Babu auawa Moshi baada ya kubaka mtoto na kumuambukiza Ukimwi

charles ndagulla

Senior Member
Feb 18, 2016
168
107
Babu anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 68 mkazi wa Kijiji cha Lego Muro wilaya ya Moshi Vijijini,ameuawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kudaiwa kumbaka mwanafunzi wa kike wa Darasa la pili na baadaye vipimo vya kitabibu kudhibitisha kuwa ameambukizwa virus vya Ukimwi.

Tuio hilo baya na la kusikitisha,limetokea Novemba 7 mwaka huu kijijini hapo baada ya mtuhumiwa huyo awali kutoweka baada ya kubaini anasakwa na wananchi lakini kutokana na umri wake mzee huyo aliamua kuanza kurejea mdogo mdogo kijijini hapo kwa kificho na ndipo wananchi walipopata taarifa na kuanza kumsaka.

Jeshi la polisi Mkoani Kilimanjaro kupitia kwa kamanda wake wa Mkoa,Hamis Issah,limedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kumtaja marehemu kuwa ni Theobist Gabriel(68).

taarifa kutoka kijijini hapo zinapasha kuwa,mtoto huyo baada ya kufanyiwa ufedhuri huo alimtonya shangazi yake lakini shangazi akapiga kimya na baadaye mtoto akamweleza mama yake mzazi ambaye alianza harakati za kuwafanyia vipimo watoto wake wote kubaini kama wanayo maambukizi.

Baada ya vipimo hivyo ni mtoto huyo pekee aliyebainika kuwa na maambukizi na kutokana na wanananchi kuwa na taarifa za mtuhumiwa kuwa na maambukizi ya virus vya Ukimwi kwa muda mrefu,walijiridhisha kuwa ndiye aliyemwabukiza mtoto huyo.

Hapo ndipo msako ulipoanzaa na baadaye babu huyo alipobaini kuwa anasakwa,alikimbia mji na kwenda kujificha kusikojulikana lakini arobaini ikifika hata ukijificha mbinguni utakamatwa tu na ndicho kllichotokea.

Mungu ailaze roho ya marehemu pahala pema peponi
 
Aisee.. mzee alikuwa Mkatili vivyo hivyo wananchi hawakutakiwa kujichukulia sheria Mkononi!
 
Mleta mada hii habari umeandikwa kukua kuda, utasemaje mtu apemzishwe peponi aisee?? Au unamaanisha kwenye MAPEPO??
 
Siku aliyobakwa angelikuwa muwazi na wazazi/walezi kuwa waelewa na kumpeleka hospitali mtoto angelipata tiba na hasingekuwa na virusi vya UKIMWI.
 
Wamekosea kukauwa kalitakiwa kabaki duniani kwa mateso mpaka kajute,ona sasa wamewahi kukauwa hata mda wa kujuta hakajapata
 
Wamekosea kukauwa kalitakiwa kabaki duniani kwa mateso mpaka kajute,ona sasa wamewahi kukauwa hata mda wa kujuta hakajapata
Wangestahili wamuuwe taratiiiibu kama kumwambia ale mkungu wa ndizi mbichi hadi aumalize
 
Kwa wazee wa kichaga suala la kubaka ni jambo la kawaida... Sema tu mbakaji alikua ana maambukizi..
 
Back
Top Bottom