Babu kupata 20% , kanisa kupata 40% ni sawa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Babu kupata 20% , kanisa kupata 40% ni sawa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Joss, Mar 31, 2011.

 1. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kutangazwa kwa mapato yaliyotokana na dawa ya Mch Mwasapile kunaonesha kuwa mgawanyo wake ni kama ifuatavyo :

  Kanisa ni sh 200 kati ya 500 = 40%
  Mch Mwasapile (Babu) 100 kati ya 500 = 20%

  Wasaidizi wanaomsaidia kuchimba dawa na mambo mengine yanachukua 40% iliyobaki.

  Swali ninalojiuliza, ni kwa nini kanisa lichukue kiasi kikubwa kuliko babu, ikizingatiwa kuwa kabla ya kuanza kutoa tiba babu alikuwa amestaafu, inamaana kuwa taratibu za kustaaafu zilifuatwa. Alipoanza kutoa tiba akaondolewa ustaafu wake na kurudishwa kazini. Hapo si inaonesha kuwa kanisa lililenga fedha itakayopatikana na si huduma ya kichungaji ya Babu?

  Source: IPP Media.
   
 2. Chona

  Chona JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 514
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Kama ulimsikiliza Babu vizuri alilitolea ufafanuzi kwamba katika Tsh 500, yeye atachukua Tsh 100, Wasaidizi wake Tsh 200 na Kanisa Tsh 200 na si kwamba Kanisa limemshinikiza bali ameamua iwe hivyo yeye binafsi na kama mchango wake. Hivyo Kanisa alikuhusika kupanga mchanganuo huo na hata hivyo alikuwa na jinsi ya kuingilia zaidi ya kupata 1/10 ambayo ingekuwa Tsh 50 kama Babu angufuata principles za dini.
   
 3. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Thanx for clarification !!!!
   
Loading...