Baba yangu anatarajia kustaafu utumishi. Nimsaidieje aweze kujikwamua baada ya kupata pensheni?

MONA WA KYEN

JF-Expert Member
Dec 23, 2016
340
271
Habari wanaJF, natumaini mwaendelea vema.

Niende moja kwa moja kwenye mada ndugu zangu baba yangu mzazi alikuwa mwalimu sasa wiki moja iliyopita huyu mzee kastaafu kazi. Kiukweli najua atapewa mafao yake ya uzee ila sasa najua kuna wengi wamepokea hayo mafao na wakayachezea wamebaki masikini kabisa.

Ninavyomjua huyu baba biashara hajui kabisa maana anapenda kuheshimiwa hatari kwa hiyo lugha ya biashara hana kiufupi itamsumbua na ataishindwa. Sasa akili yangu imekuwa inagonga sana nimsaidieje huyu baba angalau aweze kujikwamua na haya maisha asibaki nyumbani.

Nafahamu kuwa kuna wengi humu ndani walikuwa wafanyakazi wa serikali na wamestaafu lakini wameweza kujikwamua na maisha kwa namna moja ama nyingine, pia naamini humu ndani pia kuna watu wazazi wao waliweza kujikwamua na maisha kwa namna mbalimbali baada ya kustaafu.

nawaombeni ushauri ndugu zangu. ahsanteni.
 
Hongera sana,kupata baba mstaafu. Sina ushauri mkubwa sana ila msikilize mwenyewe anataka nini,,maana wastaafu wengi huwa wameshapanga wanachotaka kufanya na pesa zao.Ila msisitize kumaintain ile tabia ya kutoshinda nyumbani maana inasababisha stress na vifo vya mapema.
 
nashukuru mkuu kwa ushauri wako
 
Hongerah sana ongea naye anachofikiria kufanya. Ila mshauri kitu kimoja. Nusu ya pesa atakazopata aweke kwenye fized accoint kwanza ya miezi sita ili ajipange vizuri maana cash nayo ina majaribu yake. Sasa ushauri ni mgumu kwani mazingira yake hujaelezea kuwa yuko wapi etc. Ninamfahamu mstaafu fulani tena alikuwa mwanamke. Alikuwa amekwishajenga nyumba yake nae alisema asilani hawezi kufanya biashara yeye mwenyewe. Amejenga Frame 4 za maduka mbele ya nyumba yake hivyo anapokea kodi. Hongerah kwa kumjali Baba yako. Unanikumbusha Tangazo la LPF baba anaomba kumuoa Binti ambaye anamjibu mzee atumie pesa zake vizuri, Mbaya zaidi Binti anatoa bonge la Tabasamu ambalo lingeweza mchanganya Mzee. Hongerah sana kujali mustakabali wa mzee wako!
 
Kama unaishi nje ya Dar es Salaam ungemshauri mzee atafute kiwanja ajenge nyumba ya kupanga......awe anasubiria rent.

Uwekezaji wa namna hii hausumbui kichwa pia ni urithi hata yeye akiondoka
 
Akifikiria business ambazo nature yake inahitaji umakini sana ni rahisi kushindwa ukizingatia hana back ground ya business. Pangeni mambo kwa makini......milioni 100, 120 zinaisha haraka tu usipokuwa na mipango
 
Angry Bird ushauri mzuri.

Nimekumbuka game ya Angry Birds imebidi niende App Store kuangalia kama bado ipo halafu ndiyo nikasema ngoja nijibu ujumbe wako.

Yes bredren, mzee akiangalia option hii uliyotoa huku ame-invest his money into real estate life won't be stressful for him. The target there should be both his health and financial freedom.

Cheers
 
Atafute bajaj ,kwa mil 6 moja kwanza.hii baada ya miaka mitatu inazaa mwenzie tena kwa mil 6 na pesa ya kula haitokosekana milele.
Kwa siku bajaji inakuletea 15,000 kwa dsm kwa wiki ni 75,000 .pesa ya kula ipo tu.
Bajaji haina ushuru,
Bajaji inaendeshwa masafa mafupi fupi (haichoki) lakini ni nafuu ya tax kwenye charge watu wanazipenda.
Bajaji zinapendwa na watalii na wajanja wa kishua wasiopenda boda boda.
Kama wewe ni wa kiume uwe dereva utailinda na pesa yake utaongea mpaka basi.
 
Aanzishe mradi mmjo kati ya kufuga kuku, kufuga samaki, kama yuko kijijini anunue tractor hatojuta , pia anaweza kuanzisha kilimo cha kisasa cha bustani/mbogamboga kwa njia ya umwagiliaji walau ainstal ekar moja ya drip irrigation kwa kutumia either maji ya mto/ziwa au kuchimba kisima na fedha zingine aweke bank fix account
 
Hongerah sana ongea naye anachofikiria kufanya. Ila mshauri kitu kimoja. Nusu ya pesa atakazopata aweke kwenye fized accoint kwanza ya miezi sita ili ajipange vizuri maana cash nayo ina majaribu yake. Sasa ushauri ni mgumu kwani mazingira yake hujaelezea kuwa yuko wapi etc. Ninamfahamu mstaafu fulani tena alikuwa mwanamke. Alikuwa amekwishajenga nyumba yake nae alisema asilani hawezi kufanya biashara yeye mwenyewe. Amejenga Frame 4 za maduka mbele ya nyumba yake hivyo anapokea kodi. Hongerah kwa kumjali Baba yako. Unanikumbusha Tangazo la LPF baba anaomba kumuoa Binti ambaye anamjibu mzee atumie pesa zake vizuri, Mbaya zaidi Binti anatoa bonge la Tabasamu ambalo lingeweza mchanganya Mzee. Hongerah sana kujali mustakabali wa mzee wako!
NASHUKURU SANA MKUU YUPO KIJIJINI, unamaanisha fixed account?
 
Aanzishe mradi mmjo kati ya kufuga kuku, kufuga samaki, kama yuko kijijini anunue tractor hatojuta , pia anaweza kuanzisha kilimo cha kisasa cha bustani/mbogamboga kwa njia ya umwagiliaji walau ainstal ekar moja ya drip irrigation kwa kutumia either maji ya mto/ziwa au kuchimba kisima na fedha zingine aweke bank fix account
ahsante kwa ushauri mzuri kwa nini umesema akinunu tractor hatojuta? maana nilikuwa na wazo kama hilo na ni kweli yupo kijijini.
 
Kustaafu Maana yake ni kupumzika sio kubadilisha shughuli ya kufanya.

Mie nimestaafu naelewa maana ya kupumzika na ninapumzika.

Kama Ana Pension na hakujipanga vizuri kimaisha na Wewe akili zako zimetulia ( Sio Limbukeni) Basi Kama kuna Shughuli ya kufanya Basi Wewe Kijana ndio uwe Mfanyaji!
 
Atafute bajaj ,kwa mil 6 moja kwanza.hii baada ya miaka mitatu inazaa mwenzie tena kwa mil 6 na pesa ya kula haitokosekana milele.
Kwa siku bajaji inakuletea 15,000 kwa dsm kwa wiki ni 75,000 .pesa ya kula ipo tu.
Bajaji haina ushuru,
Bajaji inaendeshwa masafa mafupi fupi (haichoki) lakini ni nafuu ya tax kwenye charge watu wanazipenda.
Bajaji zinapendwa na watalii na wajanja wa kishua wasiopenda boda boda.
Kama wewe ni wa kiume uwe dereva utailinda na pesa yake utaongea mpaka basi.
sawa sawa nimekupata kaka yupo kijijini na mimi ndo kwanza nimemaliza chuo mwaka jana kwa neema ya Mungu
 
Kustaafu Maana yake ni kupumzika sio kubadilisha shughuli ya kufanya.

Mie nimestaafu naelewa maana ya kupumzika na ninapumzika.
sawa kabisa mku unyamudu vipi maisha yako? maana huyu mzee hana mtoto hata mmoja alie na kazi ndo kwanza mimi first born na nimemaliza chuo mwaka jana wadogo wengine bado wanasoma
 
Back
Top Bottom