Waziri wa Wamasai (Baba yoyo, a.k.a Mzee wa mamvi) alialikwa kanisani kuchangia ujenzi wa kanisa na ununuzi wa vifaa vya kwaya.
WAKATI WA IBADA HALI ILIKUWA HIVI:-
MCHUNGAJI: Wapendwa katika kristo, leo tunaye mgeni muhimu sana hapa ambaye amekuja kutuchangia harambee ya kukamilisha ujenzi wa kanisa letu. (Anamkaribisha mgeni, na mgeni anaamka kwa mbwembwe na makeke kutoa ahadi yeke mbele ya kanisa)
MGENI (BABA YOYO): Mimi atachangia silingi milion 100, ngombe moja wa masiwa kwa mchungaji na seti ya fifaa fya bendi ya kanisa (akimaanisha kwaya). Pia atatoa ngombe moja wa kuchinja siku ya krismasi.
MCHUNGAJI: Haleluyaaaaaa!! .....makaofi kwa mdhamnini wetu.....papapa aaaaa!
papapaaaaaa! papapaaaaaa!!!! !
WAUMINI: Mungu akubariki sana. Wanafiki wanao kuandama kwa ufisadi, washindwe na walegee kwa jina la Yesu.
BABA YOYO: Asante sana ndugu zangu katika kristo. Mungu hamtupi mja wake. Mimi siku zote huwa nasali nikimuomba siku moja Mungu aje waumbue kina Nape na Chiligati waliotembea nchi nzima wakinitangaza kwamba mimi ni fisasi huku wakijua kwamba mimi ni msafi, mtakatifu na nimeokoka na kumkiri Yesu. Washindwe katika jina la Yesu kwa unafiki wao, waongo wakubwa!
WAUMINI: Sema baba semaaaaaaa!!! Hakunaga kama wewe Tanzania hii. Mwaka 2015 tutakusaidia kuingia ikulu jinsi nawe unavyotusaidiaga misaada ya ujenzi wa kanisa.
WAZEE WA KANISA (huku wakinong'onezan a kwa sauti za chini chini lakini kwa busara ya kiutu uzima): Wajinga ndio waliwao, ukila na kipofu usimguse vyanda, cha mlevi huliwa na mgema. Jambo la muhimu ni kwamba kanisa letu litakamilika. Hayo mengine yote anayotarajia kutoka kwa waumini ni ndoto za Ali Nacha. Wanampa bichwa bure!