Baba wa Neymar amjibu kocha wa Caen

Shadida Salum

Journalist at JamiiForums
Sep 11, 2020
69
104
20210212_164422.jpg

Kocha wa klabu ya Caen Pascal Dupraz amekuwa sababu ya ujumbe wa kukasirishwa kutoka kwa baba wa Neymar ambao umetumwa kwenye mitandao ya kijamii, baada ya Mbrazil huyo kuumia mechi ya Coupe de France Jumatano kati ya Caen na Paris Saint-Germain(PSG).

Baada ya Dupraz kumtaja Neymar kuwa mliaji, baba wa mchezaji huyo amejibu kwa kusema.

"Lazima alie kwa sababu kuna makocha kama wewe, waamuzi wenye kiwango hiki, ligi za uzembe na za kimya, waandishi wa habari wenye upendeleo na waoga katika mchezo huu," .

"Ndio, lazima alie. Lakini kilio changu na kilio cha mtoto wangu, mwenye maajabu kwenye soka, kitadumu usiku mmoja kisha ataamka tena na kujibu changamoto hiyo."

Neymar anatarajiwa kuwa nje ya uwanja karibu wiki nne na hataweza kucheza dhidi ya Barcelona Jumanne ijayo katika Ligi ya Mabingwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom