BABATI: Askari wa FFU amuua mkewe kwa kumpiga risasi nne lindoni kwa ugomvi wa mafunzo ya mtoto

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
d165f100ab986154183f62c4b9d24532.jpg
Polisi wilayani ya Babati mkoani Manyara inamshikilia askari wa Jeshi hilo Kikosi cha Kutuliza Ghasia FFU, Cosmas James akituhumiwa kumuua mzazi mwenzake, Regina Daniel 23 kwa kumpiga risasi nne.

Chanzo cha mauaji hayo inadaiwa ni mzozo ulitokea baada ya Regina kumfuata James lindoni kudai fedha za matumizi ya mtoto.

Akizungumza tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Longinus Tibishubwamu alisema lilitokea mjini Babati jana saa 12. 30 jioni.

Alisema askari huyo alikuwa lindoni katika Benki ya NMB tawi la Babati, Mtaa wa Usalama Kata ya Bagara.

Kaimu Kamanda Tibishubwamu alisema marehemu Regina alikuwa mkazi wa Mtaa wa Ngarenaro mjini Babati.

Alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa kabla ya kifo cha mwanamke huyo kulitokea mzozo kati ya wawili hao kuhusu fedha za matumizi ya mtoto.

"Wakati wakiendelea na mzozo ndipo askari kwa kutumia silaha aliyokuwa nayo alimpiga Regina risasi nne kwenye paji la uso, kifuani na shingoni", alisema

Baada ya tukio hilo, alisema mtuhumiwa aliitelekeza silaha lindoni na kwenda kujisalimisha polisi na askari waliokwemda eneo la tukio ndiyo walioichukua huku pia wakiokota maganda matatu ya risasi.

Kaimu Kamanda Tibishubwamu alisema mtuhumiwa yuko mahabusu kwa mahojiano kabla ya hatua nyingine kuchukuliwa na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali mjini wa Babati Mrara.
 
Unaenda kudai pesa lindoni wakati unajua kabisa lindoni mdaiwa huwa ana bunduki yenye risasi na hana pesa wala kadi ya benki unatarajia nini?

Maaskari wa kwenye Malindo yoyote yale hawaruhusiwi kusogelewa na mtu yoyote kwa utaratibu wa ulinzi.

Ila Askari wa kwenye lindo ndiye mwenye ruksa ya kusogea mahali anapoona kuna hali isiyo ya kawaida na hata kutoa amri kwa yoyote yule eneo la lindo lake.

Maaskari wengi wanafanya kazi kwa mazoea maeneo ya Malindo na hilo ni shida kubwa
 
Kwa hiyo Tatizo ni mwanamke kwenda kudai matumizi ya mtoto au kuna kingine zaidi
 
Askari hawa sijui wakiwa na Bunduki zile mabegani mwao hujiona wao ni wadogo zake na Mungu au Mtume.

Ovyo sana, kama mwanamke unaua kwa risasi mwanaume si utamuua na Satan 2 ya Warusi.

Form Four division 5.
 
Askari wakiwaga na silaha wanajionaga nusu miungu....usiwakaribie wala kubadilishana nao maneno...kuna haja wawe wanafundishwa psychology na emotions intelligence... I was almost killed kisa parking...tena bank nimeenda tu kwenye atm mazafanta
 
Back
Top Bottom