baba yangu alivyomtesa mama yangu

baba yangu alivyomtesa mama yangu

mkonowapaka

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2010
Posts
1,492
Reaction score
772
ni usiku wa kama saa tano ivi namsikia mama akilia kwa uchungu wa kupigwa na kiatu cha baba.....mama anakimbilia kwa watoto baada ya kuona kipigo kimezidi,kwa wakati huo nilikua mdogo wa kama miaka 5 ivi na nililala na dada yetu wa kazi na mdogo wangu wa kike..[uhaba wa vyumba].....kama vile haitoshi baba alivamia chumbani na kuendelea kumpiga mama..nililia sana kwa wakati huo nilichoweza kukifanya ni kufungua mlango alioufunga baba na kuweka mazingira ya mama kutorokea nje mimi na yeye........nakumbuka siku hiyo nilikaa nje tangu saa sita hadi saa 8 huku mvua ikitunyeshea..........na mama alivimba mwili mzima..

baba alifunga milango yote akalala....baadae nilimwomba dada yetu afungue kwa taratibu maana baba alikua akikoroma hivyo kutosikia..nikaingia ndani na mama tukalala........tulijifungia mlango nakumbuka..

asubuh baba alikuja kugonga mlango,haukufunguliwa aliishia kuuvunja na kisha kumhoji mama kwa nini amelala kwa watoto.......akampiga makofi na kisha kwenda zake kazini........

nakumbuka nilikua kindergaten,na mama yangu ndie aliyenipeleka........

vipigo hivi viliendelea siku hadi siku pamoja na vikao kuwekwa mara kwa mara........ila tulikuja kugundua baadae alikua n amwanamke mwingine..na siku akienda huko akirudi ni lazima mama apigwe.Mama alikua mvumilivu sana,si kwa ajili yetu tu bali pia alikua ni mtu wa kusamehe haraka sana,alikua na moyo wa upendo wa hali ya juu

baba alitangulia mbele za haki mwaka 2011.........apumzike kwa amani,japo pengo lako bado lipo ila baba ulikua katili sana kwa mama.Mungu akusamehe kwa hilo...

Nimejifunza mengi sana kwa experience ile ya maisha,namshukuru Mungu kama mwanaume/kijana ninayejiamini na kujitambua..........nina familia [ndoa rasmi mwaka huu],elimu,kazi na kikubwa upendo na heshima si kwamke wangu tu bali pia kwa wanawake wote....nawapa pole wanawake wote wanaopitia magumu yasababishwayo na sisi wanaume......wazidi kumuomba Mungu wao nakuwa wavumilivu.......haya ni mapito tu,twautafuta mji udumuo!!

WANAUME TUBADILIKE TUACHE UNYANYASAJI WA NAMNA YEYOTE ILE.
 
Ukatili wanaofanyiwa wanawake majumbani unatisha, baadhi ya sababu zinazopelekea ukatili kama huu ni ulevi uliopindukia na nyumba ndogo, mwanaume akishapata nyumba ndogo basi wewe mama huna tena maana, ni chuki na vipigo bila sababu. Huko vijijini wanawake ndio hawana usemi kabisaaa, wanachomwa moto shehemu za siri na hawana hata pa kusemea .

Wakati umefika wa kukemea ukatili dhidi ya wanawake, kama umemchoka , humtaki tena mkeo afadhali umrudishe kwao akiwa mzima na sio kilema.
 
Nimejifunza mengi sana kwa experience ile ya maisha,namshukuru Mungu kama mwanaume/kijana ninayejiamini na kujitambua..........nina familia [ndoa rasmi mwaka huu],elimu,kazi na kikubwa upendo na heshima si kwamke wangu tu bali pia kwa wanawake wote....nawapa pole wanawake wote wanaopitia magumu yasababishwayo na sisi wanaume......wazidi kumuomba Mungu wao nakuwa wavumilivu.......haya ni mapito tu,twautafuta mji udumuo!!

WANAUME TUBADILIKE TUACHE UNYANYASAJI WA NAMNA YEYOTE ILE.

mkuu pole sana kwa kuwa na experience mbaya kwa kushuhudia unyanyasaji huo ukiw abado kinda!
sioni sababu ya kumuomba Mungu kuzidi kuwapa wanawake uvumilivu huo - yani wavumilie vipigo na manyanyaso!
Enyi wanaume, ni kwanini mkipata nyumba ndogo basi kwa mkewe wa ndoa mnafanya ubondia? Ndio kwamba mmenogewa saaaana na mapenzi ya nyumba ndogo!? hebu nielewesheni tafadhali!!!
 
Mmmh pole sana najua umeongea Robo kati ya mengi kuna ukatili wa hali ya juu kwenye ndoa, ndio maana juzi nilimwambia mke wangu kitu fulani, sikutaka kumwabia ila nilijikuta tu nimesema...sijawahi kumpiga na sitakaa nimpige ila
 
hakuna cha kuvumilia vipigo aisee.....nawaomba wanaume wenye matabia ya ukatii waache
 
Pole sanaa... yameshapita hayo mkuu...
Ivi ni kabila gani lile wanawake wanapenda kupigwa pigwa... ukikaa siku 3 bila kumpiga anasema humpendi... Ata ivyo hayo ni ya kizamani
 
Nice thread na mtu asiye mheshimu mama yake au mke wake namuona ni mpumbafu tu.

"We have enjoined on man kindness to his parents; in pain did his mother bear him, and in pain did she give him birth" Qur'an(46:15).

A man came to the Prophet and said, ‘O Messenger of God! Who among the people is the most worthy of my good companionship? The Prophet said: Your mother. The man said, ‘Then who?' The Prophet said: Then your mother. The man further asked, ‘Then who?' The Prophet said: Then your mother. The man asked again, ‘Then who?' The Prophet said: Then your father.
 
Hongera na asante sana kwa ushauri mzuri. Yaan ni wachache wanaopitia maisha kama yako na wakawa sio aggressive. Watoto huwa wanajifunza kwa wazazi, kijana akiona mama anapigwa akiwa mkubwa anataka mpiga mkewe kama babaye alivyokuwa akifanya akiamini hiyo ndio correct life style.
 
Pole na hongera kwa kujifunza kutoka kwa baba yako; wengine wakikulia katika mazingira hayo, hujifunza kuwa mwanamke ni wa kupigwa tu! Mungu azidi kukutunza na kukuongoza katika ndoa na maisha yako!
 
ni kweli kabisa maisha ya manyanyaso huwaadhili sana watoto, kuna familia moja tulikuwa majirani mama yao alikuwa akipigwa sana, huwezi amini wale vijana wakewanawatesa sana wake zao ila wale mabinti wa yule baba walikuwa akiomba Mungu awasaidie wasijepitia maisha kama yale na kweli wanasema wao kipigo no! uvumilivu kama wa mama yao ushapitwa na wakati.
 
Unaheri wewe ambaye hukucopy kwa baba maana watoto wengine huathiriwa na tabia za baba zao na kudhani kuwa mwanamke ni wakunyanyasa tu .

Kwa kweli wababa wabadirike, waache ukatiri kwa wamama na watoto!
 
Hakuna mwanaume duniani anayechalaza mke wake bila sababu ya msingi
Baba yako ana haki ya kutoa maelezo yake halafu ndio tuanze ku comment
 
km alisharest in peace naomba ahukumiwe kwa kadri ya matendo yake.
Nachukia sana wanaume wanaopiga wake zao na wale wanaodharau wamama......walaaniwe siku zote na wasifanikiwe kwa kila jambo wanalogusa.
 
Hakuna mwanaume duniani anayechalaza mke wake bila sababu ya msingi
Baba yako ana haki ya kutoa maelezo yake halafu ndio tuanze ku comment

wewe ni Afande Marwa,Chacha AMA mwita, nahici kama umeacha lindo hivi, msalimie Mjeda chaichungu
 
Hakuna mwanaume duniani anayechalaza mke wake bila sababu ya msingi
Baba yako ana haki ya kutoa maelezo yake halafu ndio tuanze ku comment

Kumpiga mke, bila kujali athari kwa watoto ni upumbavu mara mbili.
 
Hakuna mwanaume duniani anayechalaza mke wake bila sababu ya msingi
Baba yako ana haki ya kutoa maelezo yake halafu ndio tuanze ku comment

Unaishi ndani ya jamii au unaishi peke yako kiciwani..? Mie nimeshuhudia mume anarudi uciku wa manane na kuanza kumdunda mke wake.. Kisa chakula kimepoa..! Unaita hiyo ni sababu ya mcingi..?

Anyway kwangu mie nothing justifies kipigo kwa mwanamke.. Absolute nothing..
 
Unaheri wewe ambaye hukucopy kwa baba maana watoto wengine huathiriwa na tabia za baba zao na kudhani kuwa mwanamke ni wakunyanyasa tu .

Kwa kweli wababa wabadirike, waache ukatiri kwa wamama na watoto!

Naamini uzoefu huo utakusaidia kuwa mume na baba mwema kwa familia yako.
 
Back
Top Bottom