TANZIA Baba yake Ally Mayay afariki dunia kwa ajali Tabora

TANZIA Baba yake Ally Mayay afariki dunia kwa ajali Tabora

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,472
Reaction score
14,791
Nyota wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Ally Mayay Tembele, amepata msiba baada ya leo Juni 16, 2025 kufiwa na baba yake mzazi.

Mhasibu wa Chama cha Wachezaji wa Zamani Tanzania (Galacticos), Idd Moshi, amesema kuwa baba wa staa huyo anayejulikana kwa jina la Moshe Tembele, amefariki kwa ajali ya treni baada ya kugongwa wakati akivuka eneo la Chuo cha Reli mkoani Tabora.

"Mzee wetu kafariki leo na taarifa imetolea katika chama chetu cha Galacticos, hivyo mipango ya mazishi itatolewa baada ya Mayay kufika Tabora," amesema na kuongeza.

"Amepata ajali ya treni, hivyo ni kifo cha ghafla ndiyo maana hatuwezi kusema mipango ya mazishi itafanyikaje, ila naamini Mayay akifika ndipo tutakapojua mipango inakwendaje na tutapeana taarifa nyingine zaidi."

Chanzo: Mwanaspoti
 
Back
Top Bottom