BABATI, Manyara : Waziri Mkuu akuta ya ajabu Minjingu

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
814c5de291159e46ae4da62c2b63df74.jpg
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema haridhiki na hali aliyoikuta kwenye Kiwanda cha kutengeneza Mbolea cha Minjingu baada ya kubaini kuwa wanatumia mifuko yenye lebo ya Kenya wakati mbolea hiyo inazalishwa hapa nchini

Kutokana na hilo, Waziri Mkuu amewataka wamiliki wa kiwanda hicho waandike barua kwa Rais John Magufuli kabla hajamaliza ziara yake Jumatano, Februari 22,2017 apate nakala ya barua hiyo

Ametoa agizo hilo leo baada ya kutembelea kiwanda hicho kilichopo wilayani Babati akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake mkoani Manyara. Waziri Mkuu amerejea Babati leo akitokea Dar es salaam ambako alikuwa na ratiba za Kitaifa

"Nilikuja kukagua kiwanda baada ya kupokea malalamiko kuwa mbolea hii haikubaliki huko vijijini. Watafiti wameonyesha kuwa ikitumika inasaidia kutoa mazao mengi. Lakini wakati niko Kiwandani nimekerwa kukuta mifuko ya kupakia mbolea hii ina anuani ya Nairobi, Kenya wakati mali ghafi inatoka Tanzania", alisema
0a82b8ee0a761b843bc32af08c80bd0d.jpg

"Ni kwanini mifuko hii ina anuani ya Kenya.? Hapa tulipaswa tuone anuani ya Babati.! Je mlipata kibali kutoka Serikalini? Tena kuna lebo ya TBS. Kwanini Tanzania haionekani? Kwani malighafi iko Kenya? Haiwezekani, lazima uandike barua na uombe radhi kwa Mheshimiwa Rais Magufuli. Yeye anahimiza ujenzi wa viwanda ndani ya nchi, halafu ninyi mnafanya hivyo"?

Akiwa ndani ya kiwanda hicho, Waziri Mkuu alikuta baadhi ya mifuko ya mbolea ikiwa imeandikwa : "County Government of Bungoma", ina nembo ya Serikali ya Kenya, na anuani ilionyesha kuwa mbolea hiyo imetengenezwa na kiwanda cha mbolea cha Minjingu lakini anuani inasomeka P. 0 Box 2941-00200 Nairobi, Kenbro Industrial Park, Mombasa Road', namba ya simu +254-20-6000-970 lakini mifuko hiyo pia ina muhuri wa TBS.

Chanzo: Mwananchi
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Duuh, hivi kila kitu chetu kizuri ni Mali ya Kenya? Hii ni hujuma, ? Uzembe,? Au kuna nini kinachoendelea kati yetu na hawa Watu wa Kenya? Hivi wanakuwa hawajui kweli? Au.....
 
Yani mpaka waziri mkuu afike na kugundua hili? Hivi atafanya mangapi. Ni muhimu watendaji wetu wawe serious.
 
Duuh, hivi kila kitu chetu kizuri ni Mali ya Kenya? Hii ni hujuma, ? Uzembe,? Au kuna nini kinachoendelea kati yetu na hawa Watu wa Kenya? Hivi wanakuwa hawajui kweli? Au.....
Sisi Watanzania tunaona fahari kuwa Wakenya ndio wawekezaji wakubwa nchini wacha yatukute.
 
Usalama wa taifa, n.k. walikua hawajui hili kweli...??
Nchi inahujumiwa halafu wana usalama wako tu...??
 
Mods..!

Naomba heading iwe hivi 'Majaliwa akerwa mbolea ya minjingu kupewa lebo ya Kenya' ataka waandike barua ya kumuomba radhi Rais '
 
Waziri Wa Kilimo
Bwana/Bibi Kilimo Wa Kanda
Bwana/Bibi Kilimo Wa Mkoa
Bwana/Bibi Kilimo Wa Wilaya

Halafu Unaambiwa Watu Hawa Ni Wasomi
Mkuu Wa Mkoa
Mkuu Wa Wilaya

Hao Viongozi Wanangoja Nini Kutolewa Nje Ya Utendaji
 
Back
Top Bottom