Niko
Member
- Mar 12, 2011
- 99
- 21
Taarifa ya television ya TBC saa saba imeonyesha wananchi wenye hasira mjini Babati walioamua kupasua mabomba ya Mamlaka ya Maji Safi na Taka BAWASA baada ya fujo za kupinga mkazi mmoja mwekezaji kuungiwa bomba fasta kifisadi wakati wao wanahenya na "wanawake wanazaa njiani wakihenyea maji."
BAWASA imekiri imesimamisha mpango wa kuendelea kupeleka maji kwa mtu huyo na imeomba mazungumzo ya amani na wananchi.
Na huko Songea TBC inaripoti wananchi wenye hasira kali walizua tafrani kupinga ufisadi wa ujenzi wa ofisi ya Mwenyekiti wa Kijiji, jengo jipya ambalo limeonyeshwa bawaba za milango zake zinang'oka hata na mikono, wakati zilitakiwa zijengwe bawaba za Union na ubovu mwingine. Mwenyekiti ameambiwa wewe ni mwizi, mpambe wake mmoja anusurika kuraruriwa kwenye mkutano wa kijiji.
Maoni yangu: Kama watu mpaka vijijini na miji ya kila pembe ya nchi wanaanza kuamka namna hii, hii ni very healthy situation for the country. Siku hata siku inazidi kuwa ngumu kutawala kwa kuburuza na kufisadi nchini Tanzania, mpaka kutawala kijiji sasa hivi sio rahisi rahisi tu. Watu wanaamka.