BABATI: Wazazi waajiri Mwalimu wa hesabu, wamlipa mshahara

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,588
11,668
UKOSEFU wa walimu wa hesabu umewafanya wazazi wa watoto wanaosoma katika Shule ya Sekondari Bagara wilayani Babati kuunda kamati ya kuboreshai taaluma shuleni hapo.

Katibu wa Kamati hiyo, Dismas Kokumo alipozungumza na MTANZANIA juzi alisema wazazi wamekubaliana kuchanga Sh 25,000 kila mmoja kwa ajili ya kumlipa mwalimu wa somo hilo.

Alisema vilevile wamekubaliana kutoa Sh 5,000 kila mmoja kwa mwaka kwa ajili ya kununu karatasi.

“Baada ya kuona kuna tatizo la walimu wa hesabu tulikubaliana wazazi tuchangie Sh 25,000 kwa ajili ya kumlipa mwalimu kwa mwaka kila mwanafunzi na Sh 5000 za karatasi,’’ alisema Kokumo.

Alisema wameweka utaratibu wa wanafunzi kupewa mazoezi na mwalimu huyo kujua kama wanachofundishwa wanakielewa . Kokumo alisema kamati iliyochaguliwa na wazazi ndiyo inaratibu suala la kumlipa mwalimu baada ya michango kuchangwa na fedha kuhifadhiwa katika Benki ya CRDB.

“Kupatikana kwa mwalimu wa hesabu kumesaidia kuongeza ufaulu katika shule hii maana tumetoka zero 80 mwaka uliopita hadi zero tano ambazo ni za wale watoro,’’ alisema. Naye Mkuu wa Shule hiyo, Emmanuel Dahaye, alikiri wanafunzi kuchangishwa michango kwa ajili ya mwalimu wa hesabu baada ya uamuzi wa wazazi.

Alisema kufanya hivyo kulitokana na waraka wa elimu uliotolewa na TAMISEMI uliowataka kufanya hivyo inapobidi baada ya kukubaliana na wazazi.

"Ni nyaraka ambazo tulipewa kwamba shule inapokuwa na tatizo fulani wazazi wenyewe wafanye uamuzi, wafanye mchanganuo na hizo shughuli zote ziratibiwe na wazazi wenyewe," alisema Dahaye.

Alisema baada ya kukubaliana waliamua kila mwanafunzi achangie Sh 12,500 kwa muhula mmoja lakini hata ambao hawachangii kwa wakati hawawafukuzwi bali wanavumiliwa.

Mtanzania.

Unyania ni unyani tu kwa viongozi wetu.
 
Serikali imegoma kuajiri waalimu, huko mtaani kuna waalimu wengi tu wa hesabu!
Waliohitimu mwaka 2015 na 2016..
 
Hakuna kitu cha Bure duniani, SERIKALI ya awamu hii imejitahidi kufanya kile ikichaahidi kwa asilimia ambacho kilishindakana kufanyika kwa miaka 30 iliyopita,hata hivyo itachukua mda kwa SERIKALI hii ya Sasa kutekeleza ahadi hiyo kwa 100℅ katika mazingira kama haya wazazi wanaona mbali wameamua kujiongeza ili kuongezea nguvu juhudi za SERIKALI kutoa elimu bure kwa vijana wake.Hilo halina ubaya na anayepinga kwa kigezo kua SERIKALI iliahidi itatoa elimu bure huyo atakua kakosa busara.
 
Mmhh, elimu bure bila mkakati madhubuti ni kurudisha elimu nyuma na kuwapa wazazi mawazo. Ni heri ilivyokuwa mwanzo ambapo mzazi anajua ninajukumu fulani kuliko. Anko angalia vizuri bado unayo miaka 2.5 mbele siyo mbaya ukijisahihisha mapema. Kwa taarifa hii ni mfano wa namna ambavyo katika shule zilivyo. Hongera hao waliokubaliana kufikia lengo hilo je maeneo ambayo hayana maelewano nini hatma ya hao wanafunzi?
 
Elimu bure haiwezekani kwa hali halisi ilivywo. Walimu hawatoshi sasa je watoto wasifundishwe ikiwa hamna walimu. Wazazi wasipojiongoza hasara ni kwa watoto wao.
 
Back
Top Bottom