedha. Kilala alisema jana alfajiri alipigiwa simu na majirani wa Juma, waliomweleza amerukwa akili na anakimbia ovyo mitaani akisema anakwenda benki kuchukua fedha, wakati hana akaunti katika benki yoyote. Alisema alimfuatilia na kumwona akiwa mitaani, hivyo alitoa taarifa polisi ili apatiwe msaada, ambapo alipelekwa kituo cha polisi wilaya ya Ifakara. Juma akiwa kituoni alisema waganga wenzake wamemdhuru kwa kumtupia jini kutokana na kuona anapata fedha.
   
 2. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #2
  Jun 10, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Baba Ambilikile alionya watu wasiige.
   
 3. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #3
  Jun 10, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Kalogwa na waliomuotesha hicho kikombe....labda kakiuka masharti yao......
   
Loading...