Tunajua wote kuwa plagiarism ni serious academic offence! Lakini hili swala sasa limesambaa na kwenda mbali zaidi hadi kwenye jamii ngazi ya familia. Unakuta mke wa mtu ameolewa, halafu sijui kwa makusudi au kwa nia gani anaamua kupigwa "force king", matokeo yake ndio hivyo anaplagiarise mtoto.
Jana nilipita karibu na mlango wa jirani fulani, sasa ndani kulikuwa na akina mama na akina dada kibao. Bahati nzuri au mbaya kuna dada mmoja tumezoeana hapa mtaani, akawa ameniita, njoo uone mtoto jamani, mama fulani amejifungua.
Anyway, huyo mama sijazoeana naye kihivyo, lakini kama unavyojua kumwona mtoto hasa sisi vijana na kumnyanyuanyanyua kisanii hata kama hujisikii kivile, inakuwa kama kusafisha nyota kimtindo. Kwa hiyo mie nikamwibukia mtoto, nikambeba na kumrusharusha kidogo (taratibu, si unajua bado mchanga!).
Huko nyuma nilisikia huyo mama jirani anacheza faulu kibao! Nilipomshika tu mtoto, akina mama:
" Toto, toto, toto; ghii, ghii, ghiii, dume, dume, dume hiloooooo, handsome kama baba yake, ............"
Mama mwingine "Masikio hayo, kichwa jamani hicho, miguuuuu! Huyu ni baba yake kabisaaaaa, kajizaa"
Sasa mama mmoja, ghafla akaguna, "MMMmmh, mbona hata hafananii kabisa na baba yake, sema labda huu weupe ni wa mama yake!"
Mie fasta fasta, nikawa namtafuta mmama wa kumkabidhi mtoto nisepe, ndio mama mwingine "alimrebuke" yule aliyesema mtoto hata hafananii na baba yake, "Utasutwa mwanamke, heheeeeeeee, mjini hapa!"
Kidogo jamaa, mme wa mke mwenye mtoto mchanga, kaibuka kutoka chumbani, kaanza kunisalimia "Mambo vipi Simplicity., karibu sana mkuu, tupo bwana,........."
Aliwapotezea kabisa akina mama wote waliokuwepo hapo, badala yake tukawa tunabadilishana salamu mimi na yeye.
Ghafla mama wa mtoto naye kaibuka, na kumwambia mama mmoja ambaye nilikuwa nimemwachia mtoto "Nipe mtoto nikamwoshe", huku akiwa amekunja uso na kuonekana kutokufurahia!
Kuona hivyo, mie "kwa herini jamani, ahsanteni, nawahi sehemu", huyoooooooooo, mtaa wa kati.
Kilichoendelea sijui, ila jinsi hao akina mama walivyokuwa wanatumiana signals kishambenga huku wengi wao wakiwa macho juujuu, kuna uwezekano waliditect plagiarism!
Jamani hili swala la akina mama kuplagiarise watoto na wapambe wao kujaribu kuwanusuru kwa kuwapa watoto fake brands mbona linakua kwa kasi sana siku hizi?
Mtu ukianzisha bima ya kupakaziwa mtoto si utapiga hela ndefu sana au mnaonaje wadau? Hasa kama unaweza kumudu kununua vifaa vya kupima DNA na kuajiri wataalamu huku ukitangaza "widely" ili watu waje kupata huduma?
CC: lara 1 MadameX Madame B madameA Kongosho Nazjaz Kaunga Smile Sista sister charminglady christine ibrahim Cynthia Chriss mimi49 Heaven on Earth mwekundu watu8 Mashaxizo Himidini HorsePower farkhina King'asti mzabzab etc.,