Dah hizi mada za wazazi bana, anyway, yupo jamaa yangu yeye hakusomeshwa shule, mzee wake alimwambia wewe buree kabisa, acha nisomeshe hawa ndugu zako watakuja wakufae akili zikikuingia,yeye ni wapili kuzaliwa kati ya watoto watano.
Huku na kule, ndugu zake wote waliishia form 4 na kufanya mishe za kutafuta ugali na mlenda.
Yeye na elimu yake ya la nne aliloishia, miaka ya nyuma la nne kulikuwa na pepa, ukifeli unarudia, alipofeli, mzee wake akamwambia ishia hapohapo.
Jamaa alijichanganya mgodini, miaka 12 baadae, jamaa aliibuka na kitu ya maana. Bila kinyongo akarudi nyumbani na kumrekebishia mzee wake nyumba aliyokuwa akiishi na ndugu zake, akawanunulia na coaster yenye thamani ya milioni 45.
Huku na kule, yule mzee akasikika vijiweni akisema mtoto yule angekuwa na akili kama wale wenzake walioenda shule, angefanya mambo ya maana sana. Sasa ananinunulia basi la abiria nilifanyie nn mimi?
Mzee akaliuza kwa milioni 19, na kuwanunulia bodaboda wale watoto walioenda shule ili wapige kazi.
Jamaa kusikia hivyo, kakata mguu, mawasiliano na connections zote na nduguze.
Tukubaliane kutokukubaliana kuwa kuna wazazi na baazazi.