Babu kachoshwa kapiga Neutral comment | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Babu kachoshwa kapiga Neutral comment

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Inkoskaz, Nov 20, 2011.

 1. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #1
  Nov 20, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Kingunge ashindwa kumshukuru Kikwete

  KADA Mkongwe wa CCM, Kingunge Ngombale Mwiru alishindwa kuzungumza "neno la shukurani" baada ya Rais Jakaya Kikwete kulihutubia taifa kupitia mkutano wa Wazee Mkoa wa Dar es Salaam.

  Mzee Kingunge ambaye alikaa upande wa kushoto wa Rais Jakaya Kikwete wakati akihutubia Taifa juzi, alionekana kutokuwa tayari kusema neno hilo la shukrani licha ya Kaimu Mwenyekiti wa Wazee Mkoa wa Dar es Salaam, Brigedia Jenerali Hashim Mbita, kumsihi afanye hivyo.

  Mbita aliyekuwa upande wa kulia wa Rais Kikwete, alisikika mara kadhaa kwenye kipaza sauti akimkaribisha Mwasisi huyo wa Chama, bila ya mafanikio .

  Hata hivyo haikufahamika sababu za Kingunge kushindwa kutii ombi hilo ingawa alionyesha ishara ya kutokuwa tayari kufanya hivyo licha ya Mbita kuendelea kumsihi bila mafanikio.

  Tukio hilo lilitokea wakati Brigedia Mbita alipokuwa akizingatia taratibu za kiitifaki za kutoa neno la shukrani baada ya Rais Kikwete kutoa hotuba.

  Baada ya kitendo hicho kulionekana kuwepo kwa miguno kutoka kwa baadhi ya wazee waliohudhuria mkutano huo wakishindwa kuelewa kilichokuwa kikiendelea kwenye meza kuu.

  Hatimaye baada ya jitihada za ushawishi kushindikana Mbita aliamua kutoa neno la shukrani kwa Rais Kikwete akibainisha kuwa hotuba yake imejaa nasaha nzuri na muhimu kwa Watanzania wote.

  Katika hotuba hiyo Rais Kikwete alizungumzia mambo ambayo katika kipindi cha karibuni yamekuwa yanawagusa Watanzania wengi, yakiwemo yanayohusu matatizo ya kiuchumi na uundwaji wa katiba mpya.

  Kuhusu uchumi, Kikwete aliwataka Watanzania kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho Tanzania na mataifa mengine duniani yanakabiliwa na athari za kiuchumi.

  Miongoni mwa athari hizo alizozitaja ni pamoja na kasi ya mfumuko wa bei ambayo haijawahi kushuhudiwa katika historia ya nchi, kushuka kwa thamani ya shilingi, kupanda kwa bei ya mafuta na kuadimika kwa sukari inayozalishwa nchini kutokana na kuuzwa kimagendo kwa nchi jirani.

  Alisema serikali yake iko mbioni kukabiliana na baadhi ya matatizo na moja wapo ni kuagiza sukari kutoka nje.

  Lakini tatizo kama vile kupanda kwa bei ya mafuta na kushuka thamani ya sarafu huku dola ya kimarekani ikipaa, alisema ni tatizo kwa nchi nyingi duniani.

  Kuhusu Katiba, Kikwete alipinga hoja zilizokuwa zikitolewa na Chadema pamoja na wanaharakati wa mabadiliko ya katiba.

  Mojawapo ya hoja hizo, alisema wanapotosha kuwa suala la muungano limekatazwa kujadiliwa.

  Ukweli alisema wanapinga kwenye mchakato wa kuandaa rasimu kujadili juu ya kuvunja muungano lakini wanaruhusu maoni ya namna ya kuuboresha.

  Aliwahakikishia Watanzania kuwa katika mchakato wa kuandaa katiba hiyo, watakuwa huru katika kutoa maoni yao.

  Lakini akaonyesha wasiwasi wake kuwa kuna makundi ya watu yanayoweza kuhamasisha watu juu ya mambo yenye maslahi kwao hivyo akaonya:

  "Ninataka wananchi wawe huru. Mtu asilazimishwe la kusema."

  Akijua wazi kuwa Chadema wamekuwa wakishinikiza mambo mbalimbali kwa maandamano kwa hoja ya kutumia nguvu ya umma, Kikwete akaonya:

  "Jambo hili halihitaji maandamano… Vurugu hazina faida bali kuwaongezea machungu Watanzania. Hivyo naomba wawe na busara. Tuchague njia ya faraja. Tusichague njia ya machungu."


  NIMEJIULIZA SIJAPATA JIBU HEBU WATAMBUZI NISAIDIENI MTAZAMO WENU!
   
 2. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #2
  Nov 20, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  au alilalala wakati hotuba inaendelea??
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Nov 20, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kuna cha kushukuru pale?
   
 4. u

  utantambua JF-Expert Member

  #4
  Nov 20, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kingunge hata wewe? Ama kweli siku ya kufa miti nyani wote huteleza.
   
 5. JIULIZE KWANZA

  JIULIZE KWANZA JF-Expert Member

  #5
  Nov 20, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0


  hilo nalo neno....anyway time will tell
   
 6. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #6
  Nov 20, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Alitakiwa azungumze na vijana siyo wazee. Hebu fikiria kwa akili ya kawaida, mambo mengi sasa yanaendeshwa kwa mfumo wa kiteknolojia, mfano kijana akiwa na simu ya blackbery anakuwa ameweka dunia katika kiganja cha mkono, lakini the same blackbery ukimpa mzee kama kingunge ataitumia kupiga/kupokea simu na kutuma sms. Jk anakwepa changamoto za vijana na alaaniwe!
   
 7. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #7
  Nov 20, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,593
  Likes Received: 4,699
  Trophy Points: 280
  Aliamua kutii dhamira yake kwa mara ya kwanza katika maisha yake.Wana CCM wote hukiri kile wasichokiamini ili kulinda maslahi yao.
   
 8. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #8
  Nov 20, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180

  hakika hakuna..naona mzee anaona amalize siku zake kwa amani
   
 9. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #9
  Nov 20, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  ni kama vile anasema TUKUBEBe VIPI KIJANA WETU?
   
 10. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #10
  Nov 20, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  it is already telling!

  mwenye macho haambiwi ona!
   
 11. N

  Ngoiva JF-Expert Member

  #11
  Nov 20, 2011
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  1.Hivi kikwete aliongea na wazee wa dsm kwa niaba ya watanzania wote au kwa niaba ya chama chake na wanaccm?
  2. Hivi kikwete aliongea na wazee wa dsm kama Rais au kama m/kiti wa ccm?
  Bado sijajua mandhari na maudhui ya hutuba ya kikwete kwa wazee wa dsm.
   
 12. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #12
  Nov 20, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Aliwaambia wazee kuwa atasaini sheria ya kuunda rasimu ya katiba. Hapo nadhani utakuwa umeshajua alikuwa anaongea kama nani.
   
 13. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #13
  Nov 20, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  pale alitafuta audience ya kusemea tu ambayo haitambeza baada ya kushtushwa na waraka wa kumwambia akae pembeni
  wajumbe wa nyumba kumi hawana la kufanya hivyo ndio maana walikuwepo
   
 14. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #14
  Nov 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Hana amani hapo mkuu, huyo mzee na wazee wenzake walioshiriki kuliasisi taifa hili na misingi yake (imara na legelege) na tena wakashiriki kuivuruga na kuiua misingi ile imara (Azimio la Arusha), wana mengi sana mioyoni mwao!

  Kama hawatafanya toba na kulilia taifa hili na kuweka sawa kumbukumbu, hakika dhamiri zao zitawasumbua hata wakiwa wamekufa!
   
 15. M

  Mat.E Member

  #15
  Nov 20, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kingunge anajua Kikwete alichokuwa akiliambia Taifa. Alihofu naye kujumuishwa itakapojulikana kwa wa Tanzania. HONGERA KINGUNGE,Umeanza ku-improve!
   
 16. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #16
  Nov 20, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hakulala. Mzee si ni mpiga deki wa Mamvi kwa hiyo akapata kigugumizi kutoa maoni maana aliogopa angemuudhi mwajiri wake huyo anayemfundisha wizi uzeeni.
   
 17. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #17
  Nov 20, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Aliongea nao au alikuwa anaongea asikilizwe? Kama ni kuongea nao wangeweza kuuliza kitu au kuchangia kwenye kila alichozungumza. Wazee wamechoka kama vile wanaishi kwenye jangwa, thinking capacity yao ni iko low. Ki ukweli nilichosikia kwenye ile hotuba ni vijembe tu. Na kucheka kusikokuwa na vina kama kawaida yake.
   
Loading...